Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Lizaboni unaweza kudhibitisha kuwa mimi ndiye niliyemtuma huyo uliyemuita "kijana aliyemtukana Rais?"
Je. Hamtaki kupimwa utendaji wenu ifikapo 2020!?
Kwa nini hamjikiti katika masuala yatakayowasidia watanzania? Kupitia maeneo mliposhinda himiza watanzania wajiletee maendeleo kwa kujitegemea!!!
Watanzania waleo hawadanganywi tena na masuala ambayo hayalengi kuwakwamua! Watanzania wanataka kujitegemea kwa sasa hawataki kuwa tegemezi ; wanataka kuwa huru kiuchumi na kijamii katika kuenzi utamaduni mzuri wa kiafrika. Jikite huko, pia ongezea na la kukemea maovu nchini kama watu kukwepa kodi, kuendeleza ushetani anaoupigia kelele Makonda, kuhimiza vijana kuwa na tabia njema kwa wakubwa na wadogo pia kwa viongozi wa dini na serikali. Mkijikita huko,Mtakuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu 2020. Tunawapima hivyo mjue!
 
Mlisema chadema mtafanya mikitano kwa nguvu ,lakini hadi leo kimya! mlisema mtaandamana hadi Leo kimya, mlisema mtalinda kura hakuna hata mmoja aliyejotokeza, Leo mmekuja na nyimbo mpya.

Nakuhakikishia hyo tarehe 23 hakuna hata bavicha mmoja atayeenda huko.

NARUDIA; HAKUNA HATA BAVICHA MMOJA ATAYETHUBUTU KWENDA HUKO!!
Somtym tuache ushabiki wakisiasa natufuate logic na taifa kwanza..... Duuuh ii sii akili unafeli
 
Kama mnaona maandamano na mikutano ya kisiasa ina tija sana ,nendeni mkaandamane jimbo la Hai..

Sidhani kama polisi watawazuia
 
Ushahidi ni pale ulipochangisha fedha kumkomboa huyo kijana. Ndio Maana Godbless Lema aliwakataa na kusema haungi mkono jitihada zenu
Naona hujaelewa swali langu. Hakuna uhusiano kuchangisha fedha na madai yako kwamba nilimtuma. Kama kila ninayechangisha fedha kwa ajili yake ninakuwa nimemtuma basi nitakuwa nimetuma watu wengi sana nchi hii. Labda kama hujui nikusaidie taarifa kidogo kwamba huyo uliyedai kamtukana "Rais" si mtu wa kwanza kumchangia. Baadhi ya vijana waliowahi kukamatwa kwa "sheria mbovu" ya mitandao tuliwachangia fedha kuwasaidia ktk kesi zao. Nilifanya hivyo kwa Yericko Nyerere nilifanya hivyo kwa Bob Chacha Wangwe. Wote wawili kwa nyakati tofauti tuliwachangia fedha baada ya kukamatwa na nikawakabidhi ziwasaidie ktk kesi zao. Je hawa nao niliwatuma?
 
Naendelea kushauri..hakuna sababu ya kwenda kuwaingilia hawa watu..ni wazi hakuna sababu yoyote ya POLICE kuzuia mikutano ya CHADEMA ila ni WOGA tu wa SERIKALI YA CCM..
Siku hiyo CHADEMA nayo iitishe MKUTANO kama huo..na ujikite katika kujadili utendaji wa serikali..

Hakuna sababu ya KUCHOMA NYUMBA ili kumuua PANYA..
 
Hahaaa napiga picha ndugu Nepi akifurumushwa na maji ya kuwasha ukumbini huku baba J. akiruka ukuta kukwepa mabomu ya machozi, mzee Wa Tembo atajibanza chini ya meza kuogopa marungu, Moja liwe naye katokea dirishani kusevu uhai wake hahaaa tusubiriii.
 
Nashauri chama kiwakatie bima ya afya/maisha kabla hawajaenda huko msiishie kuwajaza uanaharakati uchwara halafu wakitenguliwa nyonga inakuwa mzigo kwa familia zao najua watakaojitokeza Ni wale wasiojielewa.

Hata kama hoja zao ni za msingi na wanapigania haki lakini nawahakikishia kwa maamuzi waliyochukua watakula kichapo tu na mkutano utafanyika kama kawa.
 
Mlisema chadema mtafanya mikitano kwa nguvu ,lakini hadi leo kimya! mlisema mtaandamana hadi Leo kimya, mlisema mtalinda kura hakuna hata mmoja aliyejotokeza, Leo mmekuja na nyimbo mpya.

Nakuhakikishia hyo tarehe 23 hakuna hata bavicha mmoja atayeenda huko.

NARUDIA; HAKUNA HATA BAVICHA MMOJA ATAYETHUBUTU KWENDA HUKO!!
Hoja yako ni nini zuio ni kwa upinzani tu au?
 
hao bavicha ni waoga balaa, ni majasiro nyuma ya keyboard!! hakuna hata bavicha mmoja atayeenda Dodoma siku hyo
uvccm sijawahi kuwaona zaidi ya majambazi yanayovalishwa nguo za green guard na kupewa silaha. Bavicha wanajulikana
 
Bilakupoteza muda naomba nikuulize mtoa post, hivi jukumu la lakuhakikisha sheria inafuatwa bila shuriti ni lanani kati ya polisi wenyedhamana na wanasiasa ambao niwadau? Pia nivema ukumbuke kuwa sheria inatungwa na kufuatwa kutokana na wakati/matukio kwa jamii husika. Haiingii akilini kuwa hatakama lengo nikusaidia polisi kuishultisha ccm itii sheria,eti nikwakuwakusanya vijana toka sehemu malimbali ktk tz. Hivi adhma inakua nimapambano au kulisaidia jeshi la polisi? Mi nadhani mbunge hakukosea kutoa kauli hiyo ya tahadhali na yenye msaadamkubwa kwa KIJANA yeyote mwenye nianjema kwa taifa na anaejitambua
 
Hilo hawawezi kukujibu. Huyu Malisa ndiye aliyemtuma yule kijana kumtukana Rais kwenye Facebook. Kijana alipohukumiwa kulipa faini, huyu Malisa akachangisha fedha ii kijana atolewe. Nasubiri nini kitatokea
Ukibaka tena nitakuchangia..
 
Strategy ya kijinga hii
Ukikubali CCM wasifanye mkutano basi maana yake unavitambua vitendo na maagizo ya Polisi kuzuia demokrasia kama matendo halali!
Kumbe mnajua vitendo vya polisi kuingilia mambo ya kisiasa sio halali lakini huwa mnajifanya hamnazo.
 
Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Yakishindikana hayo manne hapo juu, basi mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Tuwapongeze BAVICHA kwa kuliona hili.!

Malisa G.J
Waache wakachezee rungu.
Chai wataita kyai
Muhogo wataita muhoho
 
Mimi kuna kitu uwa sielewi hivi kuwa kiongozi chadema lazima utokee kaskazini?

Mwenyekiti Mbowe wa huko huko, mwenyekiti baraza wanawake Mdee wa huko huko.. Jana nimeshangaa huyo mwenyekiti wa Bavicha kavaa kimasai kabisa yani hiki chama na yule dogo aliyekuwa mwenyekiti wa kuchaguliwa ni kama kapinduliwa tayari majukumu yote sasa kapewa mkaskazini mwenzao.

Aisee awa jamaa wakigusa Dodoma hakuna rangi wataacha kuiona watataja koo zao zote za mareale mushi msuya ndossi mpaka ukoo wa mleta mada malisa.
Ni kama unawakumbusha kwenda wakiwa kamili.. Kimya kimya!! U know what I mean
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom