Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa, wanaharakati, na jamii kwa ujumla kuacha kurejea matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ili kuruhusu Tume ya Rais kukamilisha uchunguzi wake bila upendeleo.