Kwaherini Star times

na nyie wa Dstv wekeni mada yenu mtuambie kwanini tununue Dstv, mleta mada katuambia Azam sasaivi wana local channel, Dstv vipi zipo? maana siwezi acha kuangalia habari za ndani, japo burudani muhimu. Binafsi natumia start times nawaza niamie wapi sijapata jibu.
 
Watz sijui nani aliwaroga. Yani asilimia kubwa ya wanaotumia DSTV hujiona wenye hela na wajanja. Yani huhisi wapo ulaya .
Umenunua DTSV kwa 99,000 na unalipia kifurushi cha 19,000 huzidi hapo ilhali mwingine kanunua Azam 150,000 na analipia Sh. 18,000 unajiona mwenye hela na uliyeendelea.
Huwa nawafananisha na wale wanaosema hawapendi movie zilizotafsiriwa alafu unawakuta wanaangalia movies za Jet Lee wakihisi anaongea kiingereza kumbe zimetafsiriwa pia kutoka kichina kuja kiingereza. Simply unagundua anajikweza tu kuwa anajua kiingereza
Dah! Mkuu hata mie huwa nashangaa yani mtu kifaransa hajui ila anaangalia movie ya watu wanaongea kifaransa yenye subtitles ya kiingereza halafu anajisifu siangaliii movie zilizotafsiriwa.
 
Unga tela, hama....
mi hawa ZUKU wamenichosha aswaa, kwenye king'amuzi chao hamna ITV, CLOUDS TV, CHANNEL TEN, STAR TV, zaidi ya TBC tu na wasafi sijui, kibaya zaidi kifurushi kikiisha uhoni chchote, nataka ninunue King'amuzi cha azam tu kwakweli
Najutaaa
 
Back
Top Bottom