Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Yakishindikana hayo manne hapo juu, basi mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Tuwapongeze BAVICHA kwa kuliona hili.!

Malisa G.J
We MALISA wadanganye tu hao BAVICHWA. Watarudi wamevunjwa viuno hao na wala hawatafaidika lolote kwa ujinga wao!! Hiyo posho wanayoifukuzia haitasaidia chochote ukilinganisha na hasara watakayopata. Wahimizeni hao vijana wajishughulishe na mambo ya maana. Muda wa kuzurura wanaupataje?
 
Baraza la Vichaa Chadema (Bavicha) imejitangazia kuchukua Jukumu la kwenda kuzuia mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi inayotarajiwa kufanyanyika Julai 23 mwaka huu, baada kufanya mawasiliano na baadhi ya viongozi wa Baraza hilo hasa ambao akiili zao hazijaweuka bado wanazo kidogo nimegundua yafuatayo: 1, viongozi hao wanakabiliwa na njaa ya kufa mtu maofisini sasa wanatafuta kila aina ya mbinu kutafuta namna ya kuanzisha miradi ya kupiga ruzuku make huko nyuma walizoea operations mbalimbali iliyokuwa ikiwalipa posho nono sasa safari hamna mradi wa kuzunguka mikoani hawapati posho. Kwahiyo safari ya Dodoma ni mradi wa kupiga ruzuku. 2, cdm walikuwa wakipata pesa za wafadhili kutoka jumuiya ya Ulaya kupitia NGOs mbalimbali kwa kisingizio cha Utawala bora na demokrasia sasa kwa wafadhili kutoka Ulaya bila kufanya fujo hakuna pesa kwahiyo wanatafuta kila namna ya mapambano ili kuonesha wanadai demokrasia nchini. Na mwisho hii ni mbinu ya kumchomoa mzee Lowassa pesa hasa baada kutokea fununu kuwa amegoma kutoa fungu na kumwambia Freeman Mbowe ampelekee mahesabu ya pesa aliyotoa wakati anahamia chama icho 2015 zaidi ya 10bilioni zilivyotumika la sivyo chama zitumie pesa zake. Kutokana na huo ukata watendaji ndani ya Bavicha wamebuni njia ya kuhamasisha wafuasi wao kwenda Dodoma ili wakapige posho ndiyo wakaamua kumtumia Ole Sosopi kwakuwa ni Mmasai Lowassa atashawishika kutoa fungi badala ya Mkiti wa Bavicha. Tahadhari Vijana kuweni macho na hizi adaa za Chadema
Pumba tupu......
 
Safi ni vizuri kukumbushana....
BAVICHA wanaonyesha namna ya kua “responsible citizens”
 
Lizaboni unaweza kudhibitisha kuwa mimi ndiye niliyemtuma huyo uliyemuita "kijana aliyemtukana Rais?"
Hamna mikakati,usanii na maigizo havitawasaidia kusonga mbele,siku zinakatika badala ya kufanya kazi kwa nguvu kwenye halmashauri zenu,mnapanga kwenda dodoma kuwasaidia polisi kuzima mkutano wa ccm
Hivi mna akili kweli au mnawafanya wafuasi wenu wajinga?Amiri jeshi mkuu yupo kwenye mkutano,ni askari wa aina gani ataweza kumwambia mkuu wa nchi afute mkutano
 
KAKA BAVICHA WANASHANGAZA SANA. ACHENI DHARAU ZENU. MNAWEZA KUPAMBANA NA AMIRI JESHI MKUU NINYI?
 
CCM ndio chama kilichopewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi. Ni chama dola. Na ndio maana mambo yanayoandaliwa na CCM na Serikali yake yanaenda vizuri. Maonesho ya sabasaba yanaendelea. Yanga wamecheza na TP Mazembe hawajazuiliwa. Kagame kawasili nchini. Ukiwa mtawala maana yake unatawala kila kitu. Nyie Bavicha Nendeni Dodoma mkavunjwe miguu
Sema kilichojipa.
 
We MALISA wadanganye tu hao BAVICHWA. Watarudi wamevunjwa viuno hao na wala hawatafaidika lolote kwa ujinga wao!! Hiyo posho wanayoifukuzia haitasaidia chochote ukilinganisha na hasara watakayopata. Wahimizeni hao vijana wajishughulishe na mambo ya maana. Muda wa kuzurura wanaupataje?
Mimi napenda waende tena kwa wingi ili wakajifunze kwa vitendo maana ya usemi hapa kazi tu.
 
Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Swadakta !
 
Rais alisema siasa zifanywe na wanasiasa mahali waliposhinda uchaguzi na si kufanya siasa mahali ambapo hamkushinda uchaguzi. Lengo likiwa ni kurahisisha watanzania kupima utendaji wa waliochaguliwa utendaji wao ifikapo 2020.

CCM wameshinda ushindi wa jumla mkoani Dodoma. Hivyo wana haki ya kufanya Mkutano hapo Dodoma. Kama Bavicha wamepanga kufanya hayo, watakuwa wanakosea. Godlisten washauri wasifanye hivyo.

>Nawaza kukueleza hivyo Malisa .

CHADEMA kama chama cha siasa kipo kila wilaya ya nchi hii lakini wamezuiwa kufanya mikutano ya siasa ikiwemo ya ndani. CCM pia ni chama cha siasa; haiwezekani wao wakiuke zuio la polisi.
 
UNACHEKESHA SANA KIJANA. UNA MAANA CCM NI SAWA NA CHADEMA? ACHA UTANI WEWE KIJANA. CHADEMA INATAWALA?? INA SERIKALI? ACHA UJINGA WEWE!!

Ngoja nimsaidie kujibu. CHADEMA na CCM ni vyama vya siasa vyenye tofauti nyingi; kama ulivyosema CCM ni chama tawala na CHADEMA ni chama cha upinzani. Lakini ukweli unabaki kuwa vyama hivi vipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa; vyote ni vyama vya siasa vinavyopaswa kuendrshwa kwa mujibu wa sheria hiyo na sheria zingine za nchi.
 
Mimi kuna kitu uwa sielewi hivi kuwa kiongozi chadema lazima utokee kaskazini?

Mwenyekiti Mbowe wa huko huko, mwenyekiti baraza wanawake Mdee wa huko huko.. Jana nimeshangaa huyo mwenyekiti wa Bavicha kavaa kimasai kabisa yani hiki chama na yule dogo aliyekuwa mwenyekiti wa kuchaguliwa ni kama kapinduliwa tayari majukumu yote sasa kapewa mkaskazini mwenzao.

Aisee awa jamaa wakigusa Dodoma hakuna rangi wataacha kuiona watataja koo zao zote za mareale mushi msuya ndossi mpaka ukoo wa mleta mada malisa.
Huku ndio kuna majasiri, na wathubu! Hakuna mamburura kama wewe
 
Kwa kifupi:umezipanga hoja vizuri.

Cha kusikitisha sasa: hatoshangaza pale wasemaji na watetezi wa mkutano mkuu wa CCM watakuwa Polisi wenyewe na

Msajili wa Vyama vya Siasa...
 
Ngoja nimsaidie kujibu. CHADEMA na CCM ni vyama vya siasa vyenye tofauti nyingi; kama ulivyosema CCM ni chama tawala na CHADEMA ni chama cha upinzani. Lakini ukweli unabaki kuwa vyama hivi vipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa; vyote ni vyama vya siasa vinavyopaswa kuendrshwa kwa mujibu wa sheria hiyo na sheria zingine za nchi.
NDIO MAANA CHADEMA INATAWALA NA INA SERIKALI YAKE SIYO?? ACHA NADHARIA WEWE. CCM NI CHAMA DOLA!!
 
NDIO MAANA CHADEMA INATAWALA NA INA SERIKALI YAKE SIYO?? ACHA NADHARIA WEWE. CCM NI CHAMA DOLA!!
Nimesema CHADEMA na CCM vina tofauti nyingi ikiwemo ya CCM ni chama kinachounda serikali; kikatiba hakuna chama dola. Hata kama CCM ni chama tawala bado kinalazimika kufuata sheria za nchi. Hutaki kuelewa kwa sababu umezoea ndiyoooooo?
 
Mlisema chadema mtafanya mikitano kwa nguvu ,lakini hadi leo kimya! mlisema mtaandamana hadi Leo kimya, mlisema mtalinda kura hakuna hata mmoja aliyejotokeza, Leo mmekuja na nyimbo mpya.

Nakuhakikishia hyo tarehe 23 hakuna hata bavicha mmoja atayeenda huko.

NARUDIA; HAKUNA HATA BAVICHA MMOJA ATAYETHUBUTU KWENDA HUKO!!
Labda yawezekana kweli unachosema, sasa wewe unamaoni gani?
 
Back
Top Bottom