ndy wapo ila hawaishi duniani kuishi milele hapa hapa dunian hakuna maana utapoteza uwapendao wote unabaki peke yako unapata raha gan?
Kuna Uzima wa Milele baada ya kufa, Kwa maana ya Ufufuo na Watakatifu kuishi Milele.
Pia Kuna Uzima wa Milele wa kutokuonja Mauti Kwa baadhi ya Watu.
1 Wakorintho 15:51-54
51. Sikilizeni, nawaambia siri: sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52. ghafla, kufumba na kufumbua, tarumbeta ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa tarumbeta italia, wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53. Kwa maana hali hii ya kuharibika lazima ivae kutokuharibika, na hali hii ya kufa lazima ivae hali ya kutokufa. 54. Kwa hiyo, wakati kuharibika kutakapovaa kutokuharibika, na mwili wa kufa utakapovaa hali ya kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia, “Kifo kimemezwa na ushindi .”
Ukiangalia kwenye Biblia hapo, Mtume Paul anazungumza kitachotokea, anasema Sote hatutalala, means sio wote watakufa, anasema itakua ni kitendo Cha kufumba na kufumbua, Watu watafufuliwa na Miili isiyoharibika NASI TUTABADIRISHWA (Wa kina nani) wale wataokuwa Hai Watabadirishwa, anasema Miili hii ya kuharibika itavaa kutoharibika, na itavaa kutokufa.
Hivyo Kwa Wale wataopata nafasi ya kuwepo hai Wakati Tarumbeta ya 7 ikipigwa, itabidi Miili Yao ibadirishwe, hawata kufa, ila Miili Yao itabadirishwa, na Biblia inasema itakua kitendo Cha haraka sawa na kufumba na kufumbua....!
Biblia inaeleza wazi kuwa sio wote watakufa, Wapo wataishi Milele bila kufa, Wataungana na Watakatifu wengine wataofufuliwa.
Kuna Uzima wa Milele wa kwanza na Kuna Uzima wa Milele wa pili, ni sawa na Kuna Ufufuo wa kwanza na Ufufuo wa pili.