Liverpool_Jr
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,220
- 1,417
Naitwa Mr. Liverpool A.K.A Kop mimi ni yatima kama wewe niliyepitia shida nyingi.
Kwanza kabisa nilizaliwa 1989 na wazazi Matajiri sana. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana na mama alikuwa ni mama wa nyumbani.
Maisha nyumbani yalikuwa mazuri sana, yenye raha na ndugu walikuwa kibao kila mtu kuja kulia shida kwa baba.
Baba alipata stroke 1998 na kufariki ghafla, mama alikuwa mama wa nyumbani asiyejua kuendesha vitu vingi vya baba, maana alihakikishiwa maisha mazuri na mumewe, then alikaa tu nyumbani kuhudumiwa.
Mali nyingi za baba zilitapeliwa na rafiki pamoja na ndugu waliokuwa wakilia shida kwa mama na baba.
Ghafla maisha ya nyumbani yakaanza kuwa magumu. Shule nikahamishwa kutoka English medium mpaka kayumba (hela ziliisha zote mpaka za ada).
Kwa kuchanganyika, mama akaanza kuumwa sana. Nikawa namuombea sana na kila mara kuongea na Mungu asimchukue mama. Ghafla mama alizidiwa akafa.
Aisee kile kifo kiliniuma sana. Nikaanza kumlalalamikia sana Mungu: "Baba akiwa anaumwa nilikuomba sana apone ila ukamchukua, mama naye nimekulilia sana naye kafa, kweli wewe Mungu upo?"
Kujibu hili swali ziliruhusiwa shida hatari.
Kula kwa siku mara mbili. Ukienda kwa ndugu wanakuona unaenda kulia shida, "We kila siku unakuja kuomba hela kwetu, hakuna ndugu wengine?"
Nilikuwa nikienda kuomba hela za tuition na mitihani ya kujipima na mahitaji ya shule. 2001 nilijiapiza "sitomlilia ndugu yeyote shida, nakomaa nazo mpaka ziniue"
Nimekulia maisha ya shida ya kukondaa balaa. Ya kukosa hata 50 ya nauli ya kupanda daladala kwenda shule.
Nikiwa form one nilijiapiza "Elimu ndiyo mkombozi wangu, nitasoma sana"
Nilisoma balaa kwa njaa na ugonjwa (nilishawahi kwenda shule kichwa kinauma mpaka mzee mmoja njiani alishtukia!)
Nilijiepusha na bangi, unga, sigara, pombe na vyote (maana mitaa niliyokulia hivi vitu ni kawaida sana, vijana na watoto wengi waliharibika na miongoni mwao ni wenzangu).
Kwa msaada wa shangazi na wazazi wa rafiki zangu, maisha yakaenda, Form 4 ikaisha, mara Advance, mara chuo.
Kutoka tu chuo nikaajiriwa. Ashukuriwe Mungu sasa nimejiajiri.
Walewale ndugu kila mara wanapiga simu kuomba msaada. Huwa nasomaga SMS zao na kuzitupa kwenye dustbin.
Huwa nasaidia walionisaidia tu.
Kuna ndugu mmoja nikiwa form 2 nilishawahi kumwambia, "Ukinisaidia Mimi unakuwa unawekeza". Na kweli, amefariki na mimi ndio nasaidia familia yake aliyoiacha.
Kilekile kidogo alichonipa (kuninunulia vitabu form 2 tena viwili) basi narudisha kikubwa kwa familia yake.
Japo huwa najitahidi kuwasaidia walionifungia milango nilipoenda kuwaeleza shida zangu tena nikiwa mtoto, ila wengii nawafungia vioo (Mungu anisamehe kwa hili).
Baada ya vifo vya wazazi...
1.Nilimlalamikia sana Mungu.
2. Niliwaandikia sana barua wazazi wangu na kuziweka kwenye kabati la nguo zao (sijui kama walikuwa wanazisoma).
3. Nilishindwa kwenda kwa rafiki zangu, maana nikifika na kuwaona vile wanaishi kifamilia, niliishia kulia tu.
Nachotaka kukwambia:
1. Wale wale waliojifanya wapo karibu na familia yenu, watakukimbia.
2. Wale wale waliokua wakikupenda, ndio watakao kudhulumu.
3. Wale wale waliokua wakileta shida zao kwa Mzee Zambi, ndiyo watakao kimbia shida zako.
Jipe moyo mama. Pambana.
Mungu yupo na YUPO KWELI.
Japo ukiniuliza mpaka leo "Kwanini Mungu hakusikia maombi yangu asichukue wazazi wangu?" Jibu SINA.
Nachojua Mungu yupo na ananipenda na alinipigania sana.
Usikate tamaa Mungu yupo.
Maisha ya uyatima NYOKOO SANA..!!
#ASANTE
#YNWA