Kwani hii Nchi haina Lejendari hata mmoja wa soka apewe jina la uwanja?

Engager

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
1,376
2,914
Viwanja vyote vya soka hapa kwetu vilivyopewa majina ya watu ni majina ya wanasiasa tu.
Benjamini mkapa
Ali Hassan Mwinyi
Sokoine
Amri Abeid
Karume.....etc, nasasa uwanja unajengwa Arusha, hata mkandarasi hajaingia kazini tayari umeshaitwa Samia.

Wanasiasa mbona mnakuwa wabinafsi hivo aisee. Inamaana hatuna lejendari hata mmoja kwenye soka la Tanzania tukampa uwaja jinalake walau tuwe na kitu cha kumkumbuka? Nyie mbona hamridhiki?
Viwanja
Barabara
Kumbi za mikutano
Viwanja vya ndege
Stendi za mabasi
Masoko
Mahospitali...etc, vyote vimebabe majina yenu tu.
 
Wanasiasa wamehodhi kila kitu kwa ajili ya political mileage, hao walijendi wenu hata timu zao tu haziwatambui.
 
Kama hawewezi kutoa jina la mchezaji kwa ajili ya viwanja, basi hata majukwaa wayape maiina yao, mfano badala ya kuita vip b ita lunyamila, machungwa ita machupa nk
 
Gamondi angekuwa wakwetu tungempa jina la uwanja, lakini ndo hvo Tena.
 
Kama hawewezi kutoa jina la mchezaji kwa ajili ya viwanja, basi hata majukwaa wayape maiina yao, mfano badala ya kuita vip b ita lunyamila, machungwa ita machupa nk
 
Kwa kumbukumbu kidogo nilizo nazo, kuna watu walitoa burdani sana katika medani ya soka.
Manara aka Computer
Jela Mtagwa ( picha yake iliwahi kaa ktk stemp za barua)
Peter Tino ( Goli lake lilitupeleka mashindano fulani)
Leodigar Tenga
Zamoyoni Mogella aka Golden Boy
Edibilly Lunyamila
Idd Pazi
 
😁😁... Hali Mayai Tembele Complex

Hivi Utopolo Si Walisema Watajenga?

Hili Jina Mbona Linaonekana Litafaa!
 
Umefkiri Nje ya boksi....wazo jema sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…