Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Baada ya jana Baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA) kutoa kauli kuwa watakwenda Dodoma kusaidia CCM kutii sheria bila shuruti, kumetokea mijadala mbalimbali juu ya suala hilo. Wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kinachochea uvunjifu wa amani.

Jana kwenye group moja la Whatsapp Mbunge mmoja wa CCM (simtaji kwa sasa ila akisoma hapa atajifahamu) aliandika "Chadema njooni mtufanyie fujo Dodoma mvunjwe miguu"

Nikamuuliza nani kasema BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya fujo?

Jana nimesikiliza agizo la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Patrick Ole Sosopi hakuna popote aliposema wanakwenda Dodoma kuwafanyia fujo CCM. Alisema wanakwenda Dodoma kuwasaidia CCM kutii sheria bila shuruti kwa kuzuia mkutano wao.

Ili kuweka kumbukumbu sawa ikumbukwe kwamba June 7 mwaka huu Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama VYOTE vya siasa, kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa taarifa za kiitelijensia kuwa kutatokea uvunjifu wa amani.

Tarehe 20 mwezi June, mkoani Dodoma jeshi la Polisi likatoa taarifa mpya kuwa zuio linahusu pia Makongamano na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Kwa kutumia hoja hiyo wakazuia mahafali ya CHASO Dodoma, Kilimajaro, na kongamano la ujasiriamali lililokuwa lifanyike ukumbi wa KKKT Bariadi mjini (japo vyote hivyo vilikua vifanyike kama mikutano ya ndani).

Hata hivyo "Mheshimiwa Rais wetu mwema" JPM, akaongezea kuwa kwa sasa shughuli za siasa zisimame kwa muda ili watu wafanye maendeleo. Shughuli za siasa ni pamoja na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo basi shughuli za vyama vya siasa zilizozuiwa hadi sasa ni Maandamano, Mikutano ya hadhara, makongamano ya kisiasa na mikutano ya ndani.

#MaswaliMuhimu

1. Je CCM wanachokwenda kukifanya kipo ktk orodha ya vilivyozuiwa?

2. Je agizo la Polisi limefutwa?

3. Je agizo la Rais kuzuia shughuli za kisiasa limefutwa?

4. Je walichopanga kufanya BAVICHA ni sahihi?

#MAJIBU

1. CCM wanakwenda kufanya mkutano mkuu wa chama chao. Na kwa kuwa mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku, CCM wamepoteza "legitimacy" ya mkutano huo. Kwa hiyo hadi sasa mkutano huo ni batili (until further notice).

2. Kuhusu agizo la Polisi bado halijafutwa.

3. Kuhusu agizo la Rais bado halijafutwa.

4. Kuhusu kauli ya BAVICHA, hawajakosea. Hii ni kwa sababu kwa maelezo yao hawaendi kufanya fujo. Wanaenda kuhakikisha CCM wanatii sheria bila shuruti.

Nimeona watu wakiuliza eti Polisi wameomba msaada kwa BAVICHA? Swali la hovyo sana hili, na wengi wanaouliza ni wenye uelewa finyu. Lakini majibu yake ni kwamba huhitaji kuombwa na Polisi ili kumkumbusha mwenzio kutii sheria. Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki na wajibu wa kutii sheria na kumkumbusha mwenzie umuhimu wa kutii sheria za nchi.

Kwa hiyo suala la kumkumbusha mwezio kutii sheria ni wajibu wa kikatiba wa kila raia. Haihitaji kuombwa na jeshi la polisi wala jeshi la zimamoto. Kwahiyo BAVICHA wanakwenda Dodoma kutimiza wajibu wao huo kikatiba.

Kuna watu wanafikiri BAVICHA wanaenda Dodoma kufanya kazi za Polisi. La hasha. Hizi ni fikra nyingine mgando. BAVICHA hawaendi kufanya kazi za polisi.

Wanakwenda Dodoma kama raia kwenda kuwakumbusha raia wenzao (wanachama wa CCM) umuhimu wa kutii sheria bila shuruti. Kwa kuwa Rais amezuia shughuli za kisiasa, CCM wanapaswa kuonesha mfano kwa kutii agizo hilo la Rais. Wasipotii basi BAVICHA watasaidia kutii kwa kuzuia mkutano huo, ili kuondoa "double standards" ktk nchi. Hicho ndicho kinachowapeleka BAVICHA Dodoma.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_Nchi?

1. BAVICHA wapongezwe kwa ujasiri wao.

2. Jeshi la Polisi litumie BAVICHA kama kielelezo cha kuwakumbusha raia umuhimu wa kutii sheria bila shuruti.

3. Mkutano mkuu wa CCM uahirishwe.

4. CCM wapewe onyo kwa kujaribu kuandaa mkutano wa kisiasa kinyume na agizo la Rais hali inayoonesha wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

5. Yakishindikana hayo manne hapo juu, basi mikutano yote ya kisiasa iruhusiwe kuanzia leo.

#Nini_Kifanyike_ili_kuisaidia_CCM?

1. Rais afute agizo lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa muda (anaweza kuruhusu agizo hilo liendelee baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

2. Polisi wafute agizo lao la kupiga marufuku mikutano, maandamano na makongamano ya kisiasa (wanaweza kuendelea na marufuku hiyo baada ya July 23, CCM watakapomaliza mkutano wao).

3. CCM waamue kufanyia mkutano wao nje ya nchi.

NB: Kukumbushana umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ni wajibu wa kila raia. Tuwapongeze BAVICHA kwa kuliona hili.!

Malisa G.J


hizo ni fujo mjomba!!!!waliopewa kuwasaidi wananchi kutii sheria bila shurti ni polisi,mahakama,na polisi jamii na siyo mtu mwingine au kikundi kingine!!!kama BVICHA wanaenda dodoma niwashauri wakuu wa chama ngazi za juu na aliyekuwa mgombea wao wa urais wawe mstali wa mbele (front line).wasiwatangulize vijana watoto wa maskini ambao nahisi wengi wao ni la saba au form four /six failures ambao hawajui historia ya mataifa mbali mabali na taifa lao!!!!imagine mtu anamtukana baba wa taifa hivi kweli mtu huyu anajua historia ya taiofa lake na umhimu wa viongozi wake?
 
Labda tujiulize lengo la siasa ni nini. Inaonekaka kana kwamba siasa haihusiani na maendeleo, kwamba siasa ni kampeni dhidi ya chama au vyama. Mimi nafikiri kuwa siasa inahusiana na maisha ya watu ya kila siku.
Kwa hiyo labda tukataze vitu mfano maandamano, kampeni na vitu kama hivi lakini si siasa.
Malisa anasema Bavicha wanaenda DDM kuisaidia CCM kutii sheria bila shuruti. Wakifanya hivyo watashika mabango au watakuwa mabouncer getini? Ni njia ipi watatumia? Bungeni walitumia mbinu nyingi hadi kuziba midomo labda tukijua njia ipi itakuwa vizuri. Kwa maana kwa vyovyote mkutano wa ccm utafanyika.
Kwa kuwa ujumbe umefika labda tamko la kuzuia siasa laweza kutolewa upya.
 
Kama mnaona maandamano na mikutano ya kisiasa ina tija sana ,nendeni mkaandamane jimbo la Hai..

Sidhani kama polisi watawazuia
Unaongea kama mtu anayesikiliza raha ya kukata gogo huku anakula Karanga.. Hujui kusoma? Au unasoma halafu utaelewa kesho? Wapi yanazungumziwa maandamano
 
Mimi kuna kitu uwa sielewi hivi kuwa kiongozi chadema lazima utokee kaskazini?

Mwenyekiti Mbowe wa huko huko, mwenyekiti baraza wanawake Mdee wa huko huko.. Jana nimeshangaa huyo mwenyekiti wa Bavicha kavaa kimasai kabisa yani hiki chama na yule dogo aliyekuwa mwenyekiti wa kuchaguliwa ni kama kapinduliwa tayari majukumu yote sasa kapewa mkaskazini mwenzao.

Aisee awa jamaa wakigusa Dodoma hakuna rangi wataacha kuiona watataja koo zao zote za mareale mushi msuya ndossi mpaka ukoo wa mleta mada malisa.
Ulisoma thread moja inayosema ma dc mbona wengi nikutokea kanda ya ziwa? Ukabila ni mfumo wa ccm ndio maana wengi wenu mnauwimba sana hukj jf
 
Dah aisee mnaumizaga kichwa ukawa.. Hii awamu nyingine take care... Sisi tupo busy tunadai risiti na Kulipa kodi tujenge nchi yetu nyie bado Mnataka siasa...
Umesahau kitu kimoja pia mpo busy naukandamizaji wa Demokrasia nchini
 
Bavichaaa wangejikita kuhoji ni kwa nini Mbowe aliuza chama chao?

Kwa nini Leo miaka 20 chadema haina ofisi??
 
hizo ni fujo mjomba!!!!waliopewa kuwasaidi wananchi kutii sheria bila shurti ni polisi,mahakama,na polisi jamii na siyo mtu mwingine au kikundi kingine!!!kama BVICHA wanaenda dodoma niwashauri wakuu wa chama ngazi za juu na aliyekuwa mgombea wao wa urais wawe mstali wa mbele (front line).wasiwatangulize vijana watoto wa maskini ambao nahisi wengi wao ni la saba au form four /six failures ambao hawajui historia ya mataifa mbali mabali na taifa lao!!!!imagine mtu anamtukana baba wa taifa hivi kweli mtu huyu anajua historia ya taiofa lake na umhimu wa viongozi wake?
Pathetic
 
Mlisema chadema mtafanya mikitano kwa nguvu ,lakini hadi leo kimya! mlisema mtaandamana hadi Leo kimya, mlisema mtalinda kura hakuna hata mmoja aliyejotokeza, Leo mmekuja na nyimbo mpya.

Nakuhakikishia hyo tarehe 23 hakuna hata bavicha mmoja atayeenda huko.

NARUDIA; HAKUNA HATA BAVICHA MMOJA ATAYETHUBUTU KWENDA HUKO!!
kijana mbona upo kama mtoto mdogo mwenzio ametoa analysis nzuri na ushauri juu nini kifanyike ww ina reply utumbo mkiambiwa ccm hamjasoma mnakasirika rudin shule kwanza
 
Back
Top Bottom