Kwangu mimi "Kikwete is the wisest Tanzanian president ever, he's intelligent"

Fene

JF-Expert Member
May 4, 2021
2,458
3,433
Mwamba ni wa kitambo,

Ameshuhudia mengi, kabla hajawa raisi na hata baada, na hata baada ya kukiachia kiti Mwamba inasemekana alipendekezwa kitambo sana na wenye akili aje aliongoze hili taifa

Mwamba anongozwa na akili na si mihemko na ndio maana nadra kusikia kafanya maamuzi ya hovyo
Mwamba anasemwa sana at sometimes mara asifiwe mara akumbukwe lakin ana-smile tu , hata matusi pia at sometimes hutukanwa mpaka unaweza jiuliza mwamba hasikii but this mwamba he's intelligent & wise hasukumwi na mihemko
Lakin yote kwa yote naamini anawapenda Watanzania that's why he ignores
Kuna mengi mazuri ya huyu mtu mtu

Mheshimiwa Kikwete kabla hujaondoka siku moja tungependa tusome kitabu chako kwa hakika kuna mengi mazuri tunaweza jifunza hususa namna ya kuishi na watu
Forever u will be remembered na sisi Watanzania wanafki

Nb/Simjui hanijui na mimi wala si chawa tuheshimiane tafadhari😂😂
 
Mimi kwa upande wangu. Kikwete ndio best president ever aliyewai kuhudumu miaka 10. Nyerere peke yake ndie anamzidi kikwete kwa uongozi bora na Nyerere katawala miaka zaidi ya 20

Mama sijamaliza kumpima sababu bado sijaona miaka 10 yake atatuongozaje..
 
Moja kwa moja kwenye mada,jana tulikuwa kwenye msiba wa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania,mhe Edward ngoyai lowassa,(mwenyezi mungu amjalie pumziko la milele). Kumekuwa na watu wanamtizama kikwete kama ndio kikwazo cha lowasa kuingia ikulu. Na mimi nina sema,kama ni kweli jakaya kikwete ndio alizuia lowassa asichaguliwe,basi tumpongeze kikwete kwa kuipenda nchi na kuzuia mwizi kuingia madarakani.

Lowassa hakukataliwa kipindi cha awamu ya kikwete tu,hata kipindi cha mwinyi jina lake lilikatwa na kamati ya maadili mapema kabisa,na cc pia ikaja ikapigilia msumali wa mwisho kwenye jeneza la kuteuliwa kipeperusha bendera ya ccm kwa lowassa,na ndoto za lowassa kuwa mgombea urais kupitia ccm zikazikwa rasmi.

Kwenye nchi yetu hii,hakuna waziri mkuu aliyewahi kujiuzuru kwa kashfa ya ufisadi kama lowassa,tena kwa ushahidi na vielelezo,si hivyo tu lowassa amekuwa mwizi kutoka akiwa aicc. Nashangaa leo kikwete alaumiwe kwa kumzuia mwizi kuingia ikulu?!. Yaani urafiki wa kutafutiana mademu ufikie mpk kuachiana nchi!?. Hivi hawa watu kweli akili zimo na zinawatosha.

Mwisho hongera kikwete kwa kumzuia mwizi kuingia ikulu.
 
Ukweli unajulikana wakati wa vifo na maziko ya wafu hamna Cha kufanya acha tuendelee na maisha na wenye kufanya Toba wafanye. Msaliti hukosa amani maisha yake yote. Karma is also real and has a regular and perfect tendency of reciprocity. You can imagine Lowasa amekufa kabla ya Mwakyembe, Mungu fundi, Lowasa aliwatesa sana wapinzani Kanda ya kaskani leo yuko wapi chini ya maudongo huko fyiuu
 
1708239925686.jpg
 
Tangu Jana jioni naona kuna nyuzi zinafyatuliwa tu za kumsafisha Mkwere.

EPA, RICHMOND,BUZWAGI,DOWANS,SYMBION.

Hayo yote madudu ya utawala wa Kikwete. Lowassa alijiuzulu kwa Richmond japo ukweli unajulikana alifanya kuiokoa serikali ila Kikwete akamgeuka hapo hapo,hayo madudu mengine ya utawala wa Kikwete vipi?!!
 
Mwamba amewafanya watu wa kaskazini waweweseke kwa maisha yao yote,wanatamani wamfikie wamfinyange finyange wammeze.
 
Mkuu Umeuishi utawala wa nyerere?

Nimeusoma.. utawala wa nyerere unaonekana kwa macho hata kwa kuusoma tu. Kitendo cha kutuunganisha wa Tanzania kutokuwa na ukabila ni ushahidi tosha wa kuonesha alikuwa kiongozi bora..

Viwanda alivyojenga na mali kibao za uma zilizopatikana awamu ya nyerere nimeziona wakati nikiwa mdogo. Kabla Mkapa hajaja kuviuza kifisadi na vingine kujiuzia yeye na familia yake
 
Tangu Jana jioni naona kuna nyuzi zinafyatuliwa tu za kumsafisha Mkwere.

EPA, RICHMOND,BUZWAGI,DOWANS,SYMBION.

Hayo yote madudu ya utawala wa Kikwete. Lowassa alijiuzulu kwa Richmond japo ukweli unajulikana alifanya kuiokoa serikali ila Kikwete akamgeuka hapo hapo,hayo madudu mengine ya utawala wa Kikwete vipi?!!
Kikwete halaumiwi kwa sababu ya ufisadi wake,kikwete ana laumiwa kwa kumsaliti rafiki yake lowassa asiingie ikulu.kama ni ufisadi woote wale ni majizi,lkn lowassa yeye mpk na ushahidi wa memo na maelekezo,aliyekuwa waziri wa nishati na madini kipindi kile alieleza kila kitu mbele ya kamati.na bahati nzuri alikuwa ametunza vielelezo vyote kutoka kwa lowassa.leo lowassa eti amegeuka kuwa ni malaika,na kikwete eti alitakiwa amuachie nchi baada ya yeye kuondoka.
 
Mwamba ni wa kitambo,

Ameshuhudia mengi, kabla hajawa raisi na hata baada, na hata baada ya kukiachia kiti Mwamba inasemekana alipendekezwa kitambo sana na wenye akili aje aliongoze hili taifa

Mwamba anongozwa na akili na si mihemko na ndio maana nadra kusikia kafanya maamuzi ya hovyo
Mwamba anasemwa sana at sometimes mara asifiwe mara akumbukwe lakin ana-smile tu , hata matusi pia at sometimes hutukanwa mpaka unaweza jiuliza mwamba hasikii but this mwamba he's intelligent & wise hasukumwi na mihemko
Lakin yote kwa yote naamini anawapenda Watanzania that's why he ignores
Kuna mengi mazuri ya huyu mtu mtu

Mheshimiwa Kikwete kabla hujaondoka siku moja tungependa tusome kitabu chako kwa hakika kuna mengi mazuri tunaweza jifunza hususa namna ya kuishi na watu
Forever u will be remembered na sisi Watanzania wanafki

Nb/Simjui hanijui na mimi wala si chawa tuheshimiane tafadhari
pamoja na kampeni kubwa mno kumuonesha jk ni mbaya,hawatafanikiwa,ataibuka mshindi tu
 
Back
Top Bottom