Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,054
Kuna "contradiction" ya hili neno amani namna inavyotafsiriwa na hawa watawala wetu, wakati mambo yanayoendelea hapa nchini, mara Kwa mara tunawasikia watawala wakirudia msemo huu wa kuwaomba watanzania tutunze amani yetu tuliyojaaliwa na Mungu Kwa nguvu zote, wakitolea mifano wa nchi nyingine hata za jirani, kuwa amani huko nchini kwao imetoweka.
Hivi hiyo amani Gani iliyopo hapa nchini wanayoongelea hao watawala wetu, wakati hapa nchini, tayari amani ishatoweka Kwa watu kutekwa na baadaye kuuawa kama ilivyotokea Kwa kiongozi wa CHADEMA,Ali Kibao kuuawa kinyama na huyo Rais wetu, hataki kuunda Tume huru ya kuchunguza kifo hicho chenye utata mkubwa??
Hivi amani Gani wanayoongelea hawa watawala wetu, wakati Rais wetu hataki kuunda Tume huru ya kuchunguza, kutekwa viongozi wa CHADEMA, akina Soka, ambao mpaka sasa hawajulikani walipo?
Kwa hiyo Kwa tafsiri yangu, tayari amani hapa nchini, ishatoweka na tunapaswa nchi yetu tuwekwe kundi Moja na hizo nchi ambazo amani kwao ilishatoweka kitambo!
Iwapo tu nchi yetu itakuwa inataka amani hiyo irejee, basi Rais wetu anapaswa aunde Tume huru haraka iwezekanavyo ya kuchunguza matukio haya Ili watu hao wafahamike na kuburuzwa Kwenye vyombo vya sheria na tuwajue ni kina nani hao wanaohusika na matukio hayo ya kikatili sana
Vile vile ni lazima, Waziri wa Mambo ya ndani, Yusuph Masauni na mwenzake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camilius Wambura, wajiuzulu mara moja Kwa kushindwa kuwalinda raia na Mali zao, ambao ni wajibu namba Moja ya majukumu yao.
Niwaambie hao viongozi niliowataja kuwa kulinda amani ya nchi yetu hakutokani na Jeshi la Polisi, kufanya doria katika Jiji hili la kibiashara la Dar, Kwa kurandaranda Kwa askari hao kuwa na silaha za kivita na magari ya washawasha, Bali tunawataka wao watulinde na hao watu wanaotambulika kuwa ni watu wasiojulikana Ili wasituteke tena na kutuua kinyama na hapo hapo, hao Jeshi la Polisi, pamoja na vifaa vyao vya kisaasa walivyo navyo waendelee tu kutuambia kuwa hao watu wasiojulikana, wameshindwa kuwabaini ni wakina nani??😳
Soma Pia: