Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,410
- 38,699
Silaha kama hizi zilizobebwa na Askari hawa wa Jeshi la Polisi nchini mwetu zimekuwa ni zana za kawaida kabisa kubebwa na Askari polisi kwenye mikusanyiko ya watu wengi tena raia wasio na Silaha.
Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Askari wetu hao wabebe silaha za kivita dhidi raia wasio na silaha yoyote? Kwa mfano kwenye mikutano ya siasa kuna sababu gani ya kubeba silaha za kivita. Kwani polisi huwa wanahisi kuna jambo gani la hatari litakalotokea na kuhitaji ujibizanaji kwa kutumia SMG, LMG au AK 47?