Kwaheri rais Donald Trump

Licha la kudharau maelezo ya madaktari kutoka World Health Organisation kuhusu kulinda wananchi wake dhidi ya maradhi ya korona awali, pia vurugu na maandamano ya wanakundi la #BlacklivesMatter pamoja na #Antifa ndio sababu kuu ya kuregesha wana democratic party na mgombea wao Joe Biden ikuluni.
 
Huyu hajaikosa katika maishani mwake, matarajio yake yanatendeka vile anakuwa ameyatarajia. Sasa amesema Trump hatafaulu katika uchaguzi wa mwaka huu 2020.

Huyo Prof. anaweza kuwa sahihi au asiwe sahihi, Wamarekani saa nyingine akili zao wanazijua wenyewe tu mkuu. Sasa hivi jamaa ameanza kulizunguka Baraza la Congress kupitisha Executive Orders kwenye mambo ya kusaidia wapiga kura wenye hali mbaya kiuchumi; matatizo yaliyosababishwa na COVID-19.
 
Marekani sera yao ya nje ni ile ile, kutetea maslahi ya Marekani, hivyo sisi hatuna cha ku-gain hapo.

Wanaopiga kelele wanajisumbua bure tu. Sisi tuangalie ya kwetu ambayo eti bado tunaona fly overs kuwa ni vitu vya ajabu sana wakati umaskini unazidi kutamalaki.
 
Mkuu kwa sasa hivi tunaelewa kinachoendelea duniani kote, tukimuongelea Trump si kwa sababu katupa au katunyima misaada ni kwa sababu tunakiona kinachoendela huko. Tumeshasema hatutegemei misaada wala urafiki. Kujiondoa WHO ni kudhhofisha harakati za Afya duniani kote hatusaidii alikuwa anawajibika maana na sie tunatoa kinachotuhusu, kuvunja mikataba kama ule wa Iran na mataifa makubwa ni kuiweka dunia hatarini kwa mabomu hatarishi. HAFAI ANG'OKE. hatutaki misaada yake lakini marekani inaweza ikayumbisha dunia nzima kama itapoteza mwelekeo
 
😁😁

hata 2016 ilikuwa hivi hivi hakuna kipya.

Kwanza hio cnn ni wapishi wenye phd za kutunga habari feki.

Trump yupo kwajili ya kubaki mpaka 2024, Hili halina mjadala kabisa.

Ni kituko kisicho na kifani trump kuwa na mpinzani ambae ni mbaguzi na ana ugonjwa wa kusahau kiasi cha kudhani mtoto wake ni mke wake 😁.

Sababu inayopelekea media nyingi kumchukia trump ni kwamba trump yupo huru, haendeshwi afanye nini kama kina obama waliokazania kuhamashisha ushoga.

Trump ingekuwa ni enzi zile kabla ya smartphones basi mwaka huu angeshindwa kwasababu media kama cnn zingeaminisha watu wasimpigie kura trump, Ila katika kizazi hiki cha utandawazi ni vigumu sana kumzuia trump maana watu wanajua kuchambua mchanga na mchele.

Leo hii cnn inashika nafasi za chini kuzidiwa hata na channels za kawaida huko marekani, Chanel kama fox news ndio inayoongoza marekani na hawa fox news ndio media chache zisizo ripoti ama kupika habari chafu za trump na wanachi wameona waiweke kando cnn maana ni uchafu.

Trump 2020 hadi 2024 , Haipingiki hata ukichukia
 
Huyu hajaikosa katika maishani mwake, matarajio yake yanatendeka vile anakuwa ameyatarajia. Sasa amesema Trump hatafaulu katika uchaguzi wa mwaka huu 2020.
kwamba biden atashinda?....... joe biden huyu huyu anaeshindwa kuongea? mkuu ngoja tuone
 
Back
Top Bottom