Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

The fool who who knows his foolishness is wise at any rate so far.But the fool who thinks himself wise, he is indeed a fool." Dhammapada: 63"
 
Mimi ni mwanachama wa CHADEMA naunga mkono juhudi za UKAWA kutafuta demokrasia ya kweli ila kitendo cha kwenda Dodoma kuzuia mkutano sikubaliani nayo kwa sababu najua jeshi la polisi limeegemea kutetea chama tawala na tukijaribu kuzuia huenda kitavuruga zaidi amani na watu wasio na hatia watapata vilema vya maisha..!! Kwa maoni yangu napendekeza siku hiyo tufanye mikutano yetu ya ndani na hadhara (if possible) pale Dodoma na kwingineko. Iwe droo match......wakituzuia then hio plan B ya kwenda kuzuia mkutano wao ntaunga mkono
 
CCM ni chama Tawala chenye Serikali yake! Acheni kuilinganisha na Vyama Uchwara!
 
Malisa naomba na wewe uende dodoma uungane na hao bavicha sio kuhamasisha humu kwenye mitandao
 
Mambo ya UKAWA hayajawahi dum. Kila Siku ngojera na Tenzi. Hivi kesi mliyofungua mwanza mmeshinda? Nakumbuka Mbowe alisema hataondoka mwanza hadi haki ipatikane
 
Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Yakishindikana hayo manne hapo juu, basi mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Tuwapongeze BAVICHA kwa kuliona hili.!

Malisa G.J
WAKATI MWINGINE CHADEMA MUWE NA AKILI***Hivi kweli mtaweza kuwazuia CCM wasifanye Mkutano wao wa kumkabizi Uwenyekiti wa Chama Rais Magufuli?
Hawa akina Sisopi wasiwafanye Wajinga , Sisopi kwao wana N'gombe zaidi ya 5000 wakiuza 10 tu si wanamweka Wakili wa kumtetea wewe Mwenzangu na Mimi nani atakutetea ??

Nakumbuka Kisa kimoja Kuna Rafiki yangu mmoja pale Arusha cku hiyo aligombana sana na Mkewe kuhusu hari ya Chakula pale Nyumbani kwao kwa kifupi Mdudu njaa alitawala ktka Nyumba yao . Cku hiyo Chadema wanafanya Mkutano usio rasmi ktka Uwanja wa NMC sasa hivi nambiwa Kuna Soko la Samunge , huyu Mshkaji akamwambia Mkewake ngoja nikalete Sukari Uwakorogee Uji Watoto Mama akawa anasubiri kumbe huyu bwana kaenda NMC Kwenye Mkutano. Mama akiwa anasubiri Sukari ghafla anaona Mlango wa Chumba walichopanga kinafunguliwa anamwona Mume wake akiwa Hoi bin taabani Damu zinamvuja Mdomoni Taya limevunjwa na Kitako Cha Bunduki. Waliomleta wakatokomea zao Jamaa akabaki anamtolea Macho Mkewe huku Damu zinavuja Mkewake akamuliza " Hizi Damu zinazokuvuja ndio Sukariiiiii ? Matatizo juu ya Matatizo. Mbaya Zaidi Jeshi la Polis lilisha tangaza Mtu yoyote atakaenda Hospital akiwa na Majeraha lazima Awe na Pf3 kwani Kuna Watu wamefanya Uhalibifu wa Kituo Cha Polisi kwa kuvunja Vioo . Ukweli Matibabu ya huyu Mshikaji Wetu yalikuwa Magumu sana 3week ananyweshwa Uji wa Chumvi na Mkewe hakuna hata Kiongozi Wa Chadema aliyemtembelea kipindi kile.
Sasa na hili mnavyoamasishana Kwenda Dodoma Ili kuzuia Mkutano halali wa CCM angalieni familia zenu zipojepoje.
 
Hizi ni kick za kutafuta headlines kwenye media. Mbona Jana bavicha wamefanya kikao cha ndani na kutoka na tamko la ovyo
 
Hongera sana Bavicha , jukumu la ulinzi ni kwa kila mtanzania .
 
Unawezaje kuzuia mkutano ambao rais yumo? Rais wastaaf wamo? Serikal yote kwa ujumla imo? Kuwepo kwa rais tu kwenye mkutano wa tar 23 ni jawabu tosha kwamba shughuli ile ni ya chama lakini muda huohuo ni ya serikali.. rai yangu tu vijana wenzangu msikubali kupelekeshwa kwenda dodoma kuleta vurugu ilihali mwenye nchi yupo eneo husika,, huo ni uhaini.. kama walimletea vurugu bungen kipind anataka kuhutubia bunge akanyamaza basi msijaribu kuleta vurugu akiwa kikaon,, mjiulizs tu mbona walivyoambiwa watoke bungen cku ya kuhutubia bunge wakatoka c wangebakia basi kama kwel wao ni front line.. vijana wenzangu lalen makwenu msipende kupelekeshwa hovyohovyo mtakuja kuuumia bure.... Msijaribu kuleta vurugu dodoma
Nani aliyekuambia kuwa sehemu akiwepo Rais ni shughuli ya Serikali? Rais akiwa kwenye msiba nyumbani kwao ni shughuli ya Serikali? Rais akiwa ibadani kanisani ni shughuli ya Serikali?
 
CCM ndio chama kilichopewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi. Ni chama dola. Na ndio maana mambo yanayoandaliwa na CCM na Serikali yake yanaenda vizuri. Maonesho ya sabasaba yanaendelea. Yanga wamecheza na TP Mazembe hawajazuiliwa. Kagame kawasili nchini. Ukiwa mtawala maana yake unatawala kila kitu. Nyie Bavicha Nendeni Dodoma mkavunjwe miguu
Hiyo uliyosema sio siasa
 
Strategy ya kijinga hii
Ukikubali CCM wasifanye mkutano basi maana yake unavitambua vitendo na maagizo ya Polisi kuzuia demokrasia kama matendo halali!
Na wamuombe msamaha rais kwa kumuita dikteta uchwara..maana kwa mujibu wa mbowe lile ni tamko la chama.
 
Msiishie kutoa matamko, nendeni kabisa mkawadhibiti ccm kufanya kikao ambacho Mh Rais ni mjumbe. Hakuna rangi mtaacha kuona siku hiyo.
 
Back
Top Bottom