Kwani kuolewa ni utumwa, mpaka wanaume wakinipa ofa za lift na kinywaji nizikatae?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,407
Kwani nani kasema kuolewa ni utumwa? Yaani hata nikikutana na mwanaume niliyecheza ama kusoma naye nimkimbie? Hata ofa ya kinywaji niikatae??

Screenshot_20220625-161935.png
 
Ahaa! Ok.
Lkn mm nilidhani ingekifaa kama kila mtu ajichunge mwenyewe badala ya mwanamke kutazamwa kama mtoto mdogo.

Mpk kaolewa maana yake ni mtu mzima anaelewa baya na zuri.
Dini zimetufunza kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu hata akiwa na miaka 60 bado ni dhaifu. Hivyo ni mwepesi sana kurubunika hata kwa Pipi kijiti tu inatosha sembuse Bia.

Sasa wewe unapambania upewe ofa ya Bia ili uje usingizie Shetani alikupitia kumbe ni wewe mwenyewe umejirahishishia kazi ya kuja kuliwa kimasihara.
 
Kuna siku niliwahi kuona timbwili jamaa kachomoa mguu wa kuku kisa chenyewe cha kitoto eti jamaa kampa offer ya bia mkewe mbele yake.
Sio kisa cha kitoto bro. Mwanaume uliyekamilika huwezi ruhusu dume mwenzako atoe huduma/ofa kwa wife halafu ww ukiwepo, hata kama ni favor. So yuko sahihi huyo jamaa.

Hapo ni mwanaume ndiye atakaeelewa nilichoandika, mvulana utaona mapicha picha tu ambayo haya-make sense. Ila ukikua utaelewa.

Sent from simu ya kuunga unga
 
Ofa? hebu rudia tena huku ukilitafakari neno lenyewe, OFA tena ya pombe?😂

Kama ni mwanamke tu niliyenaye ye apewe tu hizo ofa, ila kama ni mke there's no such a room unless iwe ni kutoka kwa watu nisiowatilia mashaka (ndugu wa karibu wa damu ninaowatambua), na isiwe pombe au lasivyo niwepo pia.

Lakini pia kama ofa imetolewa kwa group including my wife siwezi kumind as long as the one offering is known na sina mashaka nae, ikiwa selective lazima ni judge.

NB: MKE WAKO ANAPEWAJE OFA NA WATU USIOWAJUA KISHA UTULIE? Labda kama ulikuwa unazungumzia Malaya nitaungana na wewe. Tafuta hela umpe anachotaka aache kudowea.
 
Back
Top Bottom