Kwanini academic certificates zinafanyiwa verification kwa wataalam wa sheria badala ya taasisi husika ya elimu kama RITA wafanyavyo kwa vyeti vyao?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania eti;

Kwanini academic certificates zinafanyiwa verification kwa wataalam wa sheria badala ya taasisi husika ya elimu kama RITA wafanyavyo kwa vyeti vyao?

Nilipokuwa ninamsaidia mdogo wangu kuomba mkopo wa elimu ya juu (HESLB) mwaka huu 2020 nilifanya online verification ya cheti cha kuzaliwa pamoja na cha kifo cha baba yake katika portal ya RITA. Home Page lakini academic certificates nikaenda kugongea mihuri katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

(1) Kwanini "Copies of Academic Cerificates" zinapigwa muhuri kwa wataalam wa sheria badala ya kupata verification ya taasisi husika ya elimu (zipigwe muhuri wa chuo husika kama ni UDSM, IFM, UDOM, IAA, CBE) ndio ziitwe certified.

(2) Kwanini vyeti vya kuzaliwa na kufa vinapata verification ya RITA badala ya kupigwa muhuri wa wataalam wa sheria pekee kama wafanyavyo kwa "academic cerificates"?

Kwanini hakuna Standard za vyuoni; Mafano Necta kuna standard Certificate ( Central verification) watahiniwa wote wanapata cheti kutoka mamlaka moja, kwanini vyeti vya vyuo vikuu vyote visitolewe na TCU?

Je, wale watumishi hewa waliotumbuliwa kwa kuwa na vyeti feki hawakupeleka vyeti vyao kwa wanasheria na vikagongwa mihuri?

Wataalam wa masuala haya kwanini kuna huu mkanganyiko, ninaomba ufafanuzi tafadhali wakuu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Na hata hicho cheti cha kuzaliwa km ni copy utaverify kwao sio RITA kama unavyodai.
Nilipokuwa ninamsaidia mdogo wangu kuomba mkopo wa elimu ya juu (HESLB) mwaka huu 2020 nilifanya online verification ya cheti cha kuzaliwa pamoja na cha kifo cha baba yake katika portal ya RITA. Home Page lakini academic certificates nikaenda kugongea mihuri katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
 
Verification? Wana certify copies of the original document ili usihatarishe kutuma original documents ama certificates. Halafu mbele ya Safari huko kama vyeti original vitahitajika utavipeleka mwenyewe kwa mkono.

Yaani wao wameidhinishwa tu kusema kuwa kivuli hiki kimetoka kwa nakala halisi.
 
Verification? Wana certify copies of the original document ili usihatarishe kutuma original documents ama certificates.
Sasa mbona hapa ni kama unazungumzia kitu kimoja sema tu umezungusha maneno mkuu? Kwani "certification" na "verification" tofauti yake ni nini?...
 
Umenikumbusha mbali mno...

Niligharamika pesa nyingi sana mwaka 2015 na hata ishu yenyewe sikuipata aisee! Nyie acheni tu ila ukweli unabaki kuwa "Siasa" ni "Si hasa"
 
Certification of documents ni legal procedure hivyo ni lazima ifanywe na wanasheria/mahakama maana hivyo ndio vyombo vinavyohusika na justice...vile vile vyeti vyako unavyopewa na taasisi husika vinakuwa tayari na certification ya hizo taasisi Kama vile mihuri ya moto, signatures za exucutive secretary, chairperson, vice Chancellor, deputy vice Chancellor, logos za chuo husika n.k hivyo haina tena maana ya kuvirudisha kwao eti wavithibitishe kisheria maana wao sio chombo cha sheria pia!!

Vile vile katika certification ya documents, ni lazima uende na original documents mahakamani....hii husaidia wale waliogushi vyeti vya wenzao kutiwa mbaroni
 
Wanasheria hawafanyi verification mkuu, Wao Ni mashahidi wanashuhudia kuwa vyeti Ni halali ndio maana ukienda kugonga wanagonga kopi ila wanaomba waone orijino.
 
Sasa mbona hapa ni kama unazungumzia kitu kimoja sema tu umezungusha maneno mkuu? Kwani "certification" na "verification" tofauti yake ni nini?...
The two terms "certify" and "verify" do not have fixed legal meanings. They are used in a lot of places, generally in rules and regulations saying what a government body or private actor is supposed to do in different circumstances, or else a standard for proving that something is true.

To verify something is for the party wondering whether or not it is true to make a fair effort to determine its truth. For example, if you are a bartender, you may have to verify that somebody ordering a drink is over 21 years old. If you are a company seeking investment, you may verify that somebody is an accredited investor. In these two cases you are looking at some documents to decide whether they appear genuine and show the thing in question to be true.

To certify something is to make an official pledge on behalf of oneself or on behalf of an organization where one is authorized to make such a pledge, that a particular thing is true. In the above examples, a government agency may certify that a person is 21 years old, or a person's lawyer may certify on their behalf that they are an accredited investor. It is related to the word certificate, which is a written document certifying something.

One subtle difference: verifying is usually done by the person asking the question; certifying is done by the person providing the answer. However, the word verify is sometimes used to mean an informal pledge, similar to the word 'confirm'. For example, when asked, somebody could verify about themselves or confirm that they are over 21. They haven't certified the fact unless they've pledged it on an official written document.

Copied
What is the difference between 'to certify' and 'to verify'? - Quora
 
Kwa mwanasheria unakwenda kupata uhalali ya kuwa kivuli ulichonacho kimetokana na original document ambayo mwanasheria ameiona na kuthibitisha. Issue hapa ni kwamba kwa mafunzo yao na viapo vyao hatutegemei kwamba watakuwa wadanganyifu. Lugha sahihi ni kupata certified copies.

Kwa uelewa wangu verification ya cheti ndio hufanywa na wale waliotoa cheti kuhakikisha kuwa kuwa cheti kile wamekitoa wao na ni halali pamoja na viambatanishivyake (Istad to be corrected).
 
Back
Top Bottom