Kwani wazungu wana nini ambacho waafrika hatuna: What is the missing link?

Sahihi kabisa chief

Hii ndio mifumo tunayohitaji. Pia tunahitaji katiba ya kuzuia Rais au Waziri kutumia hela za kodi anavyotaka yeye. Hela za umma lazima zifanyiwe maamuzi na Bunge kwa utaraibu wa kimfumo na kimkakati. Tunahitaji katiba, mifumo na taasisi zenye nguvu

Bunge letu haliwezi kutusaidia. Sana sana litatuchelewesha kupata maendeleo.

Wabunge wengi walo pale kuongea kujipatia umaarufu. Kupinga au kuunga mkono hoja kutokana na maslahi binafsi, sio kwa maslahi ya Taifa.
 
Fafanua kidogo mkuu

unatamani turudi nyuma kwenye mifumo tuliyokua nayo kabla ya ukoloni? Unadhani kuna mambo ya mwaka 1700 yatakua na tija sasa

Nilidhani tunatakiwa tuende mbele badala ya kurudi nyuma
/
Simaanishi hivyo ila nasema tungeendelea nayo ile mifumo na kuiboresha jinsi wakati unavyoenda tungekuwa na mfumo bora tofauti na wazungu. Jamaa walituingizia mfumo wao na wakatufanya tusahau kabisa wakwetu na leo hii tunashindwa kujikwamua kwa kuwa wameshatuingiza king na hatuna la kufanya tunafuata wanachotaka wao

Najua ni ngumu sana kunielewa unless uwe umekaa nao sana haswa katika sekta muhimu kama elimu na utawala - achana na kubeba box. Jamaa wana mipango ya ajabu sana na ya muda mrefu niliwahi kuudhuria kikao kimoja Geneva walikuwa wanataka kuweka solar power katika jangwa la sahara (Renewable Energy) ili kuachana na nyuklia kutokana na risks zake.

Bahati nzuri nilibahatika kusikia wanavyojiandaa kufanya lobbying ili waweze kuingia mikataba na mataifa ya Afrika yaliyopitiwa na jangwa la Sahara. Ilisukwa mipango na kila aina ya kuwavutia watu wakubali, walialikwa presenters wakubwa wenye ushawishi duniani ili waje pale wapate kushawishi lakini mwisho wa siku waligonga mwamba ila jamaa hawakati tamaa wanatengeneza mbinu nyingine ili waweze kututeka

Mzungu ni mjanja sana yaani hata ukikutana nae sehemu usimchukulie poa ana siri ndani yake anayoifanyia kazi, hawaji bure bure kung'atwa na mbu huku Afrika
 
Simaanishi hivyo ila nasema tungeendelea nayo ile mifumo na kuiboresha jinsi wakati unavyoenda tungekuwa na mfumo bora tofauti na wazungu. Jamaa walituingizia mfumo wao na wakatufanya tusahau kabisa wakwetu na leo hii tunashindwa kujikwamua kwa kuwa wameshatuingiza king na hatuna la kufanya tunafuata wanachotaka wao

Najua ni ngumu sana kunielewa unless uwe umekaa nao sana haswa katika sekta muhimu kama elimu na utawala - achana na kubeba box. Jamaa wana mipango ya ajabu sana na ya muda mrefu niliwahi kuudhuria kikao kimoja Geneva walikuwa wanataka kuweka solar power katika jangwa la sahara (Renewable Energy) ili kuachana na nyuklia kutokana na risks zake.

Bahati nzuri nilibahatika kusikia wanavyojiandaa kufanya lobbying ili waweze kuingia mikataba na mataifa ya Afrika yaliyopitiwa na jangwa la Sahara. Ilisukwa mipango na kila aina ya kuwavutia watu wakubali, walialikwa presenters wakubwa wenye ushawishi duniani ili waje pale wapate kushawishi lakini mwisho wa siku waligonga mwamba ila jamaa hawakati tamaa wanatengeneza mbinu nyingine ili waweze kututeka

Mzungu ni mjanja sana yaani hata ukikutana nae sehemu usimchukulie poa ana siri ndani yake anayoifanyia kazi, hawaji bure bure kung'atwa na mbu huku Afrika

Nimekuelewa vizuri sana mkuu. Uko sahihi sana. Jamaa wajanja mno wana akili mno. Wametuzidi mno sisi ni kama chekecheka ukilinganisha na mzungu
 
Bunge letu haliwezi kutusaidia. Sana sana litatuchelewesha kupata maendeleo.

Wabunge wengi walo pale kuongea kujipatia umaarufu. Kupinga au kuunga mkono hoja kutokana na maslahi binafsi, sio kwa maslahi ya Taifa.

Umenifikirisha sana

Unajua Bunge letu nalo lina evolve - slow change

Inabidi tufika mahali bunge letu lijae wasomi na matajiri - people with options and nothing to loose. Hawa ndio watu wanaweza kusimamia maslahi mapana ya nchi bila woga na kwa ubunifu zaidi. Lakini hawa wasasa akina kibajaji ni projo tu, hakuna utafiti wowote full uoga na kufata bendera ya chama. Si umeona Nape amekua ndumila kuwili baada ya kuona anataka anyanganywe mkate - ameomba msamaha kulinda tumbo na kula yake tu in reality he is not sorry for he committed no offense
 
Nini kilitufikisha tulipo,kutoka ktk mifumo yetu na kushindwa kuchukua ELIMU km nyongeza juu ya mifumo yetu
Lkn pia nipe mfano wa waliobaki hadi sasa katika mifumo yao asilia kwa dunia ya sasa
Kabla ya kuja kwa elimu ya sasa waafrika tulikuwa na mifumo yetu ya elimu mifumo ya utawala, utamaduni, mavazi namisingi yetu ya Maisha ambayo ilikuwa inafanya kazi vizuri tu na kulikuwa na mifumo ya uongozi kama machifu, wafalme n.k. Hii elimu ya sasa siipingi ila ingetumika kama nyongeza tu katika mifumo tuliyonayo

Tulichofanya sisi ni kuterekeza mifumo yetu na kuchukua ya kigeni moja kwa moja ambayo ndio uliyotuingiza kwenye matatizo.

Natamani vizazi vijavyo vya waafrika vingefanya research kwenye mifumo ya zamani ya uongozi , utawala nk ili tuweze kuiboresha iendane na wakati na kuitumia sasa. Tuwe na kitu tofauti na wao.

Mifumo yao ililenga sana kututawala na kutufanya kuwa wateja wa bidhaa zao kitu ambacho wamefanikiwa sana na sasa wanatupangia mpk uongozi ambao una maslai nao ili wapate kutu-control Zaidi. Hivi ni vitu ambavyo wanavifanya na wamewekeza mno kuhakikisha wanatushika maeneo hayo.

Kuna ukumbi wa mikutano Ethiopia wachina waliujenga na kuweka vinasa sauti ambavyo vinatuma habari moja kwa moja China kwa yote mnayojadiliana pale na kuangalia jinsi gani wanaweza kutuwahi kushughulikia maamuzi yetu na ku-interact kabla mambo hayajaenda mbali au kudaka fursa mapema Zaidi ya wenzao. Ndio akili za watu weupe hizo
 
Kwa hiyo huoni hao watu wana shida?

Katika kujifunza kuna kitu kinaitw affective domain. Yaani katika level hii mtu anaiishi elimu yake.

Hicho ndicho nachomaanisha. Hushangai daktari anajua vizuri sana matatizo yatokanayo na sigara na anavuta kama kawaida?

Huoni kuna shida? Elimu yetu lazima iboreshwe watu walioelimika waaishi na waitumie kutatua changamoto zao.

Hujajibu swali mkuu. Elimu ipi wapewe hao watu ili waache hayo matendo ya aibu kwenye ulimwengu uliostaarabika ?
 
Alichotuzidi mzungu ni ujanja na maarifa! Walipotuletea dini walitutisha na moto wa milele, wakatuachia Biblia tufunge macho tusali na wao waangalie Afrika kuna nini cha kuchukua. Hata hivyo wao hawana blaablaa! Wanachunga mda.
 
1: wazungu hawana undugu wa kurudishana nyuma. Hawabebani kipuuzi.

2: Wazungu wakweli, hawana uwongo kama waafrika.

3: wazungu wananidhamu ya Kazi.

4: wazungu wanapenda haki.

5: wazungu sio Wachoyo.

6: wazungu wanaheshimu vidogo walivyonavyo ndomana wanafanikiwa.

7: wazungu hawana nidhamu ya woga.

8: wazungu hawana kujuana juana.
Mimi naishi na wazungu kwa zaidi ya nusu ya maisha yangu. Wazungu wana tabia sawa na waafrika.

Matatizo yetu ni kuwa tunamchukua mzungu aliendelea kuwakilisha wazungu wote.

Mzungu katuachia vitu ambavyo yeye mwenyewe alivibadilisha kufanana na mazingira yake.

Kwanza kakuachia dini. Dini alikuachia mzungu aliibadilisha na anaendelea kuibadilisha hili ikubalike na mazingira yake. Dini uliyoipokea ina mazingira ya kizungu na huwezi kuihoja au kuibadilisha.

Kwa mfano Ireland ni nchi ya kikatoliki. Lakini waziri mkuu ni shoga. Wamemchagua kwa sababu anaweza kufanya kazi na sio kwa imani yake. Nitajie nchi moja ya kiafrika inayoweza kufanya hivyo?

Pili elimu yako unayopewa haitazami mazingira yako. Inatazama mazingira ya mzungu. Ukijaribu kuwa na ushupavu wa kusoma na kuangalia mazingira yako, utajua jinsi ya kukabiliana nayo.
 
Watu wameongea mengi sana ambayo yote yanaweza kuwa ni majibu ya mada husika. Nadhani hili kupata ufumbuzi au chanzo kitakachotupa majibu yenye usahihi zaidi yapaswa tuangalie kwanza mwanzo wa maisha ya binadamu ulikuwaje, binadamu alianzaje anzaje kukabiliana na changamoto za kimazingira katika maisha yake kwanzia awali mpaka hapa alipofikia.

Katika hiyo awali ya maisha ya mwanadamu je jamii zote zilikuwa zinaishi pamoja au kila jamii ilikuwa inaishi kimpango wake kulingana na eneo ilipojikuta!?

Kama jamii zote zilikuwa zikiishi pamoja nini kilichosababisha mtengano hapo baadae? Na kama hazikuwa zikiishi pamoja kwanini tangu awali tuna mfanano kwenye namna tunavyotatua changamoto zetu mbali mbali hasa za kimazingira!?

Nini kilichofanya jamii moja kupata ujasiri wa kuzivamia jamii zingine na kuzitawala kwa mafanikio? Na kwanini hizo jamii zilizovamiwa na kutawaliwa hazikuwa na uwezo wa kumzuia huyo mvamizi? Nini kilichowafanya wasiwe na nguvu sawa na mvamizi huyo?

Je, jamii hiyo iliyoenda kuwavamia wengine ilichagizwa na mazingira magumu iliyokuwa ikiyaishi ambayo yalikuwa ni tishio kwa uhai wao kana kwamba ikaona njia pekee ya kuweza ku-survive ni kujaribu kutumia mazingira ya jamii nyenzie kwa mabavu ambayo ilionekana kuwa na auheni?

Je, kuishi katika mazingira magumu ndio ilikuwa chanzo cha jamii moja kuwa na upeo mkubwa kuliko nyingine!? sababu akili yako unaifikirisha sana tofauti na yule ambaye mazingira anayoisshi yana ahueni ya kuyaishi?

Hata baada ya jamii zilizolikuwa zikitawaliwa na jamii zingine kuwa zimejikomboa, nini kimefanya mpaka leo hii jamii hizo kuendelea kuwa dhaifu mbele ya jamii zilizokuwa watawala wao ilihali mambo hayo ya kutawaliwa yalitokea nyakati zilizopita?

Je, utofauti wetu wa kiupeo/akili ni jambo ambalo tunarithishana vizazi na vizazi!? Yaani hii mtoto wa mzungu anazaliwa akiwa tayari ana akili nyingi kuliko mtoto wa mwafrika mwenye umri sawa na wake? Na je hatuwezi kutafuta namna ya kuondoa huu utofauti wa kiupeo kati ya jamii na jamii?

Je, ni kweli Mungu alituumba tukiwa tofauti katika matumizi ya akili na kama alifanya hivyo alikuwa na makusudi gani?
Haya masuala uliyoandika yapo kishule sana na mengi yameshafanyiwa utafiti na majibu yapo...

Hila vitu vinavyokosekana ni kumfikiri waafrika wote tuna fikra na hatuna tofauti zetu.

Wazungu walipigana vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Na matokeo ya vita hivyo ni kuwa na nchi zenye kukubalika na wananchi wao. Ukienda Ireland ni wa Irish.. ukiend Ujerumani ni wajerumani.... ukienda Italy ni wataliano....Ukienda Spain ni waspanish....

Njoo Afrika...Ukienda Kenya wajaluo, wakikuyu na kadharika...

Tanzania ....wasukuma, wachaga, .. wazaramo n.k

Nigeria waibo...fulani... n.k

DRC ndio usiseme..

Ukienda Afrika kusini kuna wazulu...Wakhosa...n.k na ni watu wanaowapiga wafrika wenzao ni watu wazulu kwa sababu ni easy target...
 
GDP=Gross Domestic Product. Hizi ni shughuli zote za kiuchumi zinazofanyika ndani ya nchi kwa mwaka mzima. Ukisikia uchumi unapanda ujue hizi shughuli zote za uzalishaji mali zimeongezeka na kipato cha watu kimeongezeka.
GNP= Gross National Priduct. Hizi ni shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na raia wa nchi husika bila kujali wako ndani ya hiyo nchi au nje ya nchi ili mradi ni raia wa hiyo nchi. Mfano GNP ya Tanzania ni GDP+ mapato ya watanzania waishio nje ya Tanzania(yale mapato wanayopata na kutuma kuja Bongo kuendeleza shughuli zao).

Nadhani umepata picha angalau.
Sio angalau,nimepata kukuelewa vizuri,asante sana
 
Nakubaliana na wewe, waafrika tuna matatizo na nadhani kuna shida kwenye akili zetu.

Tofauti yetu kubwa na wazungu ni nidhamu, wazungu wana nidhamu, wamestasrabika, mtu akikosea na ukamwambia anakiri kosa huku kwetu hatukosei, sisi tunajua kila kitu, sisi hatushauriki.

Duniani kote watu wenye akili ni wachache kuliko wajinga, wajinga ni wengi sana. Wazungu wao walikubaliana mambo muhimu na ya kitaaluma waachiwe wataalam, sheria zitungwe na wataalam kwa maslahi ya nchi na sio maslahi ya serikali/chama kilichopo madarakani. Wazungu walikubaliana kua wataongozwa na kanuni zilizotungwa na wenye akili.

Huku kwetu hatuna nidhamu, sheria na kanuni zinatungwa na wanasiasa wasio na akili, wabinafsi wanaojipenda na familia zao. Sheria na kanuni hazitungwi kwa maslahi ya nchi bali ya wanasiasa. Huku kwetu wajinga huongoza watu wote, wenye akili na wajinga wenzao.

Waafrika hatuna ustaarabu, wabinafsi, wenye roho mbaya, tusio na nidhamu ya chochote, tusiojali muda, tusio na maono ya mbali, tusiotaka kupingwa, sisi tunataka kusifiwa tuuu, kupongezwa hata tukifanya ujinga, kupenda kutukuzwa. Angalia viongozi wetu walivyo

Waafrika ni shida. .
Hiki ndio nlikuwa nategemea kukiona sasa
 
Sasa ulitaka awape yeye hivyo viwanja?
Kuanza umia kisa mwenzako anamiliki mali kuliko wewe ndio roho mbaya yenyewe
Tatizo roho mbaya ndio zinatusumbua,mfano kama masamaki mtu anamiliki nyumba zaidi ya 50 wakati kuna mtu anatafuta kiwanja cha 20kwa20 ajenge kibanda.
 
Uko sahihi tena uko makini sana

Baada uhuru au pale tulipofikisha miaka 20 au hata 30 baada ya uhuru kulikua na haja ya kuangalia mifumo yetu yote ya kijamii ili kujenga mifumo mipya itakayokidhi mahitaji yetu sisi wenyewe ambayo nitofauti naya mzungu. Mifumo ya kikoloni, tuliyo achiwa na kuendelea nayo, haikuundwa ili kumuendeleza muafrika au kuendeleza nchi lakini sisi tunaendelea nayo kama vipofu au nyumbu na hapo ndio tunapoishia kuingia choo cha kike
Hakuna lolote, kama unabisha wachukue watanzania wote uwapeleke Sweden au Denmark na wazungu wa kule walete Tanzania, yaani fanya exchange.....come back after 20 years utaniambia nini kimetokea...
 
Waafrika wanazaliwa na uwezo mdogo wa kufikiri. Hiyo ndio missing link. Zaidi ya hapo mtaishia kudanganyana na kupeana matumaini.

Kwako mwalimu kashasha Karma
 
Mataifa yetu hayana dira. Kila kiongozi anayeingia anakuja na lake iwe kuiba au kuwakomoa wabaya wake au kufanya ili aendelee kuwepo
 
Back
Top Bottom