Albosignathus
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 4,898
- 1,051
- Thread starter
-
- #41
si kweli kuwa waislam hawaruhusu mtu asiye kuwa muislam aingie msikitini. mtu yoyote anaruhusiwa kuingia msikitini bila kujali dini yake ili mradi afate masharti kama vile kuvua viatu na kwenda kutia udhu. sema akishaingia msikitini haruhusiwi kusali hadi asilimu. ACHA KUKALILI NDUGU.
Papa benedictor akiwa anasari masjid.
wanaolumbania dini huwa ni watu maskini tu kama akina ponda ila viongozi wote wakuu wa hizi dini beyond the scene together their sailing in one boat......Papa benedictor akiwa anasari masjid.
Ungeuliza kwa nini hakuna Kanisa Saudia yote wakati msikiti upo Vatican ungeeleweka zaidi
Ndugu wana JF.Ningependa kupata ufafanuzi kwa wale wanaojua kwamba kwanini Papa huingiaga msikitini ilhali yeye sio muislam na ukizingatia kwamba waislam hawaruhusu mtu yeyote asie muislam kuingia msikitini???
si kweli kwamba mtu asiye muislamu harusiwi kuingia msikitini,unaingia vizuri tu,ukiona mtu ana mkataza asiye muislam kuingia msikitini ujue elimu yake ndogo na aufaham uislam,cha msingi afate taratibu za pale,ila hataswali mpaka aamini,labda aswali kwa taratibu za dini yake,ndugu zangu hili jambo lilishatokea enzi za mtume,walimfata watu wasio waislam wakamkuta msikitini,wakawa wanafanya mazungumzo,ulipofika mda wa ibada yao wakamuomba waswali,akawaruhusu.
waislam wa nchi za mbele kidogo wanaustaarabu lakini wa hapa bongo huwa wanatamani dunia hii wengekua peke yao ila bahati mbaya allah wao anaendelea kuproduce makafiri........tafakari
Mkuu kanisani ni kwa ajili ya wote ila msikitini si unajua lazima uwe muislam,sasa nashangaa papa yeye aliruhusia akaingia na akapiga dua na waislam japo sio muislam.
sheikh naye ruksa kuingiaa kanisani mbona.....wenyewe tu wana gwaya
Kukaa mbele katika uislam sio kama ndio utukufu ama cheo la hasha,kwan hata imamu akichelewa akikuta ibada anakaa nyuma{safu ya nyuma}Lakini papa aliingia na hakusilimu na AKASWALI tena akakaa mbeleee.Unasemaje hapo kwenye picha????
| Papa Benedict XVI | Sunday, May 10, 2009 5:39 AM Papa Benedict XVI ameingia na viatu vyake msikitini alipotembelea msikiti mkubwa wa nchini Jordan uliopo katika jiji la Amman. |
Nakumbuka marehemu Pope John Paul wa pili aliingia msikitini alipotembelea nchi ya Jordan na Uturuki.
sioni uajabu wowote...sana saana watu wnakuwa wana attitude tofauti!!
Ni kama kuonesha Amani kwa wote