Kwanini amri ya kunyongwa ni mpaka Rais apitishe?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,200
12,692
Rais anajua nini kuhusu masuala ya sheria na adhabu? Rais anataka kuonekana mwema kwa raia wake, na rais anayenyonga hawezi angaliwa vizuri sana. So rais anayejielewa hawezi kunyonga mtu. Kwanini mahakama ikisema isiwe mwisho kama zilivyo adhabu nyingine?

Kuna ulazima gani wa Rais kupitisha adhabu ya kunyongwa?
 
Kwanini mahakama ikisema isiwe mwisho kama zilivyo adhabu nyingine?
Nadhani jambo la muhimu zaidi lipo hapa, kuna kila sababu bunge kurekebisha hii sheria swala la adhabu ya kunyonga mpaka kufa kwa watenda makosa yenye kuhitaji hii adhabu halipaswi kuwa uamuzi wa Rais.

Ni lazima mahakama ipewe mamlaka kamili ya kuwa mwanzo na mwisho wa kuamua adhabu ya kunyongwa kwa mtenda makosa na sio chombo kingine nje ya mahakama.
 
Adhabu ya kifo huwa kama haipo tu kwetu
Na ingekuwa hukumu ya mwisho na tarehe anaitoa hakimu basi naona wengi wangekuwa wamenyongwa

Mahakimu wengi wala rushwa
Imagine wakuu wa Wilaya na Mikoa kuambiwa unaweza kumsweka mtu ndani uliona walivyokuwa wanaonea watu na Ubabe wa kupitilza

Sasa hiyo nguvu wakipewa na Mahakimu kuuwa wengi watanyongwa kwa kuonea acheni wawafunge tu inatosha adhabu hiyo ingawa wengi wameonewa
 
Nadhani jambo la muhimu zaidi lipo hapa, kuna kila sababu bunge kurekebisha hii sheria swala la adhabu ya kunyonga mpaka kufa kwa watenda makosa yenye kuhitaji hii adhabu halipaswi kuwa uamuzi wa Rais.

Ni lazima mahakama ipewe mamlaka kamili ya kuwa mwanzo na mwisho wa kuamua adhabu ya kunyongwa kwa mtenda makosa na sio chombo kingine nje ya mahakama.
Kumbuka magereza hayapo chini ya Mahakama bali yapo chini ya Serikali, na mkuu wa magereza ni mteule wa rais, na rais ndiye anatakiwa atoe amri ya kunyonga ndipo magereza watekeleze.

Kwa hiyo usidhani kwamba magereza na rumande vipo chini ya Mahakama.
 
Kunyonga hadi kufa kwa lugha ngumu maana yake ni kuua.

Kumuua mtu siyo jambo dogo hata kidogo, na ndiyo maana rais anahusishwa.

Hata hao majaji na mahakimu wanaohukumu watu kunyongwa huwa hawapendi na hata kalamu wanazoandikia wakati mwingine huzitupa baada ya kazi.

Ni sheria tu ila ianaumiza katika kuitekeleza na ndiyo maana marais wanakwepa kusaini.

Hivi wewe na akili zako unaweza kusaini hati ya kumuua mtu?
 
Kumbuka magereza hayapo chini ya Mahakama bali yapo chini ya Serikali, na mkuu wa magereza ni mteule wa rais, na rais ndiye anatakiwa atoe amri ya kunyonga ndipo magereza watekeleze.

Kwa hiyo usidhani kwamba magereza na rumande vipo chini ya Mahakama.
Sheria namba ngapi inasema hivyo ?
 
Rais anajua nini kuhusu masuala ya sheria na adhabu? Rais anataka kuonekana mwema kwa raia wake, na rais anayenyonga hawezi angaliwa vizuri sana. So rais anayejielewa hawezi kunyonga mtu. Kwanini mahakama ikisema isiwe mwisho kama zilivyo adhabu nyingine?

Kuna ulazima gani wa Rais kupitisha adhabu ya kunyongwa?
Rais haendeshi mashtaka yeye husaini tu kibali kwa mamlaka na kwa mujibu wa sheria.. Mambo mengine yote yanakuwa yameshafanyika huko chini
Labda rais aamue kuunda 'killing squad' kwa mtazamo wake mwenyewe
 
Rais anajua nini kuhusu masuala ya sheria na adhabu? Rais anataka kuonekana mwema kwa raia wake, na rais anayenyonga hawezi angaliwa vizuri sana. So rais anayejielewa hawezi kunyonga mtu. Kwanini mahakama ikisema isiwe mwisho kama zilivyo adhabu nyingine?

Kuna ulazima gani wa Rais kupitisha adhabu ya kunyongwa?
Ndo maana Magu kipindi kile cha kuziia safari alisema kuna mzizi umeenda chini zaidi ya mingine
 
Back
Top Bottom