Kwani Mwigulu Nchemba ni nani bwana wewe?

Kwani Mwigulu Nchemba ni nani bwana wewe?

Yule aliyesema hata watanzania wakila nyasi lazima ndege ya rais inunuliwe? Mramba aliyekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi na rushwa? Serikali ya Mkapa iliyouza nyumba za serikali kwa bei ya karanga huku zingine wakipeana bure? Serikali ambayo mkuu wake ana kashfa ya kujiuziq mgodi wa makaa ya mawe? Serikali iliyouza NBC pamoja na assets zake zote kwa 15b? KAMA HUNA CHA KUSIFIA bora ufungue uzi umsifie Gentamycine jinsi anavyochangamsha hapa JF.
Kuna tuhuma za kuuza bandari, umezisikia?

Mimi sijui lkn
 
Mawazo yako mazuri ila mengine hayana ukweli pili mtu huwezi kuyakataa madhehebu yake kisa kuna mwanachama flani wa upinzani anasali huko ! Lakini ndiyo maana tunasema ni mtu wa watu wote na ni kiongozi wawote tofauti na kipara ambaye anataka awe mkristo kwa sababu anazozijua yeye
Mwambie akae mbali na mambo ya kumnunulia Askofu gari la zaidi ya milioni 400... yeye kama kiongozi anayetaka urais inamchafua.
 
Tangu nchi hii ipate uhuru sijawahi kuona waziri bora wa fedha kama Bazil Pesambili Mramba.
Kama ni timu ya mpira,serikali ya Mkapa ilikuwa Barcelona ya akina Iniesta,Mesi n.k
Mramba huyu huyu aliyehukumiwa mahakamani kwa ufisadi au mwingine? 😳😳😳

Dar 24 dot com Chrome.jpg
 
Unamfahamu Madelu Lameck Mwigulu Nchemba ? nimeguswa na kuamua kuandika makala haya kuhusu mbunge wa Iramba Singida Waziri wa fedha na baba wa familia ya watu wengi sana wanaomzunguka : Nitamuelezea Mwigulu kwa namna ninavyomfahamu kwa mambo yafuatayo :

Moja Mwigulu Nchemba ni mtu mwenye huruma na upendo haya yote yanaonekana katika maisha yake , anaidadi ambayo haina mwisho ya kusaidia watu Mwigulu hakusaidii mtu ili uende bali husaidia watu ili wafike anakusaidia huku ukiishi kwenye maisha yake yaleyale sio kubagua , atakusaidia na kukufanya ndugu hakuachi uende ! Mwigulu ni mwalimu , mlezi , mganga kwa wagonjwa faraja kwa wazee na wajane yatima ndio usiseme huyu ni kimbilio la wengi sana .

Mwigulu ninayemfahamu mimi nimtu wa kujituma kwaajili ya taifa lake halali , yupo tayari kubeba lawama ili mradi jambo muhimu la Kitaifa liweze kufanikiwa , nimsomi mwenye udaktari wa Uchumi elimu yake ya kweli kwani kaivusha Nchi katika wakati ambao Dunia inapita katika janga kubwa la anguko la uchumi .

Zaidi Mwigulu ni mtu mwenye moyo wa uvumilivu sana hasa anaposhambuliwa humkuti akijibu mitandaoni majibu yake daima atajibia bungeni haijalishi umemuandama namna gani yeye atakujibu kwa kutumia kanuni na jambo lenyewe lilivyo .

Mwigulu ni mtu wa maamuzi , sifa kubwa inayompasa kila kiongozi kuwa nayo sio mtu wa kuyumba yumba ana msimamo na jambo ambalo ni muhimu kwa wakati huo kwa taifa lake lakini zaidi ni mtu anayeshaurika , kusikiliza watu nadhani ni waziri wa kwanza Tanzania kuwa na uthubutu wa kusikiliza maoni dukuduku , changamoto za watu mbele ya hadhara huku kila mtu akinena anavyotaka .

Wengi tulishuhudia hili anapomaliza kusikiliza watu wanamkimbilia na kumshangilia hata ungekua wewe ungefurahi kuwa na kiongozi wa namna hii ya Mwigulu Nchema .

Kubwa zaidi ninalompendea Mwigulu Nchemba hana kinyongo na mtu kwa wizara anayoongoza angeitumia kama fimbo kwa wabaya wake lakini yeye huwatumikia wote kwa usawa kwani anajua akiwa kama waziri wa fedha hana mpinzani tofauti na baadhi ya mawaziri wanaotumia ofisi zao vibaya .

Kubwa na muhimu kwa Nchi Mwigulu ni Mzalendo sana kwa nchi yake mtiifu sana kwa watu wote anaowaongoza na mtiifu sana kwa Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
Kwa sasa Ndiye Waziri ambaye mataifa mengi ya Afrika yanatamani angekuwa ndiye waziri wao Mungu ametupa huyu mtu tumtumie .
Kanywe naye chai baada ya hapa
 
Sikushangaii ndugu ukifanikiwa Tanzania wewe ni mwizi pole sana tafuta hela
Kwani mimi nakula kwako au k a mwigulu, angefanikiwa kama angekuwa na uwezo wa kuzuia kifo aishi milele vinginevyo mnavyoviita mafanikio kwangu ni ubatili mtupu. Kaa na uchawa na upumbavu wako
 
Anafanya kazi nzuri mpaka sasa analipa mishahara , miradi inatekelezeka fedha za miradi na stahili mbalimbali zinashuka mpaka kwenye lower levels hiki kwangu ni kipimo kikubwa sana. Tafadhali mwigulu kazana unakwenda vizuri so far.
 
Back
Top Bottom