Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,533
Heshima mbele wadau........Ni wazi hapa nyumbani ukanda fulani au makabila fulani yanatambuana na kutambulika kirahisi kwa lafudhi zao. Mifano ni mingi lakini akiongea Msukuma toka Shinyanga au kule Magu sio jambo gumu kumtambua. Akija "pure" likurya la pale sirari au mugumu pia ni jambo rahisi kulitambua kwa lafudhi pekee bila kuuliza. Vivyo hivyo kwa Ndugu zetu hapo mji kasoro bahari wapogoro " wazee wa kambale" na jamaa wa kule kaskazini-wachagga, maarufu kama "Mangi" au "meku". Nimefuatilia kwa baadhi ya haya makabila mathalani Wasukuma hata wakiongea kiingereza you can still note accent yao ipo pale lakini kwa kina mangi inapotea.....je mnabadilishaje? Is it something deliberate or natural? Kama wewe inakuhusu hebu tuambie!