Tatizo la mafuta ni 'artificial' na ni la wafanyabiashara. Kumbuka wakati mafuta yanapanda bei katika soko la dunia hatukuwahi kuona upungufu hata sku moja. Kitu cha kushangaza mafuta yalikuwa yanapanda bei kila siku utadhani ni maji yanayonunuliwa ruvu na kuuzwa siku hiyo hiyo. Nina maana kuwa kama kuna shehena imenunuliwa mwezi wa 3 na bado ipo kwanini bei ikibadilika usiku mmoja iathiri shehena hiyo?
Wapo watakaosema ni soko huria, lakini soko huria na bei za mafuta linaathiri sana nchi zinazoagiza mafuta kila siku na matumizi yake ni makubwa. Huko nyuma ilishawahi kutokea TPDC walipandisha bei miezi 3 baada ya bei kupanda soko la dunia kwasababu walishagiza kwa bei ya wakati huo.
Soko huria ni zuri likiachiwa kufanya kazi kwa maana hiyo, lakini wafanyabiashara wameamua kufanya ushirika kinyume na taratibu za soko hilo popote duniani. Kwa hivyo, kuachia huria ni kuhalalisha maumivu zaidi kwasababu watakaa vikao na kusema tuuze lita 7,000. Ni kwa msingi huu ndipo EWURA iliundwa si kuthibiti bei bali kumlinda mtumiaji 'consumer'.
Hata nchi zilizoendelea zina consumers organizations, sio kudhibiti bei bali kuhakikisha kuwa soko linakuwa huru kwa maana hiyo na kuwa mtumiaji hakamuliwi mpaka tone la mwaisho la damu kwa ushirika wa wafanyabiashara, bali bei zinapangwa na soko lenyewe.
Kama TPDC ingekuwa katika ushindani wafanyabiashara wasingefika hapa walipo kwasababu soko lingekuwa huru na si la ushirika. Hatujajifunza kuwa kuweka sekta muhimu kama hii mikononi mwa watu wawili au watatu ni hatari, na kwamba ikitokea dharura sijui tutafanya nini.
Wafanyabiashara hawa wana nguvu sana na wanatumia umoja to creat demand, na wanajua serikali haina pa kutokea. Ndio manaa hadi leo suala nyeti na la hatari kama hili linashughulikiwa na EWURA inayoonekana kutokuwa na uwezo kukabiliana nao. Serikali ipo kimya na sijui ni kwanini inawaogopa.
Marekani ina stategic reserve na ndio wenye soko huria, sasa tujiulize kwanini wana reserve. Kuna wakati waliachia mapipa milion 30 na yaka stabilize bei kiasi, na ile psychology tu kuwa uwezekano wa kutumia strategic reserve upo ulishusha bei sana. Sisi ya kwetu ipo wapi?
Hili ni tatizo la kutokuwa na mkakati, nguvu kubwa ya waagizaji inayoizidi serikali na madudu mengine ambayo tutayafahamu tu huko mbeleni. Sitashangaa nikisikia wanahisa ni viongozi, nani alijua Kapuya ana hisa Simon au mwenyekiti wa bodi ni consultant pia !!