Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

Kwani ni lazima mwanafunzi asome English Medium?

walimu gani wanapeleka watoto eng medium,au unazungumzia wabunge??waalimu hawa hawa wa mishahara yenye makato ya bodi ya mikopo??
Mimi mtoto wa mdogo wangu ni Mwl. Temeke anamsomesha mtoto wake English Medium Mkombozi,kwa hiyo wewe na mawazo yako duni endelea kufikiri hivyo hivyo kuwa walimu hawawezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilisoma kayumba, nikipata hela kwanza wanangu watasoma shule za maana, na ndo maana nitachelewa sana kuwa na familia. Yaani nitalipiza kisasi, nina akili kama zote lakini natamka English ya kipuuzi kabisa ukichanganya na matatizo yangu katika kuongea. Mengine yote najua ila kutamka kimbembe.
 
Tatizo sio shule mwanafunzi anayosoma, tatizo ni kumuandaa mtoto katika elimu yake ya msingi kwa kumfundisha kwa kutumia Kiswahili miaka zaidi ya 7 kisha baada ya hapo unambadilishia gear angani aanze kujifunza kwa kwa lunga ya Kiingereza kwa miaka 4 hadi 6 alafu ufaulu ukiwa duni watoto wanaitwa vilaza.

Kwani kinashindikana nini mitaala yote ya elimu yetu ikawa ya Kiswahili tuu level zote za elimu? Au ikawa ya Kiingereza tu level zote?

Tuchague moja kisha tupime ufaulu.

Mtag Ndaliwize.
Ndaliwize mwenyewe leo kambwela mbwela [emoji23][emoji23][emoji23] alikuwa anam-mind mchina kwa kingredha ametoa maboko balaaaa bablai! Video ipo inazunguka WhatsApp humo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani English medium ni za private tu mkuu?
Mbona Government ina English medium nyingi tu? Wewe unaishi wapi? Kwa kuanzia tu kuna Olympio,Bunge, Diamonds,Mkoani nk
Chaguo ni lako, na magari yapo
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimesoma kayumba ila napambana wanangu toka nursery wapo hizo hizo medium, kayumba ukisoma usipokuwa mbishi kwenye maish hutoboi. Sitaki wanangu wapitie niliyoyapitia.
 
Ndaliwize mwenyewe leo kambwela mbwela [emoji23][emoji23][emoji23] alikuwa anam-mind mchina kwa kingredha ametoa maboko balaaaa bablai! Video ipo inazunguka WhatsApp humo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha bado sijakutana nayo lakini najua nitaiona tu. Hii wizara yetu ya elimu sijui wanaoiongoza huwa hawana plan B.
 
Hata mm naumiza kichwa xana Leo na kazi kesho kazi inaisha c unajua kazi za watu binafsi mguu nje ndani, sasa akianza private tena aje arudi government ck mambo yameenda mrama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kwa kufikiri kwangu ninaona sio lazima mwanafunzi apite English medium schools ndio academic performance yake iwe vizuri secondary.

Nilikuwa najaribu kuwaza hili maana nimeona mzazi anampeleka mtoto English Medium alafu huko baadae anamrudisha primary ya serikali kwa kukwama ada.

Mimi sioni kama kuna uhusiano mkubwa sana kwa elimu ya primary na secondary. Au English medium na secondary, hata kama upo ni mdogo sana.

Mbona secondary tulisoma na waliopita government kuanzia chekechea na walitandika A kote hadi English yenyewe A.

Ninaona kama una muda mzuri wa kusimamia elimu ya mwanao baada ya kutoka shuleni. Mfano ajisomee muda mwingi jioni na weekend baada ya shule na umpatie vitabu vya kutosha inaweza kumsaidia.

Nimeona wazazi wengi wanaona jirani kapeleka English medium naye anapeleka baada ya mwaka anarudisha government mtoto anabaki akishangaa.

Pia nimejaribu kutazama Walimu wa English medium sio kuwa wana elimu kubwa sana au uwezo mkubwa wa kufundisha hapana, ila ni ule uwezo wa kuwa karibu na watoto kwa kuwa ni wachache.

Hiyo wazazi acheni kuyumbisha vijana wenu leo huku kesho kule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio lazima. Hakuna sheria inayoelekeza ni lazima watoto wasome English medium.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weee unaakili Sana mwalimu anawatoto wanne kwa mfano hio ada atatoa wapi labda Kama ameekeza na sijui aliekeza lini

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hivyo kama angekuwa na uwezo wa kulipa ada za hizo shule angewapeleka huko English Medium za private?
Yaani wanatamani lakini hawana uwezo, sivyo?
 
Usidanganywe na mtu ipo tofauti kubwa sana kwa watoto wawili wenye uwezo sawa kiakili lakini mmoja kasoma English medium na mwingine Swahili medium ya serikali.
Mengine ni mbwembwe, wivu na sizitaki mbichi hizi huku unazitamani.
 
Mimi hill nimeshaapa nalo sio kama sina uwezo mwanangu anasoma primary ya govt then badae secondary nitampeleka huko panapostahili kama nilivyosoma mimi.
 
Wasiojua kiinglish kwa mfumo wetu wa kitanzania huu wengi huwa wanakosa kujiamini hata kama kitu anajua atashindwa kuchangia hapa nazungumzia mashuleni na vyuoni huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
English Medium kuna elimu bora,mfano kuna shule mtoto hawaruhusiwi kwenda na hela ni unampa maji tu kula ni hukohuko sasa njoo katika hizi za serikali mtoto anawaza hela ya shule asubuhi na akifika shuleni break kwa Mangi kununua icecream na visambusa ,,hapo darasani dawati mutu 5 kitabu kimoja, somesha English Medium 1-7, Secondary government
 
Back
Top Bottom