Mkuu Tukiacha ushabiki wa kivyama hata CCM haipaswi kufanya mikutano ya kisiasa kwa sababu mikutano hiyo imezuiwa. Lakini hilo siyo la msingi sana kwangu. Ninachotaka kusema ni kwamba haya mambo watu tusiyachukulie juu juu. Mipasuko katika jamii huanza hivi hivi na isipotafutiwa ufumbuzi mapema, basi tegemea madhara makubwa. Huwezi kujua nini kiko nyuma ya BAVICHA. Ni sawa unamkata mtoto au mke asifanye jambo fulani yeye anasema nitafanya tu. Katika Maisha tujifunze kuvumiliana, mkubwa kwa mdogo, mdogo kwa mkubwa, hayo ndo maisha. Kuna mwanafalsafa mmoja aliwahi kuandika hivi. "There may be times when we are powerless to prevent injustices, but there must never be a time when we fail to protest". Hiki ndicho BAVICHA wanaenda kukifanya. Tunajua CCM wana vyombo vya ulinzi na usalama, na hawata kubali mkutano wao uvunjwe au hawakotayari kusikia kitu hicho kinatokea. Watareact namna yoyote endapo wafuasi wa BAVICHA wataenda DODMA kweli. Sasa nini kitatokea, endapo msuguano kati ya BAVICHA na polisi ukianza. Tutegemee vifo, majeruhi, n.k. Je, itaishia hapo tu? huwezi kujua nini kiko nyuma ya BAVICHA kama nilivyosema mwanzo. Inaweza kuwa ndio mwanzo wa amani ya Tanzania kuisha. Je, Kweli Watanzania tumefikia hatua hiyo? Je, Taifa limekosa watu wenye Busara kusaidia mambo haya yasitokee? Je, huko polisi pamoja kwamba wao ni watu wa kutumia amri wameshindwa kuwaita Viongozi wa BAVICHA wakakaa chini kutafuta suluhu ili kuepusha vurugu? Je huko Chadema kumekosekana watu wenye busara na hekima kuwashauri BAVICHA wasifanye hivyo? Je, CCM haina wazee wenye busara na hekima wanaoona tunakoelekea siko? Tusishabikie mambo ya vyama, tuongee ukweli tu hapa. Hao BAVICHA ni ndugu zetu, rafiki zetu n.k tusikubali kutumika kwa maslahi ya wanasiasa. We must defeat the evil with the triumph of love