Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Mwanangu atasoma English medium .
Nataka aanze kuizoea lugha ya bibi akiwa mdogo.ukubwani asipate tabu.
Umewaona waliosoma elimu ya mkoloni?
umewaona wakenya ?na waganda?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
walimu gani wanapeleka watoto eng medium,au unazungumzia wabunge??waalimu hawa hawa wa mishahara yenye makato ya bodi ya mikopo??
Wako kibao tuu wewe acha dharau. Huku kasikazini hasa Moshi na arusha Kuna English medium Zina ada Hadi laki 6. Sio walimu tuu Hadi mama ntilie watoto wao wanasoma huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha dharau ndg yangu. Malengo yoyote sio lazima uwe na kipato kikubwa. Mimi ni mfano hai, nilisha jiapiza wanangu hawato soma s/m za serikali ambazo zimejaa madudu. Elimu itolewayo haitofautiani na kipato apewacho mwalimu. Siwezi muweka mwanangu ktk darasa lililo jaa watoto 200 kwa wakati mmoja. Mwl tu anakosa hewa darasani sembuse mtoto.
walimu gani wanapeleka watoto eng medium,au unazungumzia wabunge??waalimu hawa hawa wa mishahara yenye makato ya bodi ya mikopo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ameamua kuwa mbishi tu, Mimi ni mwl tena sina hata miradi. Ila nina malengo na NAMPENDA sana mwanangu. Pre unit kasoma ka shule kalikua kanaanza ada 1.3. Iyo nursery ina vifaa mpk raha. Mwanangu alijipeleka shule akiwa 3yrs. He is approximately 7yrs old yuko class 3 na kwa umri huo kawapita wa rika lake wa St.Kayumba mbali sana kiupeo. Sasa uyo anaye ishi kwa kukalili kalaghabaho
Ada Mil. 1 mpaka 1.5 mwalimu mwenye nia hawezi shindwa m
Kumlipia mwanae

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada ungeweka wazi kwanza kipato chako na shughuli unayoifanya hapo ndo tutajadili vizuri hili swala...binafsi nimesoma hizo English Medium na pia nilisoma hizo Kayumba ila mtoto wangu atasoma English Medium mwanzo mwisho wa kayumba atakutana nao chuo kikuu
 
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app

Peleka watoto kwenye mashule ya kipumbavu ya bwana mawe halafu baadae mitoto inakua misukuma mikokoteni uanze kulia

Toa hela hiyo acha justifications za nyani kujenga nyumba mpaka leo hwajajenga
 
Kote kuna faida na hasara...

Shule za govt kwa sasa usimamizi wa wanafuzi ni mdogo kutokana na hali ya mishahara pamoja na madaraja ya walimu.

Shule binafsi zinaushindani, kufaulisha ndy chaguo lao la kwanza. Ila huku Binafsi watoto wanakosa michezo mingi kutokana na kuwa wameBase sana kitaaluma.
 
Wako kibao tuu wewe acha dharau. Huku kasikazini hasa Moshi na arusha Kuna English medium Zina ada Hadi laki 6. Sio walimu tuu Hadi mama ntilie watoto wao wanasoma huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
sidharau waalimu mimi.

hii nchi ina waalimi zaidi ya 80elfu.kama umekutana na waalimu watatu au wanne sitoe hitimisho la jumla jumla.
 
Angalizo hapa. English medium tumekutana nao A level kwa masomo ya sayansi uwezo wao ni wa kawaida mno na utashindwa kuwatofautisha, kwa arts na biashara najua wanakimbiza tu. Lakini nimekuja chuo ndo nimewatofautisha haraka mno kwenye presentation na the way wanavyojiamini tofauti na wengi wa sisi kina kayumba. Pia wazazi acheni roho mbaya kama hela unazo kwanini ukomae mwanao asome kwenye taabu, sasa hela za nini si upigwe umaskini tujue moja. Yani kuna wazazi wanajenga tu na kununua viwanja alafu wanao tiamajitiamaji.
 
Dunia ina bidhaa nyingi
Ni wajibu wako kuamua ni bidhaa ipi utainunua

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia Kuna mengine unataka mtoto.azumgukwr na watoto wa daraja lipi? La chini au la Kati au la juu

English medium sehemu kubwa Ni kea ajili ya watoto wa maisha ya daraja la Kati na la juu
Ni Kama hoteli Ziko za daraja la chini kwa ajili ya watu wa chini na ziko.za daraja la juu kea ajili ya watu wa juu

Shule pia Ziko za bure kwa watu wa chini na Ziko za ada Hadi milioni kumi na mbili kwa mwaka kwa ajili ya watoto wa daraja la juu mabweni yao unakuta kila mwanafunzi anakaa chumba self contained halali kwenye bwalo
 
Hii thread bora January, binafsi mwanzo nilikuwa na mpango wa kumpeleka mtoto primary kayumba harafu secondary nimpeleke private,nikashauriliwa tena na Mwalim kuwa government schools bado zinachangamoto nyingi,pia msingi mzuri mtoto ni primary,hivyo aende private harafu sekondari sense government school

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilisoma kayumba, nikipata hela kwanza wanangu watasoma shule za maana, na ndo maana nitachelewa sana kuwa na familia. Yaani nitalipiza kisasi, nina akili kama zote lakini natamka English ya kipuuzi kabisa ukichanganya na matatizo yangu katika kuongea. Mengine yote najua ila kutamka kimbembe.
Uwe unaongea kiingereza kimoyomoyo….huwa kinapanda na hakina shida
 
Back
Top Bottom