Kwako Mzee Mwinyi, idhibiti furaha yako isikufanye kuchanganyikiwa!

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,501
27,001
Heshima yako Mzee wetu.

Sina shaka na busara zako, umelitumikia vema Taifa letu, na hata sasa umekuwa ukitumika kama mshauri.

Kitendo cha kutamani kugawa ‘nyongeza’ ya mhula wa utawala, kama zawadi kwa mtu fulani kisa ‘amekurejesha’ ikulu, ni ulevi wa madaraka kama sio kuchanganyikiwa.

Taifa linawategemea wazee kama nyie, kwa heshima kama washauri, hebu ona sasa mnavyoonesha ubinafsi hadharani!

Nchi sio mali yenu binafsi, ingawa mmekuwa mkijimilikisha siku zote. Yamekuwa yakisemwa mengi kuhusu ‘kugawa’ rasilimali za Taifa kwa maslahi binafsi, hili ni moja ya kuthibitisha ukweli wa yaliyosemwa.

Kwa heshima nawajibika kukukumbusha hili, usitoe ahadi ukiwa mwenye furaha sana. Bila shaka kwa sasa unajutia kauli yako iliyopingwa hadharani, kamzawadie kwa namna nyingine kakutendeeni makubwa sishangai.

Miaka mitano ya zawadi, kwa sababu hiyo tu.? Nchi ni yetu sote, nasi zamu yetu ifike.

Wasalaam,

Ncha Kali.
 
Kwa kifupi tu madiwani hawajalipwa mishahara, wafanya kazi wa serikali hawana pata nyongeza ya mishahara mwaka wa tano huu.

Ungeniwekea Ushahidi ' Vivid ' kabisa juu ya haya Madai yako hapa hapa Jamvini JamiiForums ningekuamini ila nachukulia huu kama ni Uzushi tu.
 
Back
Top Bottom