Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

ketone

JF-Expert Member
Jan 22, 2016
508
622
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio shule mwanafunzi anayosoma, tatizo ni kumuandaa mtoto katika elimu yake ya msingi kwa kumfundisha kwa kutumia Kiswahili miaka zaidi ya 7 kisha baada ya hapo unambadilishia gear angani aanze kujifunza kwa kwa lunga ya Kiingereza kwa miaka 4 hadi 6 alafu ufaulu ukiwa duni watoto wanaitwa vilaza.

Kwani kinashindikana nini mitaala yote ya elimu yetu ikawa ya Kiswahili tuu level zote za elimu? Au ikawa ya Kiingereza tu level zote?

Tuchague moja kisha tupime ufaulu.

Mtag Ndaliwize.
 
Kimsingi elimu ya zamani huwezi kufananisha na sasa.
Walimu wengi wa zamani walitufundisha kwa upendo zaidi tofauti na sasa, kama huna uwezo waache wenye uwezo wawapeleke watoto wao English medium, wewe peleka wako huko kayumba,
Ukifika huko kayumba muulize mwl mtoto wake anasoma wapi? Upate majibu
Maana zamani watoto wa walimu tulisoma nao lakini siku hizi wanawapeleka English medium, sasa kama mwl tuu husika kampeleka mwanae huko, Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nikushauri tu mleta mada,wanasema ukipewa kilema unapewa na mwendo.


kama una nia ya dhati mwanao afike mbali kielimu,atafika ilimradi umeamua hivyo.yes ndio ,umekosa kabisa ada lakini muandae mtoto kusoma hiyo shule ngumu.kama akili anazo atapasua tu,ila kama kibungo hata ungepeleka wapi ataharibu tu.

kuna tuition,mazingira ya home,na mtaani,uki master hapo utafanikiwa.
 
English medium bado ni nzuri. Toa yale ya darasani utaona wana advantage kubwa kuliko waliosoma st.Kayumba. nimesoma government schools na huwa naona vitu gani nimemiss haswaa kwenye cycle yangu ya watu. At least kwa sasa ile jeshi, chuo na mihangaiko inakuletea more positive people

Asikudanganye mtu, kumpa mtoto mentality ya kuwa ni bora na kuzungukwa na vitu positive vitamjenga sana. St kayumba huwa tunapambana na negativities nyingi sana ambazo kwa wemgi huwabomolea confidence na spirit ya kufanikisha makubwa in life
 
Ukweli kwa dunia ya sasa na jinsi Teknolojia inavyoeenda kwa kasi
Lazma mtoto ajue English iwe cha kusoma na cha kuandika.
Hajalishi ataiishia wapi kielimu lakin ni muhimu sana kwa wezesha watoto wajua English

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uko sahihi kabisa. Ajue English kwa utaratibu wowote ule.

Mimi Binti yangu hakupata shida kufaulu form VI sababu hakuhitaji kufaulu English kwenye mchepuo wake.

Ila Chuo ( yuko nje ya nchi) mwanzoni amepata shida sababu alikuwa anamwelewa mwl ila kujieleza ikawa shida.

Kilichomsaidia ni room mates wake ambao wote hawajui kiswahili kabisa walimnyosha English yake sasa hivi yuko vizuri.
Ni muhimu kujua English mapema hilo halikwepeki.

Yale madarasa tulikuwa tunakaa @45 kwa darasa hayapo tusiwalaumu walimu.
 
Walimu wengi tuu watoto wao wanasomesha english medium. Nafahamu kadhaa wanaofundisha muhimbili, mbezi na bunge primary
tuzungumzie waalimu katika uhalisia wao,sio hao waalimu maalumu wachache,watoe hatima ya wengi.

kwamba waalimi siku hizi wanasomesha watoto wao eng medium.
 
Shule nyingi za St. Kayumba, kuanzia mandhari,idadi ya wanafunzi, (viijini lugha za asili), jamii ya hovyo, series, n.k vinakinzana na Elimu.
Kwa mtizamo wangu, mtoto alelewe vyema kwenye familia kisha apelekwe Medium.
Baada ya hapo anaweza kuwa mjanja kiasi
 
  • Thanks
Reactions: amu
Tafauta hela mzee mimi ni binafsi yangu nimesoma medium green hill primary school,aise foundation niliyopata siyo mchezo kingereza kinakupa confidence ya hatari sana ,kuna baadhi ya interview zilikuwa ngumu sana ili kwa sababu ya ugwiji wa lugha ya malkia nilipita bila shida lakini nilikuwa empty brain ..peleka mtoto akapate exposure na confidence aje kupunguza uwoga wa maisha!!
 
Back
Top Bottom