KwANINI BAADHI YA WATU HUWASHA UDI MADUKANI KWAO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KwANINI BAADHI YA WATU HUWASHA UDI MADUKANI KWAO?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Apolinary, Sep 7, 2012.

 1. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ukipita sehemu nyingi hususani za biashara. Utasikia,harufu ya udi kwenye baadh ya maduka hayo japokuwa si maduka yote. Je kuna faida gani inayopatikana pindi utakapowasha udi katika biashara yako au nyumbani kwako?
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni imani kwamba watafanikiwa zaid. Mara nyingi huwa na uhusiano na ushirikina. Hata hivo nadhani kuna dini fulani ina imani za kutumia udi na marashi...
   
 3. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wengine zinawakera! Nadhani labda kwa ajili ya marahamu au imani fulani za kukaribisha madudu eti yanayoitwa ya kiroho sina uhakika lakini. Ni vizuri wangewasha kwenye majumba yao ili wasikere wengine. Naona hilo nalo tutaliweka kwenye katiba mpya!!!
   
 4. m

  mwitu JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  wanadai udi unaondoa nuksi
   
 5. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ....................dini fulani ! funguka na ulete ushahidi ! kwani wale wakina mama wanaojifukizia udi chini ya mapaja ni kwa ajili ya nini ? na wale wanajipaka vitu makwapani huwa ni kuwasaidia nini ?
   
 6. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ..........nuksi ni nini ? husababishwa na nini ? je unaweza kuizuia ?
   
 7. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,213
  Likes Received: 10,558
  Trophy Points: 280
  Huleta harufu nzuri..
   
 8. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 9. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,190
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280

  Zion daughter katupa jiwe Gizani limemdondokea mchizi ally kombo...heh ehe , ukisikia , ng'weee! ujue limempata. ha aha aha kwaheri kwa sasa
   
 10. m

  markj JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  imani ya udi ni kuleta mvuto na na harufu nzuri! sasa sio kila mtu anapenda harfu ya udi, ni sawa na wewe unapulizia perfume kuna kila aina ya perfume na si kila mtu anapenda hiyo perfume, na imani ya perfume pia nikuleta mvuto na imani ya kunukia vizuri. udi umekaaa kiarabu zaidi na perfume zimekaa kizungu zaidi! hazina tofuti hizi kitu, udi kwa kuwa uko kiarabu zaidi na watu wa pwani wnapenda kuutumia kwakuwa ni natural na hauna madhara na perfume si natural zaidi na ina mazara zaidi. sasa kwakuwa watu wanachuki na watu wenye asili hii ya udi ndo mana wanaropoka mabaya na kwa kukuwa wanawatukuza watu wenye asili hii ya perfume ndo mana wanazidhamini sana bila kugundua kuwa zina wazuru. KWA kifupi hata hizo perfume tunazpulizia pia zinakaribisha mashetani na madudu mengine ya ajabu kwani unapopulizia perfume flani kuna zinazofanya upatwe na hisia za kimwili na kuvutiwa na mtu husika sasa hii kitu ni tabia ya shetani ambaye amekariishwa na harufu hiyo kwa ajili ya kuwarubuni wawili nyie, hata hizi airfresh nazo niko kama udi,perfume. hii ni ishu ya utamaduni na asilia ya kimanukato zaidi yankotokea. sasa kama mtu wewe unakereka na udi basi usiingie dukani hapo wewe nenda maduka mengine yamejaa mengi tu, na hata kama hayo mengine unayoenda utakuta unafanya bishara na mtu aliye uchi bila wewe kumuona, au amechimbia mavitu yake humo dukani isiyoyaona, kwa kifupi ushirikiana hauna dini! bali asilimia 99 ya dunia hii watu wanaushirikina, HATA WEWE ULIETUPIA HUU UDHI NINAUHAKIKA USHIRIKINA UNAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, tusidanganyane dunia ya sasa inaendeshwa kishirikina mana hata hao tunaowaamini katika imani zetu za dini kuwa ni viongozi, ndio washirikina namba 1.
   
 11. m

  markj JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
   
 12. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Ni kwa ajili ya masuala ya kimajini tu hakuna lolote
   
 13. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,221
  Trophy Points: 280
  Mkuu umejibu kiutu uzima..big up.
  Sisi wabongo kukicha milawama tuuuu...oh sijui hili sijui yule. Hilo duka si la kwake? Ili mradi hajafukiza huo UDI nyumbani Kwako inakusumbua nini?
  Kazi kuita Wenzao washirikina kumbe wao ndio wanatembea na matunguli na mivichwa ya Paka kwenye mipochi Yao mikubwa. Wabongo bwana!!!! Kutwa kulalama tu. Wewe mleta mada nenda ukaunde Tume Kuchunguza hayo maduka yanayofukiza UDI,halafu upeleke hiyo ripoti kwa Prof. Maji Marefu.
   
 14. P

  Paul J Senior Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiwa wa shetani utamwamini shetani na atakusaidia kwa mashariti ya kishetani lakini mwisho wake utakuwa ni majuto na ukiamini katika Mungu wa kweli atakusaidia kimungu na mwisho wake utakuwa ni wa rehema. Kwa mfano wafanyabiashara nyingi wanaotumia nguvu za giza huwa yule aliyeshikilia hizo nguvu za giza akikosea mashariti au akafariki ghafla bila kurithisha hayo mahetani kwa mwingine biashara hata kama ni kubwa kiasi gani lazima iondoke naye and sometimes hayo mashetani huweza kuwazuru watu wa karibu yake e.g mke na watoto. Believe in True God, he will lead you to success with very simple conditions-Prayers, Repentence & Forgiveness nje ya hapo utakuwa mtumwa wa shetani siku zote
   
 15. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wahindu (tumezoea kuwaita BANIANI) hii ni sehemu ya mambo ya ibada zao za kidini
   
 16. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60


  Mkuu, umezungumza vizuri ila hapo kwenye red ndo umechafua kabisa. Anyways, inawezekana wewe ni mshirikina ndo maana unaamini 99% ya dunia pia ni washirikina. lakini si kweli.
  Ukweli ni kwamba udi ni kwa aijri ya harufu nzuri tu, kama ilivyo kwa perfumes, ila naona kuna watu wamekaa kimtazamo wa kiimani zaidi ndo maana wanuhusisha udi na dini fulani hivi. Inawezekana mtu akautumia kwa malengo mengine kama mtu anavyotumia kisu kuua wakati ni kwa ajiri ya kukatia nyama/nyanya/vitunguu au klorokwini kujiua badala ya kuitumia kujititibia.   
 17. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mapepo.
   
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Buddha huwa wanawasha udi especially wakiwa wanatoa heshima ya mwisho kwa mtu aliyefariki au wakiwa wanawaplease miungu yao
   
 19. j

  joely JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  =uchawi=ushirikina=misukule

  MIE NIKIFIKA DUKANI NIKASIKIA UDI UMEWASHWA HUWA NA MPIGA SHETANI CHENGA NAENDZ DUKA LINGINE
   
 20. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni sababu za ushirikina, ni kwamba majini ya uhusiano mkubwa na harufu fulani fulani.... Udi ni mojawapo kuwantract, kuwapoza nk. matumizi makubwa katika shughuli hizi ni UDI na UBANI! ni ushirikina tuu!!
   
Loading...