Kwako Mh. Lyatonga Mrema.

Kwako Mh. Lyatonga Mrema.

msnajo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
3,066
Reaction score
1,142
Mhe. natanguliza salam zangu kwako. Kwa muda mrefu umeweka historia nzuri ya uwajibikaji kama mpinzani wa ukweli. Japo msimamo wako haueleweki sana hadi watu wanahisi kuwa wewe ni mbomoaji wa upinzani badala ya kujenga.

Na hata umekuwa mtu wa kung'ata na kupuliza na ukawa vuguvugu! Kuna hili swala la posho za wabunge, ambapo kimsingi zinaonekana kuwa ni mzigo kwa Watanzania na imeshauriwa na baadhi ya wabungu zifutwe ili kiasi hicho cha bil 900 kielekezwe kwenye huduma za jamii.

Ukiwa miongoni mwa watumishi wanaonufaika na hizo posho wakati una mshahari mkubwa wakutosha kukidhi mahitaji hujasikika kwa lolote haza kufutwa kwa hizo posho! Inadhihirisha wazi kuwa nawe huna msaada sana kwa wananchi kwani una mind hiyo miposho.

Tafadhali hebu toa msimamo wako tujue kuwa huna undumilakuwili. Samahani kama huu ujumbe utakukera, ni kwamba bado ninakutambua na ningependa kutambua uwepo wako bungeni Hh. Kwa mwana jf yeyote nawe unaruhusiwa kuchangia hii mada.

Asanteni
 
Yuko kimaslahi zaidi,hawezi kuitema posho huyo.
 
Aise biashara imechanganya hawezi kuacha, alisha sema alikuwa amefuria sasa amerudi
 
Lyatonga alisema hizo posho amezikuta na yeye anazichukua tu maana hao walioziweka walikuwa na maana yao
 
Mrema hawezi kuacha posho nyie, labda wamuue, Yaani mzee wa Kiraracha kweli aseme sihitaji hii poso wacha iende Vunjo kwa wapiga kura wangu??!!, Lo napata taabu kidogo.

Inataka moyo wa uwajibikaji kukataa pesa. Wenye uthubutu huo ni wabunge wa CDM tu, hawa ndo wana uchungu na maisaha ya waTZ. achana na kina Mrema, kwanza kura alizopigiwa zilikuwa za "huruma" tu.
 
Hivi uliyeuliza swali hujui kama Mh. Mrema ni Mchaga?
 
Hivi uliyeuliza swali hujui kama Mh. Mrema ni Mchaga?

phyliss-Violence_against_Muslim_women.gif
 
Back
Top Bottom