Utaratibu wa kuthibitisha vyeti

DMmasi

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
421
648
Habari wanajamii wenzangu,

Baada ya salamu niwapeleke moja kwa moja kwenye hoja

Kuna hili swala ya kuthibitisha vyeti kwa kutiwa muhuri wa mwanasheria, vyeti hivyo ni kama;
(cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu katika ngazi mbalimbali utakazo kuwa umepitia kama astashahada, stashahada, sekondari n.k)

utaratibu huu nimeshindwa kuuelewa na sioni umuhimu wake kwa sababu zifuatazo

#Kwanini visibitishe wakati vyeti hivyo tayari vina muhuri na saini za viongozi wa taasisi inayokutunuku cheti/vyeti hivyo.
Je taasisi hizo zimeshindwa kuaminika?

#Nguvu ya muhuri na saini za wasimamizi wa izo taasisi ni ipi kama vyeti bado vitahitaji kuthibitishwa

#Kama muhuri wa mwanasheria ni muhimu kwanini lisiusishwe moja kwa moja na mwanasheria wa taasisi inayokutunuku chetii

Karibuni tuelimishane kwa hoja katika hii dunia ya sayansi na teknolojia
 
Nafikir pale ni ku prove kati ya cheti halisi na copy zake.
Namaana mwanasheria anatakiwa aangalie au athibitishe kwamba hii ni sahihi copy from original.
 
Nafikir pale ni ku prove kati ya cheti halisi na copy zake.
Namaana mwanasheria anatakiwa aangalie au athibitishe kwamba hii ni sahihi copy from original.
sawasawa mkuu nimekupata vizuri
 
Back
Top Bottom