Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 318
- 662
Hivi karibuni mitandao imeghubikwa na taarifa chafu za aliyekua kiongozi wa kanisa la SCOAN nchini Nigeria, Marehemu TB Joshua.
Watu wengi tulimuamini sana akiwa kama mtumishi wa Mungu. Lakini swali ni kwanini tuumie pale maovu ya mtumishi wa Mungu yanapoibuliwa kwenye jamii?
Inawezekana alifanya na pia inawezekana hakufanya hayo yanayozungumziwa. Tusiwe wepesi sana kutetea na zaidi tusiwe wepesi sana kuhukumu.
Sisi kama wakristo, mafundisho yanaagiza kuweka imani zetu juu ya YESU KRISTO pekee. Hatujaagizwa kuweka imani zetu juu ya watumishi. Watumishi ni binadamu tu nao wana mengi ya kibanadamu ambayo pasipo Roho Mtakatifu huwa wanaanguka kama tuangukavyo wengine.
Nakumbuka mwaka fulani video ya ngono ya mtumishi wa Mungu maarufu hapa Tanzania (sasahivi ni Mwanasiasa) ilivuja mitandaoni. Waumini wake walipambana sana kumtetea.
Waumini tunakua kama vichaa muda mwingine. Tunasahau kwamba huyo ni binadamu tu na ana tabia zake za asili ambazo zinaweza kulipuka muda wowote.
Hatupaswi kuwachukulia watumishi wa Mungu kama malaika. Hata malaika nao walikengeuka (kumbuka habari za Lucifer na malaika wenzake). Kama Lucifer kipenzi cha Mungu alikengeuka, hawa tunaowaita watumishi wao ni nani hata wasianguke katika dhambi?
Wanaosema kwamba kwanini hayakuibuliwa kipindi yupo hai, jibu ni jepesi tu. Kumbukeni taarifa hizi zimeibuka kutokana na shuhuda za wahanga. Isingekua rahisi kwa wahanga kuibuka na kuzungumza wakati mtawala wao alikua bado yupo.
TB Joshua alikua na nguvu na mamlaka hata kwa Serikali za nchi. Kwa Nigeria kanisa lake ni moja ya kivutio cha kuvuta watalii. Halafu unadhani ungeweza kusimama ukaongea mambo hasi juu yake serikali zikuache tu?
Jitihada za kufichua haya hazijaanza kufanyika 2024. BBC walijaribu kumtafuta mmoja wa kiongozi wa sasa wa kanisa la SCOAN na waliishiwa kujibiwa kwamba “Tuhuma kama hizo juu ya TB Joshua zipo tangu zamani na hakuna aliyeweza kuthibitisha”
Kwa kumalizia, kama nilivyoeleza awali. Hatuna uhakika kama alifanya au hakufanya. Pengine inaweza kuwa agenda tu ya kuliangusha kanisa. Ila katika haya yote tujifunze kwamba tunapaswa kumuamini YESU KRISTO pekee.