Kwanini Azam TV kwenye tangazo lake la afcon linasema ' kuoneshwa Tanzania pekee'?

Maco marco

Member
Jun 10, 2023
98
72
Naomba niingie kwenye swali moja kwa moja..

Hivi kwanini Azam TV kwenye tangazo lake la afcon linasema ' KUONESHWA TANZANIA PEKEE' hii mimi sijaielewa ina maana gani? Naomba kusaidiwa.
 
Hiyo michuano azam tv ataonesha ika ni kwa hapa tanzania tu, hana haki ya kurusha nchi nyingine.
Hapana kwenye matangazo yao wameonesha mpaka ratiba za mechi na wamesema kuwa wataonesha zote kupitia azam tv..... Ina wezekana ukawa sahihi lakini kutokana na tangazo lao bado inafikirisha juu ya lile tamko lao
 
UNauliza swali ukiwa tayari unauelewa wako,
Hapo ndio tatizo
 
UNauliza swali ukiwa tayari unauelewa wako,
Hapo ndio tatizo
Hapana ila yeye alisema kuwa inawezekana ni sabababu wataonesha mechi za Tz pekee mm nikamwambia kuwa kuna tangazo la azam linasema watonesha mechi zote... Hapa tatizo lipo wapi chief
 
Azam anarusha matangazo katika nchi za Tanzania, Kenya na Rwanda (probably na zingine sijazijua bado/sina uhakika). Huko kote anakorusha matangazo anarusha kwa kibali, na kila maudhui (program) yana kibali chake.

Kwenye maudhui ya AFCON, hana kibali cha kuyarusha nchini Kenya na Rwanda (na nyinginezo kama zipo). Hivyo lile tangazo ni mahsusi kwa wateja wake waliopo Kenya na Rwanda kwamba hataonyesha matangazo hayo huko, wajipange kuyaangalia kupitia sources zingine.
 
Hapana kwenye matangazo yao wameonesha mpaka ratiba za mechi na wamesema kuwa wataonesha zote kupitia azam tv..... Ina wezekana ukawa sahihi lakini kutokana na tangazo lao bado inafikirisha juu ya lile tamko lao
Hizo games wataonesha hapa tz tu na sio hizo nchi nyingine. Maana rwanda, kenya na uganda ambako azam tv yupo hawatoona hizo game kuoitia azam tv, hawana kibali kirusha hizo game katika mataifa memgine zaidi ya tz.
 
Back
Top Bottom