Kwako Yatima Anna Zambi (16)

Kwako Yatima Anna Zambi (16)

Hapa ndipo maswali mengi yanaibuka kuhusu muumba we mbingu na nchi, mwenye-enzi yote na uwezo wote. Ukifikiria sana unaweza kuvuka mipaka...
Tumshukuru tu kwa yote...mema na mabaya yote yanatoka kwake
 
Uzi mzuri sana,ndugu anaekupenda wakati una hela muangalie mara mbili mbili,kwani usije kufikiria siku mambo yako yakiwa hovyo utamuona.Iliwahi kuikuta familia yangu wakati mzee wangu aliekuwa na uwezo mambo yalipokuwa sio mazuri,ndugu na marafiki wote waliingia mtini,tulipambana na ndugu zangu kila mtu kivyake mpaka hatimaye tuliweza kufikia kujitegemea,tuwe makini sana ndugu zangu...
 
Mungu ana msaada gani kwa huyo binti kama yeye ndie alieamua kuchukua familia yake nzima
 
Ushauri wangu kwakwe ufunge mdomo asijaribu kukufuru,mungu ana makusudio yake kwa kila jambo
 
Hata mimi nina hiyo sera ya kumsaidia aliyenisaidia, sio walime wengine halafu waje kuvuna wengine.
Nilkuwa nafikira kama hizo lakini nikaja kutambua kuwa ni bahati sana kuteuliwa na mwenyezi mungu na kukufanya chombo cha msaada kwa mwenzako.Kitendo cha kujenga imani ya kwamba sisi ndio watoa msaada na si mwenyezi Mungu kupitia kwetu,kimeufanya msaada wa kibinadamu uwe wa kibaguzi na hauzai matunda ya baraka.

Ni vizuri kurudisha shukrani,lakini nguvu ya msaada wako isitoke kwenye wema uliotendewa bali kwenye huruma kwa mwanadamu mwenzako hata kama hakuwai kukupa msaada.

Ukiwekeza katika kurudisha wema kwa mabaya uliyotendewa hapo lazima uone matunda ya uwekezaji wako hadi vizazi vyako watafurahi.

Mfumo wa kishetani ni ule wa kurudisha baya kwa baya.Mfumo huu unazaa matunda mwanzoni na yanakuwa kama ni baraka furani lakini badae matunda hayo yanakuwa ni mateso kwako na kwa kizazi chako kwa badae.

Kwa kifupi,mfumo wa kishetani unasema,ukitaka mafanikio (mara nyingi ni mafanikio ya masharti kwa sababu ni ya muda mfupi) hakikisha unasababisha maumivu au auondoi maumivu kwa mwenzako.

Mfumo wa Mwenyezi Mungu ni kinyume kwamba ukitaka kufanikiwa duniani na huko mbinguni hakikisha unawekeza katika kuondoa mateso kwa mwanadamu mwenzako awe ndugu au sio ndugu,awe wa dini yako au sio wa dini yako,awe ni mwenye dhambi au mwema we timiza tu .UPENDO WA KIMUNGU HAUBAGUI.
 
Back
Top Bottom