Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

kwahiyo sasa waalimu wameyapatia maisha kwa sasa si ndio???
Kusomesha mtoto ni nia ya mzazi na sio kuyapatia maisha,hebu acha akili za kimasikini ndugu yangu kwamba kila amayekula wali ni tajiri
Wapo mama lishe wanasomesha watoto shule nzuri itakua Mwalimu ambae ana uwezo wa kusomesha mtoto kwa kukopa Benki kila mwaka na akakubaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mawazo yakp upo sahihi.Ila unatafuta justification ya kuhalalisha kuwa english medium si lolote wala chochote.

Hujiulizi au kufikiri kwa sekunde 5 ni kwanini wenye fedha na mamlaka wengi watoto wao wanasoma hizo shule unazozidharau wewe?

Mshirikishe kidogo basi mkeo ili upate uelewa kama naye kichwani zimo.

Shule za Serikali na private zina umuhimu wake kwa jamii ndio maana Serikali inazipa usajili kwa kutoa kazi/ajira,kukuza uchumi,mapato kwa Serikali n.k.Soma sera mbalimbali kuhusu elimu ndio upate mwanga kwenye akili yako.

Umeleta uzi wa kifala mno mkuu wenye sizitaki mbichi hizi kumbe ujanja ujanja wa mjini kupata hela kimchongo hazipo tena awamu hii.

Hahahahaha!
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo mgando kweli haya.Kuna walimu wako vizuri kiuchumi kuliko hata baadhi ya maprofesa.We kariri tu.

Halafu walimu wapo wa kada tofauti yaani msingi,sekondari,vyuo,madrasa,kwaya,chekechea n.k.Ulilenga walimu gani?
Weee unaakili Sana mwalimu anawatoto wanne kwa mfano hio ada atatoa wapi labda Kama ameekeza na sijui aliekeza lini

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni umasikini tu.

Hivi kuna nchi nyingine duniani ambayo inatumia lugha mbili tofauti za kufundishia?
 
Mawazo mgando kweli haya.Kuna walimu wako vizuri kiuchumi kuliko hata baadhi ya maprofesa.We kariri tu.

Halafu walimu wapo wa kada tofauti yaani msingi,sekondari,vyuo,madrasa,kwaya,chekechea n.k.Ulilenga walimu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
hata wauza karanga wapo wenye maisha safi kuliko ma engeneer,ni swala la umekutana na kuishi na yupi baas.
 
Ni vzur kusoma English medium,lakin kama watoto wanaweza kupata walimu wazuri nyumban wa kuwafundsha kiingereza vzur kila siku,haina haja sana ya kusomea huko,KIINGEREZA N CHA MUHIMU SANA KUKIJUA KTK UMRI MDOGO,husaidia mazingira ya ujifunzaji kuwa rahis
 
Kiswahili ni lugha ya mikosi sana.Lugha isiyo na mvuto wowote wa kielimu.Lugha ya kutapelia tu katika nyanja zote,siasa,mapenzi na hata katika imani za dini.

Ni lugha ninayoitumia lakini siipendi kwani ni chanzo cha umaskini na fikra finyu kwa wengi.
Tatizo sio shule mwanafunzi anayosoma, tatizo ni kumuandaa mtoto katika elimu yake ya msingi kwa kumfundisha kwa kutumia Kiswahili miaka zaidi ya 7 kisha baada ya hapo unambadilishia gear angani aanze kujifunza kwa kwa lunga ya Kiingereza kwa miaka 4 hadi 6 alafu ufaulu ukiwa duni watoto wanaitwa vilaza.

Kwani kinashindikana nini mitaala yote ya elimu yetu ikawa ya Kiswahili tuu level zote za elimu? Au ikawa ya Kiingereza tu level zote?

Tuchague moja kisha tupime ufaulu.

Mtag Ndaliwize.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa Elimu bado haujabadilika ila mahitaji ya elimu yamebadilika, kuna haja ya mzazi kujua unataka mwanao ajifunze nini au apate elimu ya namna gani kwa manufaa yake ya baadae. Binafsi nitajitahidi wanangu wapate private tutor kwa ajili ya baadhi ya vitu ambavyo ningependa wajifunze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe pia unataka mwanao aishi kama blue iv,sababu hujawa jay z,basi hutazaa???

au ulitaka kusemaje?
Nilitaka kusema kwamba fikiri kabla ya kuzaa,kama fikra zako ni kuwalea wanao Bora wale walale wakue basi zaa kila siku ila kama unatamani wanao walale makazi bora,wakue mazingira Bora hata kama ni Bora ya kati basi huna budi kuzaa watoto amabao utaweza kuwapa hayo maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom