Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 27,137
- 65,467
KIJANA MASKINI UNATAKA NYOTA YAKO ING'AE KISIASA NA WAKUBWA WAKUCHAGUE. HIVI NDIVYO UTAKAVYOFANYA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuna vijana maelfu kwa maelfu wapo kwenye siasa miaka na Miaka lakini hawatambuliki, hawajulikani, hawaonekani na zaidi wanaishia kuwa vibaraka vya wakubwa wakilamba nyayo za Wakubwa.
Sio kwamba nafasi hiyo ya kulamba viatu wanazipenda hasha, hawana jinsi. Nyota Yao ipo chini Sana.
Miaka nenda Rudi kuvalishwa mashati yenye majina ya watu wengine. Miaka na miaka kuvaa mavazi yenye kauli Mbiu za Wakubwa. Sio kwamba wanapenda. Hali imewalazimu.
Kazi yao kudandia dandia watawala kama Ngedere anavyodandia matawi ya miti. Alipokuwa Kikwete wakadandia tawi la Kikwete, alipokuwa Magufuli wakadandia tawi la Magufuli, sasa ni Samia wamedandiamo tawi la Samia. Kudandia Napo kwahitaji moyo, uvumilivu na pumzi. Wengine pumzi ikakata wakaamua waendelee na mambo mengine. Kudandia matawi miaka ishirini tangu Kikwete Mpaka Leo sio Jambo dogo. Ni miaka mingi Sana.
Mbaya zaidi wanazuka watu pasipojulikana wanapewa vyeo na kuwaacha wadandia matawi kurukiarukia matawi.
Sasa Mimi Mtibeli nikasema, isiwe kesi nitawapa ABC za kufungua lango la kuonekana kwa Wakubwa..
Lazima uelewe Saikolojia ya watu Wakubwa na watawala hii itakusaidia katika kupanda kwako ngazi au wao kukupandisha;
Saikolojia ya watu Wakubwa ni kama ifuatavyo;
1. Heshima kwao sio kipaombele. Kipaombele cha watu Wakubwa ni MATOKEO.
Usilete lete heshima kwa watu Wakubwa. Kwao haina maana yoyote Ile. Kwa hadhi yako umheshimu au usimheshimu kwake haina maana yoyote.
Kwanza cheo chake tuu anajua lazima aheshimike. Hivyo usimpe mtu kitu ambacho kwake kipo na ni uhakika.
Watu dhaifu, wanyonge, na wasiojiamini kwao heshima ndio kitu cha thamani kwa sababu hiyo heshima hawana uhakika NAYO, hawako NAYO.
Hivyo unapokuwa mbele ya watu Wakubwa na watawala jitahidi kuonyesha wewe ni mtu wa matokeo chanya.
Kwa sababu Wakubwa wao hufikiria namna utakavyowapa faida, matokeo chanya.
Elewa, Wakubwa hata usipohitaji ukaribu nao, au hutaki kujiingiza kwenye mambo yao ya siasa. Kama wameona kuwa utawafaa na wewe ni mtu wa matokeo chanya watakuchukua iwe direct au indirect.
Mfano, kama wewe ni Chawa kama ndugu zangu kina Lucas Mwashambwa Wakubwa hawataangalia vile unavyowafanyia kazi ya uchawa, vile unavyowaheshimu.
Nope! Wataangalia, je katika uchawa wako Una - Fans Base ya kiwango gani.
Kama fans base yako ni kubwa kumaanisha unawafuasi wengi na wanakusikiliza na wanakuona kama Role model wao. Basi watawala lazima wataona unatija na utawapa matokeo Yale wanayoyataka.
Unaweza humu kuwa chawa miaka na Miaka lakini kama huna fans base kwa upande wa mitandao ya kijamii elewa kuwa Kazi unayoifanya ni Useless kwa Watawala.
Nakukumbusha, kuwa mtu wa matokeo kwa sababu Wakubwa wanahitaji watu wa MATOKEO.
2. Uwe na Mvuto ambao Watawala watautumia kwa Mambo yao ili nawe mambo yako yaende.
Kuna kanuni ya wajina wangu, Robert Greene inasema "Never outshine your Master"
Ni kweli huenda Nyota yako ni Kali kuliko watawala Hilo hata watawala wanaweza kulijua na kuliona. Lakini jitahidi Mvuto na Nyota hiyo ionekane kuwa Watawala ndio wamekufanya ung'ae hivyo.
Yaani Onyesha kuwa mtawala ndiye kakufanya kuwa hivyo.
Elewa kuwa, wananchi wengi ambao hapa ni watawaliwa huathiriwa na kile wanachokiona na kukisikia kuliko kile wanachokitafakari.
Ndio maana Media zinanguvu zaidi kwa watu wa kawaida na chini.
Unapofanya biashara yako mtawala ataiunga mkono kadiri wewe ulivyomsapoti na kumpa matokeo.
Kuna Mvuto wa kikata kiwilaya, mkoa, kitaifa na kimataifa.
Kwa vile sitaki kukuchosha. Basi tumalizie namna utakayofanya ili kupanda juu au kuonwa na Wakubwa ukawa kundi la Wakubwa;
1. Kuwa ujuzi Fulani kwa kiwango cha juu kabisa.
Usiwe mtu wa kawaida. Kama ni Daktari kuwa Daktari Bingwa, kama ni Mwanasheria kuwa Mwanasheria mbobevu.
Kama ni Injinia kuwa mtabe.
Kama ni mwandishi kuwa mwandishi mahiri kama Taikon Master hapa.
Kama ni Askari kuwa na ujuzi wa Hali ya juu katika fani yako.
Iwe ni MC, mshonaji, mpenzi, dereva n.k.
Ukiwa kawaida au below utaishia chini siku zote. Labda uwe mtoto wa watawala au ndugu, au uolewe au kuoa kwa Watawala.
2. Uwe na Msimamo na mwaminifu.
Lazima falsafa zako watawala wazijue. Lazima wakujue kuwa wewe ni mtu wa Msimamo kumaanisha wewe ni mwaminifu. Kama ni mbaya kuwa mwaminifu kwenye ubaya. Kama ni mwema kuwa mwaminifu kwenye wema. Na isiwe kwa mdomo tuu huku moyoni unawaza mengine huo ni unafiki siku zote wanafiki huwa Wasaliti.
Nilikuambia Wakubwa wanahitaji watu wa MATOKEO na huwezi kuwa mtu wa matokeo kama sio mwaminifu yaani hauna Msimamo.
3. Usiwe na Kiherehere. Usiwe na mdomo mdomo na kuongea mambo yasiyomhusu au kukandia wengine.
Kama hukupewa Kazi ya kutafuta taarifa Fulani na mtawala ukasikia anaulizia habari fulani hata kama unaijua hiyo taarifa usiwe na Kiherehere kuitamka.
Labda kama taarifa hiyo inahusu usalama wa mtawala husika.
Usiwe roporopo.
Siku utakayotoa taarifa ambayo haukuombwa na hiyo taarifa haihusu usalama wa mtawala husika ndio siku hiyohiyo ambayo uaminifu wako utaanza kutiliwa Shaka.
Kuwa msiri. Kitu hujaulizwa usiseme. Hujaombwa ushauri usitoe ushauri. Kaa kimya.
Taarifa ikiletwa ambayo unaijua, na kwa hakika kama ulikuwa unaijua Muda inamaanisha tayari akili yako ilishaandaa majibu ya kutosha ya kushauri.
Ikatokea Mkuu akaomba ushauri na wewe upo kwenye kundi linaloombwa ushauri. Basi unaweza kuutoa huo ushauri.
Ushauri utakaoutoa utawashtua wengi kwa sababu hawajui taarifa hiyo ulikuwa nayo Muda mrefu wakati wao wakiwa kwenye kuchanganyikiwa kutokana na upya wa taarifa hiyo. Kwako utapew Credit kuwa unaakili hata kama hauna.
Tofauti na ukisema taarifa hiyo ulikuwa unayo. Hata ukishauri ushauri wako hautakuwa na thamani ingawaje unaweza kuwa mzuri na kutumika.
4. Usipende kujiweka kwenye Makundi ya Kisiasa. Ingefaa kama usipokuwa na kundi.
Sio uigize hauna kundi. Hakikisha hauna kundi. Jitahidi usimamie katiba ya chama husika ulichopo.
Jitahidi panapotokea uhasama wewe uwe msuluhishi na mpatanishi. Waeleze na wakumbushe ninyi bado ni chama kimoja. Hampaswi kugombana kwani hiyo itawapa nguvu wapinzani wenu.
Elewa, watawala huwaamini zaidi wale wasio na Makundi kuliko wenye Makundi.
Wenye Makundi Wana maslahi Fulanifulani hivyo maslahi hayo yasipofikiwa usaliti ni Hakika. Yaani mtu anaweza kuhamia kundi hasimu na kutoa Siri za upande mwingine.
Inapotokea mtawala amemtumbua mtu wa kundi lake vita vya ndani huwa kubwa Sana tofauti na kumtumbua ambaye hakuna na kundi ambaye huona ilikuwa bahati yake tuu.
5. Usionyeshe wewe unauwezo mkubwa kuliko wengine Bali uwezo wako watu wauone wenyewe.
Kadiri unavyotumia nguvu kubwa kuthibitisha unauwezo ndivyo inavyothibitika hauna huo uwezo.
6. Usiingilie Mambo yasiyokuhusu ikiwa hayakudhuru.
Kisiasa kila mtu anamaslahi yake. Unapoingilia maslahi ya wengine unatoa kibali cha watu wengine kuingilia mambo yako.
Jambo lolote lisilo kuhusu ambalo hujashirikishwa hata kama unaliona au kulisikia achana nalo kama halikuhusu.
Ikiwa itatokea, mtu Mmoja anaonewa, akakuomba msaada, na mtu huyo anayeonewa ni mwema unaweza ingilia hiyo Kesi kwa kukutana na anayemuonea.
Lakini ikiwa moyo wako unakulazimisha kumtetea mtu anayeonewa na ubinafsi ya kufanya chochote ikiwemo kusema, basi huo ni utume. Unaweza kuingilia lakini ingilia kwa uwezo wako usizidishe.
7. Usikae Kikao chochote cha Kumfanyia mtu fitna, kumpangia Njama au hila.
Wazo lako, NENO lako, rasilimali yoyote kutoka kwako usithubutu kuitumia kufanya Njama, hila au zengwe ikiwa wewe sio mtawala.
Utafanya hila, Njama au zengwe kwa adui wa taifa. Adui anayehatarisha usalama wako na mtawala ambaye upo chini yake. Lakini Hakikisha hila, zengwe au Njama hiyo haivuki mipaka ya HAKI.
Yapo makosa ambayo ni HAKI mtu kuuawa katika ulimwengu wa kisiasa na kijamii. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, zinazuia au zinaruhusu. Makosa hayo ni kama ifuatavyo;
a) Uhaini.
Kwa tafsiri ya HAKI ya Uhaini wenyewe. Na sio kwa maoni ya mtawala.
b) msaliti na mtoa Siri za nchi na kijeshi ambazo hazitakiwi kutolewa.
c) Anayelala na mke au Mume wa mtu.
Makosa hayo unaweza shiriki vikao vya kupanga hila, Njama au zengwe na kuruhusu mauaji.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam