Kwanini BAVICHA wanakwenda Dodoma?

Marufuku hiyo ilishaondolewa.Anayetaka kufanya mkutano wa hadhara atoe taarifa kulingana na sheria.
 
Usiseme wakavunjwe miguu boss, kuvunjwa miguu unaona swala la kawaida sana. # Ogopa sana kauli yako hiyo* Yawezekana moja ya watakao vunjwa miguu ni Demu wako hujui wewe.



#mtazamo tuu!
 
Nimesema CHADEMA na CCM vina tofauti nyingi ikiwemo ya CCM ni chama kinachounda serikali; kikatiba hakuna chama dola. Hata kama CCM ni chama tawala bado kinalazimika kufuata sheria za nchi. Hutaki kuelewa kwa sababu umezoea ndiyoooooo?
KAMA UNASEMA CCM NA CHADEMA NI SAWA BASI WAAMBIE HAO BAVICHWA WATIE PUA DODOMA WAONE KAMA WATAFANIKIWA KUZIMA MKUTANO WA CCM ZAIDI YA KURUDI WAKIWA NA VILEMA!!
 
CHADEMA kama chama cha siasa kipo kila wilaya ya nchi hii lakini wamezuiwa kufanya mikutano ya siasa ikiwemo ya ndani. CCM pia ni chama cha siasa; haiwezekani wao wakiuke zuio la polisi.

Kuwepo kila wilaya ni tofauti na kushinda kila jimbo/ wilaya kutokana na matokeo ya uchaguzi. Imarisha Chadema /Ukawa maeneo "tuliyoshinda" kwa kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii kiasi cha kuwawezesha waondokane na fikra tegemezi! Hii "itatusaidia " kuwakabili wapinzani wetu 2020.
 
Tumia akili kufikiri kabla ya kuandika mkuu,usichukulie mambo kishabiki,kwanza kabla ya kubandika maswali yako ungejiuliza maswali yafuatayo;
1.CCM wanakwenda kufanya mkutano wa hadhara au Mkutano mkuu wa chama? (shughuli za kisiasa zilizozuiwa ni public political activities kama maandamano na mikutano ya hadhara-hili liliwekwa wazi bila chenga,)
2.Kama kweli CCM wanakwenda huko kuvunja sheria je kuanzia lini CHADEMA imejibadilisha kutoka kuwa chama cha siasa na kuwa chombo cha kusaidia kulinda uvunjwaji wa sheria?
3.Je ni jukumu la chama cha siasa kulinda uvunjifu wa amani wakati jeshi la polisi lipo na halijakiri kushindwa kazi hiyo?
4.Je Tanzania ina vyama vingapi vya siasa na kwanini ni Chadema pekee kati ya vyama vilivyopo ndio wanakuwa na KIHEREHERE cha kuingilia kazi ya polisi?
Kwa maoni yangu hawana sababu yoyote ya kwenda huko,ila MWENYE HAMU NA AENDE.
 
Kabisa boss! Hawa ndio wanaohitajika, akathibishe bila shaka.
 

Ni sawa ulivyosema. Ulichosahau ni kuwa chama cha siasa kina haki ya kufanya shughuli za siasa hata maeneo ambapo hakikushinda kwa sababu:-
(1) Muundo wa vyama ni wa kitaifa. Huko wilayani kuna uongozi wa chama ambao una kazi ya kujenga/kuimarisha chama kwa nia ya kushinda uchaguzi unaofuata.

(2) vyama vya siasa ni vya kitaifa; si vya kanda. Viongozi wa kitaifa wana haki ya kufuatilia shughuli za kisiasa za chama husika sehemu yoyote ya nchi.
 
KAMA UNASEMA CCM NA CHADEMA NI SAWA BASI WAAMBIE HAO BAVICHWA WATIE PUA DODOMA WAONE KAMA WATAFANIKIWA KUZIMA MKUTANO WA CCM ZAIDI YA KURUDI WAKIWA NA VILEMA!!

Usifikiri wote waliopo humu ni wafuasi wa vyama vya siasa. Hii ndiyo quality ya wasomi wa Tanzania?

Usipende kushabikia vurugu kwa maana amani ikivurugika hakuna atakayekuwa salama. Changia kwa busara ndugu ukitumia vizuri mtandao huu.
 
We uloyepost akili hazikutoshi, chadema wakikutana leo hii mle kwenye NYUMBA ya mtei manyanya nani atawafuata? Kuna tofauti kati ya mkutano ya chama na mikutano ya hadhara kwani mikutano ya hadhara unahutubia hadharan kwa watu na wasio husika wanajua unaongea nn, lakin mkutano wa chama ndan ya ukumbi ni tofauti na unavyosema
 
Kweli nimeamini Mungu kakunyima akili na Maarifa pamoja na wenzako yaani ndiyo umejibu HOJA nzito kwa HOJA GOIGOI hivyo???
Then ukalipwe alafu uchafue khali ya hewa?????????Very shame stomach thinkers...agizo meneja huyu asilipwe leo zaidi ya salala za shingo tu mpaka akili ifunguke na kutumia kichwa na akili kufikiri badala ya TUMBO.
 
Tunaiomba serekali hii ya mh.magufuli itupatie Maelezo ya kina, maana kwa sasa tunashuhudia mivutano kari ya ccm na chadema /
*Tunaomba serekali itueleze ni kwanini ccm inaruhusiwa kufanya mikutano yake sehemu mbalimnali huku chadema kwao ikiwa ni mwiko.
-->>MAELEZO YA KINA YATATUSAIDIA KUEPUSHA SHARI MBALIMBALI,MAANA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI NASHUHUDIA KUTUNISHIANA MISULI, HALI AMBAYO SI AFYA KWA TAIFA LETU.
-->>NASHUHUDIA HATA VYOMBO VYA DOLA VIKITOA MATAMKO TATA.
 
maelezo ya kina upewe ww?? we ushaambiwa hakuna kufanya mikutano ya kisiasa, kama unabisha Fanya!! zingine ulizoandika ni porojo tu
 
maelezo ya kina upewe ww?? we ushaambiwa hakuna kufanya mikutano ya kisiasa, kama unabisha Fanya!! zingine ulizoandika ni porojo tu
***
Kwa maana hiyo kwa ccm ni ruhsa Bali kwa ukawa ni hapana.
..have a little wise..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…