Kwanini Askari wetu hubeba silaha za kivita!!

Kwanini Askari wetu hubeba silaha za kivita!!

Tunazungumzia hizo silaha kwenye mikutano ya siasa ambako hakuna majambazi. Ni mjinga gani anayetaka Askari Polisi aende kupambana na majambazi akiwa na Bakora mkononi?

Hahahaha kwny mikutano ya hadhara sijajua utaratibu wao waliojiwekea. Ila wabebe tu hujui muda wa saaa masasi yatarindima
 
Huko Liberia na Rwanda mpaka mapanga yaliyopotumika unajua ni kwa kiasi gani bunduki na Askari walikwishatumika?
Hiyo ni mada mpya sasa. Fananisha hivyo vijiti vya askari wako pichani na hiki kidude nilichobeba utambue ipi ni ya kuzuia wezi wa kuku na ipi ya kivita
 
Kwanza umedanganya watu....

Ni lini ushawahi kuona police kabeba Light machine gun.....kwenye Mikutano yoyote ile..???

Kutokana wimbi la ujambazi uliojitokeza ndio umepelekea matumizi ya silaha kama smg...Ak47....Uzigun....smg s'cz...kuanza kutumika sehemu mbali mbali lakini sio kwenye mikutano

Hata mimi nimepatwa na wasiwasi , labda mleta maada anaweza kutusaidia, kwa mfano ni mkusanyiko au mkutano gani ambao ameona askari wamebeba LMG, LMG ni silaha kubwa Sana ya kivita, hata matumizi yake wakati mwingine huhitaji watu wawili kwa wakati mmoja kuweza kuitumia...... Ni jambo la kushtua kusikia silaha Kama hiyo hubebwa na askari kwenye mikusanyiko kama mtoa maada anavyotuambia.
 
Ngoja aje mkuu......au huyu Mzee ni mpigajia nini???_

Anataka askar watumie SAR....au short gun...katika shughuli zao mbali mbali..kama ma bank ili ule mtandao wake ufanye kazi vizuri..

Ninamashaka na mtoa mada..Afande sirro njoo uku..
 
Majambazi wa siku hizi wanatumia Silaha za kivita na sio rahisi kuweza kujua kama kati ya hawa raia kuna Silaha ya hatari
Ni sawasawa na wewe unapojenga nyumba imara lkn unaweka pia na fence, jiulize ni kwanini?
 
Jambo kutojulikana kwako haimaanishi kwamba halipo. Mimi nimeshawahi kwa macho yangu hapa Iringa, kuona kwenye Mkutano wa Msigwa Polisi walikuwa wameweka LMG kwenye Kebini ya One ten yao nikajiuliza kwani na wao wana LMG, ya nini hasa?
Hakuna kitu kama hicho.....
 
Wanazishika kuringishia nchi jirani waone nao wanazo, lakini jambazi mwenye panga anawamaliza na kuondoka na hizo silaha zao za kupigia picha.
Hizo zilizofungwa na mipira, vipi hiyo mipira ikifunguka si ndo jangili anawakamata kama watoto.
 
Subject wanawaza kubadilika na kuwa aggressive kupitiliza,
Nafikili ni kwa kujilinda mwenyewe binafsi na kuwalinda wenzao endapo watashambuliwa na wakajilidhisha hakuna option nyingine rafiki ya wao kujilinda isipokuwa matumizi ya silaa ya Moto.

Remember international rules of engagement and use of firearms.
Tatizo polisi wetu weñgi huwa hawafuati utaratibu, hata kama hakuna sababu utasikia risasi zinarindima huku teargas zipo.
 
View attachment 331497
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?

nchi zilizoendelea ni nadra sana askari kuonekana na silaha za kivita..kumbuka hizo nchi pia raia na viongozi wao wako highly civilizid than us..

pia kumbuka nchi zetu japo raia hawamiliki silaha lakini mipaka yetu iko wazi na silaha zinaingia kwa sana na zinatumika katika matukio ya uhalifu. katika maeneo ya kisia askari kuonekana na silaha ni matokeo ya kutoaminiana! kitu ambacho hatujui waafrika ni ustarabu...muoneka wa silaha ni kama vitisho..
 
Magazine zenyewe wamefunga na mpira ,hatari tupu tu

hizo magazine zimebebena..kwa maana ziko mbili ya kwanza ikiisha anageuza ya pili..hiyo inasaidia kupunguza muda wa kupakia risasi magazine iliyoishiwa..mind you kupackia risasi need time..so kama mapigano ni makari hiyo njia ni nzuri
 
View attachment 331497
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?
Ndio serikali zetu zisizo na upeo polisi shurti watembee na bastola silaha za kivita hutumika pale wanapokutana na majangili wana silaha kali. Na hakika Polisi hawapendi kutembea na mitutu basi tu hawana uwezo wa kubadilisha mambo. Lakini nashukuru hizi forum kwa sababu hili ni wazo linaweza kupelekwa kwa wahusika
 
marekebisho ni kufungwa kwa mpira. Zero brain
Unapokosoa kwanza jua sababu ya wao kubeba magazine hivyo, badala ya kuweka kwenye mifuko ya shati na suruali, ama mapochi ya kubebea risasi. Maana hivyo vipo lakini kwanini hawavitumii, ukipata jibu kosoa alafu uwape ushauri wangetumia njia gani bora ya kubeba magazine tatu au mbili za risasi. Na hata ndugu zetu waliopigana vita ya uganda walichagua njia hii kubeba magazine tatu au zaidi, ila walikua na kombati zenye mifuko mikubwa ya kutosha kubebea magazine, na mapochi ya risasi na mabomu pamoja na begi kubwa la mgongoni, sasa kwanini wanafanya hivi tavuta jibu uone inawasaidia nini kufanya hivyo, alafu toa ushauri wako, sio kukosoa tu.
 
Hata mimi nimepatwa na wasiwasi,
wewe endelea kuwa na wasiwasi, lakini kama imewezekana kuwa na vifaru mitaani huko zanzibar unashangaa LMG. Niliposema LMG nilikuwa najua ni nini ninachosema na nina hakika nayo na ninajua jinsi LMG inavyotumika iwe ile ya kizamani na hizi za kisasa. Mimi pia nilipatwa na wasiwasi kwenye mkutano ule kuina silaha nzito kama ile imetundikwa juu ya Gari ikiwa na Mkururo wa risasi!!
 
View attachment 331497
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?

Nenda jeshini ukajifunze maswala ya kiulinzi kabla hujaposti vitu vya ajabu.Unaonekana hata mgambo hujapitia.silaha ndogo kabisa ni sr na inafuatiwa na smg na zote ni silaha za kivita sasa wewe ulitaka wabebe magobole ya kuulia wanyama?
 
Unataka kusema haijawahi kuonekana Polisi wakiwa na silaha hizo. Hoja yako ni nyepesi mno. Huko zanzibar magari ya deraya yanaranda randa mitaani kwa ivo unataka mpaka twende kuuliza jeshini kwamba magari ya deraya ni zana za kivita au la?
 
Back
Top Bottom