Kwa yeyote atayeguswa kunisadia

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,920
12,127
Wadau salaaam.

Ndugu zangu waswahili wanasema ''mficha maradhi kifo humuumbua''

Kwanza Mimi ni mwanachama wa JamiiForums tangu February 2013.
Mimi ni mhitimu wa shahada ya ualim ( Sanaa) mwaka 2015.

Kwa bahati mbaya nimetafuta kazi sijafanikiwa na hadi kufikia sasa hali tangu kiuchumi ni mbaya mbaya sana.

Nimefikiria mengi hasa kufanya biashara lakini nakwama kupata mtaji nimejaribu Kwa ndugu na jamaa nimekwama, nimetumia kila njia imeshindikana.

Nimeona niwashirikishe wenzangu humu jamvini ili Kwa yeyote atakayeguswa aweze kunisaidia namna ya kupata mtaji, ushauri na mawazo mbadala.

Kiasi cha mtaji kinachohitajika ni kuanzia 500,000 kwani nimeona niingie kwenye biashara ya nafaka ( mahindi).

Msaada huo uwe ni mkopo usio na riba , naweza kueleza mengi yakawachosha .

Nipo Mbeya na nipo tayar kujibu na kutoa information zozote ambazo itaonekana zimekosekana katika andiko langu.

Hali yangu kiuchumi inanichanganya mpaka nashindwa kuweka vizuri hoja zangu hapa.

Mungu awabariki.
 
Pole sana mkuu, vipi hukuweza kupata ajira ya serikali ama uliipiga chini make kiukweli kuna wakati kuna maeneo palikuwa hapafai kufanya kazi na kufanya wengine kuhama na wengine waliokataliwa kabisa waliamua kuacha kazi. Vipi hii kwako ikoje?

Nakupa pole lakini kwani hakuna fundi wa maisha
 
Mkuu tuliomaliza 2015 bado mpaka Leo hatujaajiriwa.
 
Njoo huku makongolosi, unisaidie kutoa felo kwenye shimo langu nitakupa mawe kidogo upate mtaji
 
Mwaka huu kilimo ni risk kubwa hasa Kwa mashamba yanayotegemea mvua
 
Naona hizi mada zinazidi kuongezeka kwa kasi humu jf......
Yaani unakuta mtu anaanza na kuelezea historia za kusikitisha...... Kisha ndipo anakuja kutaja shida yake kwenye umaliziaji.

Samahani kama nitamkwaza yeyote kwa mawazo yangu hasi.
 
Hongera kwa kuzidi kuzitatua changamoto zinazokupata, kuwa mhitimu wa chuo sio mchezo ni mtaji tosha kwa badae na sasa.

Pambana kiukweli hakuna mafanikio ya mkato na mara nyingi wenye kutoa msaada sio kama unavyoweza kuzani ni ngumu sana sio jambo rahisi mtu asiyekufahamu kukupatia ama kukukopesha pesa.

Naimani bado hujaweza Ku master mazingira unayoishi pia akili yako bado hujaisumbua zaidi.

Tambua kwamba pesa, furaha, Mali, utajiri, nguvu, afya vinapatikana katika sehemu saba
1.Kipaji
2.Mungu
3.Watu
4.Matatizo
5.Huduma
6.Kazi
7.Ubunifu na ugunduzi.
 
Usichoke nuombe muumba WA mbingi NHS Ardhi akupe wepesi utafanikiwa kisha ingia mtaoni name maifisi mashuleni utapata kama UKo freshi
 
Hongera kwa kuzidi kuzitatua changamoto zinazokupata, kuwa mhitimu wa chuo sio mchezo ni mtaji tosha kwa badae na sasa.

Pambana kiukweli hakuna mafanikio ya mkato na mara nyingi wenye kutoa msaada sio kama unavyoweza kuzani ni ngumu sana sio jambo rahisi mtu asiyekufahamu kukupatia ama kukukopesha pesa.

Naimani bado hujaweza Ku master mazingira unayoishi pia akili yako bado hujaisumbua zaidi.

Tambua kwamba pesa, furaha, Mali, utajiri, nguvu, afya vinapatikana katika sehemu saba
1.Kipaji
2.Mungu
3.Watu
4.Matatizo
5.Huduma
6.Kazi
7.Ubunifu na ugunduzi.
Kuomba pesa kwa watu sio jambo la staha ni bora kuomba kukopeshwa pia kufanya hivyo kwa watu usiowafahamu sio jambo la staha.....
Tumia njia zote lakini sio kuomba msaada ingali una maarifa kichwani.

Jitahidi kumaster jamii inayo kuzunguka kuna rafiki yangu amewah kumshawishi mmasai fulani mpaka akauza ngombe 2 na kumpatia pesa yote kisha akaenda zake Comoro kutafuta maisha.

Siamini kama matatizo ama Shida zaweza mfanya mtu adumae akili, binafsi napokuwa na madeni + matatizo mengi akili yangu kufanya kazi sana na hatimaye napata suluhisho.

Nina mikasa mingi sana lakini haka ka utamaduni ka kuandika atakayeguswa sio njia sahii, kuna wakati watu wanafikia ukomo wa kufikiri wawapo wazee lakini vijana kinachotusumbua sio kukosa mitaji ni TAMAA ya kuwa na maisha bora pasipo kuwa na MIKAKATI.

Kwa sasa badala ya wazee kuomba misaada vijana ndio tunaongoza kwa kuandika stori za maisha yetu pengine tuonewe huruma ni vema kujitahidi uonekane na sio ujioneshe ama ujitangaze.

UKWELI ni kwamba wenye matatizo na Shida mbali mbali ni wengi kuliko wasio nayo ama wenye ahueni.....hapa nazani nimeeleweka
 
Naona hizi mada zinazidi kuongezeka kwa kasi humu jf......
Yaani unakuta mtu anaanza na kuelezea historia za kusikitisha...... Kisha ndipo anakuja kutaja shida yake kwenye umaliziaji.

Samahani kama nitamkwaza yeyote kwa mawazo yangu hasi.
Hali ni mbaya ssna mtaani ndugu..
 
Elewa mtaji sio pesa tu,ykifikiria business halafu ukawaza mtaji hela utakwama,,,kukusaidia unaweza tumia maarifa uliyopata shule kupata mtaji,pili unaweza kutumia nguvu zako kupata mtaji na mwsho kwa yeyote ambae yupo HAI,na anavuta pumzi huo ni mtaji tosha kabsa.....
 
Back
Top Bottom