Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Unawezaje kuzuia mkutano ambao rais yumo? Rais wastaaf wamo? Serikal yote kwa ujumla imo? Kuwepo kwa rais tu kwenye mkutano wa tar 23 ni jawabu tosha kwamba shughuli ile ni ya chama lakini muda huohuo ni ya serikali.. rai yangu tu vijana wenzangu msikubali kupelekeshwa kwenda dodoma kuleta vurugu ilihali mwenye nchi yupo eneo husika,, huo ni uhaini.. kama walimletea vurugu bungen kipind anataka kuhutubia bunge akanyamaza basi msijaribu kuleta vurugu akiwa kikaon,, mjiulizs tu mbona walivyoambiwa watoke bungen cku ya kuhutubia bunge wakatoka c wangebakia basi kama kwel wao ni front line.. vijana wenzangu lalen makwenu msipende kupelekeshwa hovyohovyo mtakuja kuuumia bure.... Msijaribu kuleta vurugu dodoma
 
Nakusubiri uje unipeleke Mahakamani
Hakuna mtu atakayekuja kukuchukua samasi itakufuata.

Ulichofanya ni kosa kubwa sana kwanza,

umeidharau mahakama iliyokwisha toa hukumu,
kosa la pili ni kusema uongo na kuiaminisha jamii kuwa kuna watu wanatuma watu kumtukana rais.

Ili Malisa kujiweka kwenye safe side lazima kauli (post) yako ukaikane mahakamani ili mtu mwingine yeyote asitokee kumtukana rais akasingizia katumwa na Malisa.
 
Tunailinda kauli ya Rais kwa gharama yoyote

Subirieni 23/07/21016
Mtaisoma namba zote
Tunaomba polisi watupatie ushirikiano
 
Strategy ya kijinga hii
Ukikubali CCM wasifanye mkutano basi maana yake unavitambua vitendo na maagizo ya Polisi kuzuia demokrasia kama matendo halali!
Mnatudhihirishia kuwa nchi hii chini ya ccm kuna double standard?, kama ndio hivyo nihalali kuwa anachofanya Tulia ,nihalali kuwa anachofanya polisi nimaagizo ya ccm kuukandamiza upinzani,mnadhihirisha kuwa ccm haina jema kwa watanzania,mnatudhihirishia kuwa kila igizo linalochezwa nikutafuta " legitimacy" ya kuhuisha ccm kwenye nyoyo za watanzania?


Ccm ya 1977 haitarudi mioyoni mwa watanzania,mnaongeza uimara Wa chadema nchi hii kuliko ilibyowahi tokea subiri na vita IPO hapohapo Ikulu
Hakika watakuja kwenye meza ya mapatano wakiwa na bandeji na plaster,subiri
 
Ushahidi ni pale ulipochangisha fedha kumkomboa huyo kijana. Ndio Maana Godbless Lema aliwakataa na kusema haungi mkono jitihada zenu
Kwa hiyo huyo kijana alitumwa na wote waliomchangia? Unafahamu maana ya neno kitenzi "tuma"? Dodoma tunakuja,tena tupo vizuri kisheria na kikatiba!!
 
Kwanza atakaye kuwa dodoma ni Rais wa nchi!!!!!! mimi ngoja niuze huu mpunga wangu ili nilipe kodi na kusomesha wadogo zangu, niende kuvunjwa huko ddm nani atakuja kuniona huu si utakuwa mzigo kwa familia tu na hivi niko huku MPUNZE ndan huku!!!
 
Kwa hiyo huyo kijana alitumwa na wote waliomchangia? Unafahamu maana ya neno kitenzi "tuma"? Dodoma tunakuja,tena tupo vizuri kisheria na kikatiba!!
Polisi watakuwa elfu moja vijana watakuwa laki tatu. Hapo patamu. Labda jeshi liitwe kuzuia, lakini polisi naona Kama hawatatosha.
 
Mimi kuna kitu uwa sielewi hivi kuwa kiongozi chadema lazima utokee kaskazini?

Mwenyekiti Mbowe wa huko huko, mwenyekiti baraza wanawake Mdee wa huko huko.. Jana nimeshangaa huyo mwenyekiti wa Bavicha kavaa kimasai kabisa yani hiki chama na yule dogo aliyekuwa mwenyekiti wa kuchaguliwa ni kama kapinduliwa tayari majukumu yote sasa kapewa mkaskazini mwenzao.

Aisee awa jamaa wakigusa Dodoma hakuna rangi wataacha kuiona watataja koo zao zote za mareale mushi msuya ndossi mpaka ukoo wa mleta mada malisa.
Tuoneshe kiongozi Wa juu tangu Nyerere azaliwe hadi kifo Wa ccm alitoka usukumani,Lindi,Mtwara,Rukwa na mikoa mingine

Historia ya ccm nichama cha Wazaramo na watanga
 
Dah aisee mnaumizaga kichwa ukawa.. Hii awamu nyingine take care... Sisi tupo busy tunadai risiti na Kulipa kodi tujenge nchi yetu nyie bado Mnataka siasa...
Kadai risti had I wauza nyanya kama uchumi ulidanganywa kuwa unapanda kwa kuwakandamiza maskini huku waliochukua Madini,Gesi wakilipa chini ya lengo .
 
Ccm haina hati miliki na nchi hii,ni nchi yetu sote.Katazo la mikutano ya kisiasa ni la vyama vyote ikiwepo ccm,this time watawala wataelewa nini maana ya nguvu ya umma,
Tumejipanga kiakili na kimkakati kusaidia katazo la polisi
 
Matamko ya ovyo ovyo mazuio ya kijinga yasio kuwa na tija kwa taifa ndio yataleta machafuko kama polisccm watashindwa kumzibit mpiga sumari sisi tuta wasaidia
 
Ushahidi ni pale ulipochangisha fedha kumkomboa huyo kijana. Ndio Maana Godbless Lema aliwakataa na kusema haungi mkono jitihada zenu
MTU unaenda shule kisha unatoa akili mflisi,nani alikudanganya kuwa mtuhumiwa hana rafiki?

Hata Mandela aliposhitakiwa,Nyerere aliposhitakiwa alihukumiwa kifungo au faini ,lakini wanachama wapenzi waliotaka nchi huru walimchangia akalipa na kuepuka kifungo.


Niraia mwenye fikra mfilisi kama we we utaona mtu / raia yeyote kumchangia mwenzake aepukane na kifungo nikosa.

Au kwa midadi yako ulitaka afungwe?, " usitukane wakunga na uzazi ungalipo," hii ni nchi yetu sote ukitaka kujifunza kamtafute familia ya Dr. Horace Kolimba au waliokuwa Wabunge Wa ccm Leo waisomaje!!!,
 
Nendeni mkavunjwe viuno.
Ila vijana wa Arusha na Kilimanjaro nao waende.
Demokrasia nigarama unaweza kuvunjwa hata na jambaz bora tuvunjwe tuki tetea haki kuliko kupokwa haki hio siku ndio mtajua tofauti ya makamanda na makada
 
KWANINI BAVICHA WANAKWENDA DODOMA??

By Malisa GJ,

Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Viva BAVICHA, Viva Chadema.!

Malisa G.J
 
Kuiruhusu ccm kufanya mkutano wakati serikali imepiga marufuku shughuli zote za siasa, ni kwamba ccm wanataka kuithibitishia umma kuwa nchi hii kuna udikteta uchwara.

Kama kweli ccm wataruhusiwa kufanya mkutano wakati kuna katazo la serikali, Polisi watatakiwa watuthibitishie kuwa CCM siyo chama siasa, bali NGO
Mkuu na wewe utakwenda Dodoma kuwasaidia Polisi kuzuia mkutano!
 
Back
Top Bottom