Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,786
Wenye nyoyo ziliosononeka na sura za huzuni, Viongozi wa Wandamizi TFF, jana walijivisha ngozi ya kondoo kujumuika na Wazanzibari kusheherekea ushindi mkubwa walioupata kukubaliwa kuwa mwanachama wa CAF,
Viongozi hawa wa TFF na wengine wenye fikra za mgando wamezisahau kauli zao za kusikitisha na kukatisha tamaa kuwa Zanzibar haiwezi kuwa mwanachama wa CAF kwa vile Zanzibar si " nchi" kamili
Kauli zao leo zinawasuta na wanajaribu kuzilainisha kwa kusema kuwa uwakilishi wa Tanzania sasa umepanuka zaidi.
TFF walijisahau kujua kwamba Zanzibar katika nyanja nyingi ikiwemo soka inajuulikana zamani kuliko Tanganyika. TFF walijisahau kuwa Zanzibar inaheshimiwa na nchi nyingi barani Afrika na wanajua kinachoendelea kuhusu mustakabali wa Zanzibar ndani ya Muungano.
Leo Bendera ya Zanzibar inapepea mjini Cairo, Makao Makuu ya CAF na wimbo wa Taifa huru la Zanzibar utaanza kunguruma barani Afrika na watu kulazimika kusimama kwa heshima.
Hiyo ndio Zanzibar tuitakayo:Kwaheri Ukoloni,Kwaheri Uhuru Karibu Mamlaka Kamili!