Tanzania commecial bank tawi la Pamba Nyamagana Mwanza mna tatizo gani kwenye kutoa mikopo?

danfodio

Member
Dec 2, 2018
80
58
Habari ndugu wana JF.

Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada.

Ni kwamba katika bank ya Tanzania commecial bank zamani ikiitwa Posta bank tawi la Pamba Nyamagana kumekuwa na ucheleweshaji wa kutoa mikopo kwa watumishi na wastaafu wanaomba mkopo kupitia bank hio kwa tawi la Pamba lililopo Nyamagana Mwanza.

Watumishi na wastaafu wamekuwa wanapata taabu kusubiria muda mrefu mpaka kupa mkopo. Wengi wao wanasema kuwa toka kuondoka kwa madam mmoja aitwaye Leticia kwenye kitengo cha mikopo imekuwa tatizo. Sasa hivi yupo jamaa mmoja hivi mtu anajisikia sana nafuatilia wala hajali sana tofauti na mtangulizi wake.

Ndugu meneja wa tawi hili la Pamba okoa jahazi kufuatilia huo issue. Angalia mikopo ulioombwa ina muda gani na kwa nini inachelewa kutoelewa ilhali siku zilizopita ilikuwa ni ndani ya siku moja au mbili mtu anapata mkopo ila sasa ni zaidi ya wiki.
 
Habari ndg wana jf. Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada .
Ni kwamba katika bank ya Tanzania commecial bank zamani ikiitwa posta bank tawi la pamba nyamagana kumekuwa na
kwani lazima tukukopeshe. unajua ni uamuzi wetu kukopesha au kuacha. tulia
kakope kwingine
 
Back
Top Bottom