Kwanini Askari wetu hubeba silaha za kivita!!

Niliwaona juzi pale mwenge wameshika yale mabunduki ya vita vya kwanza vya dunia yenye kutumia gun powder na mkisu mkubwa mbele...nikasema ok wanatuzoesha taratibuu tu hadi kwenye majegeja na vifaru..!!
 
Hakuna unachokijua mkuu, ila ndiyo hivyo kwa vile tumeumbwa kukosoa tuendelee kukosoa hata taaluma tusiyoijua.
Ni kweli mimi sijasema najua kitu Mkuu ,nimeshangaa tu hiyo mipira ya manati
Hongera mwana taaluma
 
View attachment 331497
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?
 
Simaanishi mimi ni mwana taaluma, ila watanzania tumezoa kukosoa taaluma za watu, hatakama hatujui chochote kwa fani hiyo. Wewe umesema kufungia ile mipira ni hatari, ukiulizwa hatari kivipi huna majibu. Kuna vitu vimetengenezwa viwandani huko, ila ukiihitaji uvitumie kwa uimara au kudumu muda mrefu, lazima uvifanyie marekebisho, ikiwezekana unang'oa kilichotengenezwa kiwandani unaweka cha kwako, Ila samahani mkuu kama nimekukwaza.
 
Wanazishika kuringishia nchi jirani waone nao wanazo, lakini jambazi mwenye panga anawamaliza na kuondoka na hizo silaha zao za kupigia picha.
Kwani panga sio silaha? mkuu hata pen ni silaha na inaua ukiwahiwa.
 
Nimeamua kusema ili siku nyingine asirudie
Nisirudie kitu gani? Kwani unadhani dunia hii inaendeshwa kwa mtazamo wa mtu mmoja? Kama wewe unaona ni suala la kipuuzi lazima urudi ukaangalie orodha yako ya vitu vya kipuuzi ina nini na nini. Kuna watu wanaona kuamini kwamba kuna mungu ni upuuzi!!
 
Simaanishi mimi ni mwana taaluma, ila watanzania tumezoa kukosoa taaluma za watu, hatakama hatujui chochote kwa fani hiyo. Wewe umesema kufungia ile mipira ni hatari, ukiulizwa hatari kivipi huna majibu. Kuna vitu vimetengenezwa viwandani huko, ila ukiihitaji uvitumie kwa uimara au kudumu muda mrefu, lazima uvifanyie marekebisho, ikiwezekana unang'oa kilichotengenezwa kiwandani unaweka cha kwako, Ila samahani mkuu kama nimekukwaza.
Hapana mkuu hujanikwaza ni kweli kabisa kuna vitu vimetengenezwa viwandani ili kuendana na mazingira lazima ubadilishe kidogo ,nisaidie kufanya modification kwenye matairi ya gari yawe meupe
Hatari ya mpira wenyewe ni kwamba unaweza kukatika ukajikuta umedondosha Magazine sasa sijui itakuaje
 
Shule zenu za kata taabu kweli...
 
Wakati mimi nasoma wewe ulikuwa haujazaliwa ndugu yangu!!
Kwanza umedanganya watu....

Ni lini ushawahi kuona police kabeba Light machine gun.....kwenye Mikutano yoyote ile..???

Kutokana wimbi la ujambazi uliojitokeza ndio umepelekea matumizi ya silaha kama smg...Ak47....Uzigun....smg s'cz...kuanza kutumika sehemu mbali mbali lakini sio kwenye mikutano
 
View attachment 331497
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?
AK47 haitumiwi na mtanzania
Pia LMG ni nadra sana kuonekana kwa polisi
 
Hapana mkuu hujanikwaza ni kweli kabisa kuna vitu vimetengenezwa viwandani ili kuendana na mazingira lazima ubadilishe kidogo ,nisaidie kufanya modification kwenye matairi ya gari yawe meupe
Hatari ya mpira wenyewe ni kwamba unaweza kukatika ukajikuta umedondosha Magazine sasa sijui itakuaje
Si jambo linalotokea mara nyingi, ndiyo maana hawatafuti njia mbadala, hiyo itakua kama tairi la gari kuchomoka gari huku gari ikiwa kwenye mwendo, dereva si kitu anachotarajia kutokea, ingawa chaweza kutokea. Uncle Ben.
 
Si jambo linalotokea mara nyingi, ndiyo maana hawatafuti njia mbadala, hiyo itakua kama tairi la gari kuchomoka gari huku gari ikiwa kwenye mwendo, dereva si kitu anachotarajia kutokea, ingawa chaweza kutokea. Acle Ben.
Sawa Mkuu mimi niliona ni tatizo kwa sababu kwa vyovyote vile matumizi ya hizo silaha ni kwenye matukio hatarishi na lolote linaweza kutokea ndio maana nikaona mimi kufunga Magazine kwa mpira sio salama ,wala sikua na nia mbaya kama ulivyo nichukulia kwamba kazi yetu watanzania ni kukosoa vitu tusivyo vijua
 
Kwanza umedanganya watu....

Ni lini ushawahi kuona police kabeba Light machine gun.....kwenye Mikutano yoyote ile..???
Jambo kutojulikana kwako haimaanishi kwamba halipo. Mimi nimeshawahi kwa macho yangu hapa Iringa, kuona kwenye Mkutano wa Msigwa Polisi walikuwa wameweka LMG kwenye Kebini ya One ten yao nikajiuliza kwani na wao wana LMG, ya nini hasa?
 
Unataka wabebe gobore au short gun? Watauliwa kama kuku, majambazi wanazo silaha za kivita plus mabomu. So nadhani ni vema polisi wakawa advance zaidi ya majambazi
 
Angalia vzr, wamebeba magazine mbili mbili... Kikawaida moja ndio inawekwa kwenye bunduki hiyo nyingine wameifunga(kuziweka pamoja) in case ya kwanza ikiisha unapachua na kupachika nyingine,
kwani amna magazine pocket hadi wazifunge kwa mpira??
 
Unataka wabebe gobore au short gun? Watauliwa kama kuku, majambazi wanazo silaha za kivita plus mabomu. So nadhani ni vema polisi wakawa advance zaidi ya majambazi
Tunazungumzia hizo silaha kwenye mikutano ya siasa ambako hakuna majambazi. Ni mjinga gani anayetaka Askari Polisi aende kupambana na majambazi akiwa na Bakora mkononi?
 
Simaanishi mimi ni mwana taaluma, ila watanzania tumezoa kukosoa taaluma za watu, hatakama hatujui chochote kwa fani hiyo. Wewe umesema kufungia ile mipira ni hatari, ukiulizwa hatari kivipi huna majibu. Kuna vitu vimetengenezwa viwandani huko, ila ukiihitaji uvitumie kwa uimara au kudumu muda mrefu, lazima uvifanyie marekebisho, ikiwezekana unang'oa kilichotengenezwa kiwandani unaweka cha kwako, Ila samahani mkuu kama nimekukwaza.
marekebisho ni kufungwa kwa mpira. Zero brain
 
Back
Top Bottom