Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezo wa akili unatofautiana
Wa mwenzio akipata A sio kwamba na wako atapata A kwenye hizo shule za serikal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lazima lakini ni muhimu. Wa kwangu nitawapeleka English medium..kayumba wataenda fees ikikosekana.
 
😅😅😅 Sasa unaanzaje kumpeleka mtoto wako sehemu kama hii wakati unao uwezo wa kumpeleka shule bora zaidi?
Huko kayumba iwe by the way tu kwa kweli.
😀 😀 Si ndo hapo sasa, Mzazi inabidi kupambana watoto wapate elimu bora tena kwenye mazingira salama zaidi.
 
Kama kuna jambo namshukuru mzee wangu ni kunisomesha Medium Primary..

Ningekuwa mgeni wa nani !??Interview ningeziwezea wapi bila confidence ya hiki kithungu changu cha kuombea maji!??

Hali ya maisha yanavyoenda English ni muhimu sana,Utandawazi unavyozidi kuongezeka aisee tuwapeleke tu watoto shule za Medium tuwaongezee kujiamini mtaani na kuweza kuleta ushindani katika soko la ajira la miaka ijayo!!

Ni sawa ila andika kiume... Au we ni rafiki wa lokole?
 
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli sisi wazazi tunaohangaika na shule za english medium tulisoma shule za kawaida na tumefaulu ndio maana tuna kipato cha kuwatafutia watoto wetu english medium. Changamoto ya sasa na zama zetu ni umri; wakati sisi umri wa chini wa kuingia shule "kenda kenda" ilikuwa miaka saba sasa hivi tunataka watoto wetu wa miaka 2.5 mpaka 3 waanzishwe shule. Wakati wetu tulisoma kwa nafasi; darasani watoto 45 (A), na wenginge 45 (B) leo watoto 200 darasa moja? Hakuna mwenye kipato chake atakubali mwanawe arundikwe kwenye darasa la watoto 200
 
Shule nyingi za St. Kayumba, kuanzia mandhari,idadi ya wanafunzi, (viijini lugha za asili), jamii ya hovyo, series, n.k vinakinzana na Elimu.
Kwa mtizamo wangu, mtoto alelewe vyema kwenye familia kisha apelekwe Medium.
Baada ya hapo anaweza kuwa mjanja kiasi
Jamii ya hovyo ni ipi? Acha mazambarau Kimbori
 
Mimi nilisoma kayumba, nikipata hela kwanza wanangu watasoma shule za maana, na ndo maana nitachelewa sana kuwa na familia. Yaani nitalipiza kisasi, nina akili kama zote lakini natamka English ya kipuuzi kabisa ukichanganya na matatizo yangu katika kuongea. Mengine yote najua ila kutamka kimbembe.
... pole sana mkuu; kutamka english kwa ufasaha ni janga la kitaifa sio tatizo lako tu ndugu yangu. Lakini cha ajabu mtoto anayei-master english vizuri hata kiswahili anakimudu vizuri pia. Pia English inaonekana kuwa na uwezo mkubwa sana tena saaana wa kumaliza lile janga la R vs L, F vs V, na S vs Z. In short, tukitaka Kiswahili chetu kiboreke, tuwapeleke watoto wetu English medium; ni mwarobaini wa kuboresha Kiswahili.
 
Nilianza darasa la kwanza miaka ya 90 mwanzoni...baba yangu akiwa Agriculturist kwenye kampuni ya George Williamson Tanzania Ltd. iliyopo wilaya ya Rungwe.

Mzee wangu alipenda kusoma vitabu...maktaba yake ya nyumbani ilikuwa na vitabu vya kutosha. Alitusisitiza kusoma sana na alitusaidia kwa kutuletea mwalimu tuition alietufundisha kiingereza kila jioni tukitoka shule...vitabu vyake vingi vikiwa vya kizungu vilitusaidia kujifunza kiingereza ikiwemo audio tapes zilizoambatana na kitabu cha Big Red Bus (Read,Listen and Follow).

Nilikua nikijua kuzungumza kiingereza sababu ya tuition ya kiingereza nyumbani (maeneo hayo hayakuwa na English Medium) ...uwezo wa kiingereza niliona ulivyonitofautisha na wengi darasani...mathalani darasani kitabu cha kiingereza cha akina Musa na Neema nilikuwa na uwezo wa kukitafsiri na kukisoma vizuri...kwa hiyo ule usomaji wa makundi mara nyingi nilichaguliwa kusoma kwa niaba...nashukuru mazingira ya nyumbani.

Baada ya kujiunga secondary nilipata unafuu sana kuelewa masomo sababu tayari nina msingi mzuri wa lugha.

Nikiwa chuo kikuu presentation hazikunisumbua mara nyingi wenzangu walipenda ni present kwa niaba yao kwa sababu niliimudu lugha ya malkia....nikiwa first year wakati wa presentation lecturer mmoja Dr. Kimambo aliuliza wewe ni mtanzania? Sababu hajazoea kukutana na first year anae present vizuri kwa lugha hiyo.

Baada ya chuo usaili wangu wa kwanza tu nilipata kazi...japo kusema ukweli kuna jamaa walinizidi na ninawafahamu walipasua vizuri GPA kali lakini waliikosa ile kazi...nahusisha kufaulu usaili ule na uwezo wa kulikabili jopo la wasaili kwa lugha ya malkia.

Nikiwa kazini mara nyingi niliteuliwa kuwa focal na rapporteur kwenye vikao hata vya ngazi ya juu sababu ya lugha.

Baadae niliacha kazi.

Hapa jamii forum hunitishi na kizungu chako....ukikutana nami huko mtaani ukadhani mie mvimba macho ukaleta ki ze you know me nakujibu bila wasiwasi!...kizungu ktk mazingira haya kinaongeza ujasiri,hilo halina ubishi (hasa 'verbal ')

Vijana wangu hivi leo wanasoma English Medium Primary schools...nikipiga nao story kwa lugha ya malkia naiona future kubwa kwao iliyojiviringa kwenye uwezo wao wa lugha ya malkia.

Somesheni watoto kwenye shule nzuri...msiogope laah sivyo mnawaweka rehani...elimu nzuri IPO huku English Medium .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@Alvajumaa,walimu gani wanapeleka watoto eng medium,au unazungumzia wabunge??waalimu hawa hawa wa mishahara yenye makato ya bodi ya mikopo??
Mkuu wapo kibao wanasomesha watoto english medium

Mi nimewaona kabisa Kuna mmoja ni mwalimu kayumba lakini alisema piga us mwanangu hasomi hizi shule za serikali mwanae kapiga english.medium since chekechea leo Yuko form 1 one of the 7 best govt schools

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe haupo kwenye cycle ya mabwanyenye ya watawala, nakushauri peleka mwanao English Medium.

Huu ni ulimwengu wa skills. Ukijua English vizuri ( Ukaongezea na Coding, Graphics Design na Communication Skills ).

Una Silaha kamili kabisa za kupata pesa UMELALA. Hakika
 
Kusomesha mtoto shule nzuri ni jambo zuri ila siku za hivi karibuni kumeibuk hadi wauza vitumbua wanapeleka watoto wao shule za bei kubwa kitu ambacho baadae wanakuja kukwama kuishia tena secondary shule za kata
Pendekezo langu kwangu kama mtu hauna hela naona ni bora mtoto aanze shule za serikali halafu baadae mpeleke private
 
@Alvajumaa,walimu gani wanapeleka watoto eng medium,au unazungumzia wabunge??waalimu hawa hawa wa mishahara yenye makato ya bodi ya mikopo??
Mkuu acha kukariri watu wanaangalia Elimu bora, watoto wa walimu wengi wanasoma hizo English Medium hata kama wazazi wao wana kipato duni lakini wanaangalia future ya watoto wao.
 
Shule za serikali zilikuwa na maana wakati ule wa ujamaa mpaka miaka ya mwishoni mwa tisini. Baada ya hapo, shule za serikali hazina kitu tena cha kujivunia linapokuja suala la ubora wa elimu. Dunia hii ya sasa ya kibepari, mwenye kisu kikali (ubora wa kitaaluma na kijamii) ndiye anakula nyama iliyonono. Binafsi sina pesa tu, ningekuwa nazo mwanangu angesoma IST. Kule hawapati elimu bora tu, wanapata na connection za maisha. Ndege wa aina moja huruka pamoja. Ukisoma na akina MwajumaNdalaNdefu, ujue hao ndio utakaoishi nao kitaa.

Tukumbuke zile zama ambazo mtu anarudia shule ili achaguliwe shule ya sekondari ya serikali zimepita. Siku hizi watu wanapangiwa shule nzuri za serikali lakin wanachomoa kwenda wanaenda private ambako kuna mazingira mazuri ya kujisomea na kujichanganya. Dunia ijayo siyo ya vyeti (si unaona Magu kashindwa kuwapa ajira maelfu ya wasomi?), ni dunia ya stadi za kazi, uwezo wa kushirikiana na wengine na uwezo wa kuongea/kuwasiliana. Hivi vitu havipo shule za serikali za msingi, tena tunapozungumzia kuongea, tatizo halipo kwenye kiingereza tu, bali hata kwenye kiswahili. Vijana wetu hawawezi dialogue. Ni kelele tu na nidhamu ya uoga.
 
Back
Top Bottom