Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,768
- 37,585
Kuna tetesi zimezagaa mkoani Kilimanjaro zikidai kuwa Jeshi la Polisi wilaya ya Mwanga limetoa taarifa isiyo sahihi kuhusu kufukuzwa kazi kwa askari wanne wa barabarani waliohusishwa na tukio la rushwa nono iliyopelekea wao kufuta picha za kwenye kamera ya barabarani ya kurekodi matukio ya mwendo kasi kwa magari, tukio la tarehe 30/5/2024. Baadhi ya wananchi wanadai kuwa, kiuhalisia hakuna hata askari mmoja aliyefutwa kazi bali askari wote hao wamehamishwa maeneo mengine baada ya kupewa likizo!
Sasa ili kuondoa sintofahamu hizi na kulinda hadhi ya jeshi letu la Polisi mbele ya jamii, tunaomba jeshi la Polisi lijitokeze upya na kufanya haya:
1. Litoe orodha yenye majina, jinsia na vyeo vya askari hao.
2. Picha za askari hao ziambatanishwe.
Hili likifanyika litajenga imani kwa jeshi letu la Polisi katika jamii na pia litakuwa limewalinda raia dhidi ya vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinaweza kufanywa na askari hao waliofukuzwa kwa mwamvuli wa jeshi la polisi.
PIA SOMA
- Askari wanne wafukuzwa kazi kwa kufuta picha za kwenye kamera ya mwendokasi