Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,334
- 7,873
Kwa ufupi tu unachosema kinachotutofautisha sisi na wao ni kwamba wao wana mataifa yanayoundwa na watu wao kimshikamano, wakati sisi huku hatuna hayo mataifa bali ni mkusanyiko tu wa jamii mbali mbali zenye tamaduni tofauti sizizokuwa na mshikamano wowote zinazoishi ndani ya eneo moja ambalo nalo walitengewa na mipaka ya watawala wao.Haya masuala uliyoandika yapo kishule sana na mengi yameshafanyiwa utafiti na majibu yapo...
Hila vitu vinavyokosekana ni kumfikiri waafrika wote tuna fikra na hatuna tofauti zetu.
Wazungu walipigana vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Na matokeo ya vita hivyo ni kuwa na nchi zenye kukubalika na wananchi wao. Ukienda Ireland ni wa Irish.. ukiend Ujerumani ni wajerumani.... ukienda Italy ni wataliano....Ukienda Spain ni waspanish....
Njoo Afrika...Ukienda Kenya wajaluo, wakikuyu na kadharika...
Tanzania ....wasukuma, wachaga, .. wazaramo n.k
Nigeria waibo...fulani... n.k
DRC ndio usiseme..
Ukienda Afrika kusini kuna wazulu...Wakhosa...n.k na ni watu wanaowapiga wafrika wenzao ni watu wazulu kwa sababu ni easy target...
Sent using Jamii Forums mobile app