Kwa yeyote atayeguswa kunisadia

Kwa yeyote atayeguswa kunisadia

Hali ni mbaya ssna mtaani ndugu..
Kwa hili la ugumu wa kitaa, kweli nakubaliana na wewe Mkuu.
Lakini kwa dunia ya sasa ukweli no kwamba swala la imani kwa binadamu lime poromoka sana.
Pia kizazi hiki cha sasa kimetopea uvivuni kuliko zama zote tangu ilipo umbwa dunia.
 
Kuomba pesa kwa watu sio jambo la staha ni bora kuomba kukopeshwa pia kufanya hivyo kwa watu usiowafahamu sio jambo la staha.....
Tumia njia zote lakini sio kuomba msaada ingali una maarifa kichwani.

Jitahidi kumaster jamii inayo kuzunguka kuna rafiki yangu amewah kumshawishi mmasai fulani mpaka akauza ngombe 2 na kumpatia pesa yote kisha akaenda zake Comoro kutafuta maisha.

Siamini kama matatizo ama Shida zaweza mfanya mtu adumae akili, binafsi napokuwa na madeni + matatizo mengi akili yangu kufanya kazi sana na hatimaye napata suluhisho.

Nina mikasa mingi sana lakini haka ka utamaduni ka kuandika atakayeguswa sio njia sahii, kuna wakati watu wanafikia ukomo wa kufikiri wawapo wazee lakini vijana kinachotusumbua sio kukosa mitaji ni TAMAA ya kuwa na maisha bora pasipo kuwa na MIKAKATI.

Kwa sasa badala ya wazee kuomba misaada vijana ndio tunaongoza kwa kuandika stori za maisha yetu pengine tuonewe huruma ni vema kujitahidi uonekane na sio ujioneshe ama ujitangaze.

UKWELI ni kwamba wenye matatizo na Shida mbali mbali ni wengi kuliko wasio nayo ama wenye ahueni.....hapa nazani nimeeleweka
Mkuu ulicho sema ni ukweli maana vijana tumekuwa na tamaa kiasi cha kuhitaji ambavyo hatuna uwezo navyo
 
Binafsi nafahamu vizuri sana how it feels to be all alone and broke...
No shoulder to lean on na mambo kama hizo.
I know it ain't easy but keep your head up.
Through every dark night there's a brighter day!
 
Naona hizi mada zinazidi kuongezeka kwa kasi humu jf......
Yaani unakuta mtu anaanza na kuelezea historia za kusikitisha...... Kisha ndipo anakuja kutaja shida yake kwenye umaliziaji.

Samahani kama nitamkwaza yeyote kwa mawazo yangu hasi.

Upo right bro lakin hayo unayotafsiri kuwa ni historia ya kusikitisha ni vile tu lengo ni kujibu maswali tarajiwa.

In short hum tupo wengi hivyo mawazo ni mengi na Kwa upande wangu Mimi nimeleta mada hii Kwa lengo la kupata mawazo mbadala pia.

Sijaja direct nikitegemea kuna mtu atanipa pesa ndio maana unaona sijaweka popote namba ya M-Pesa ,tigo - pesa or bank account.

Thanks kwa ushauri wako pia.
 
Ni kweli him wengi hatufahamiani lakin uwezekano wa kufahamiana upo na ndio maana
Hapo nimeweka maelezo mengi Kwa target kwamba katika maisha tuna experience mbali mbali ambapo pengine mtu alishawah kukutana na hali kama hii yangu( ambapo Kwa sasa ni hali ya wengi) so mtu mwenye experience hii ni rahisi kuguswa na pengine kunpa uzoefu wake ili nami nijifunze. Ni ngum kuandika Kwa kifupi tu " Nahitaji mkopo usio na riba" then utegemee kupata mawazo tofaut.
 
Brother private zenyewe hazipatikani hasa Kwa sisi arts ndio maana naona suluhisho ni kujiajir hasa kwenye biashara
Daah pole mkuu,hapa nchini kuna shule nyingi sana ambazo raia aa kigeni na wasio na sifa hufundisha,Wizara ya mambo ya ndani (uhamiaji) wafanye msako mkali kukamata hawa watu,ili watanzania wenzetu wapate ajira..
 
Naona hizi mada zinazidi kuongezeka kwa kasi humu jf......
Yaani unakuta mtu anaanza na kuelezea historia za kusikitisha...... Kisha ndipo anakuja kutaja shida yake kwenye umaliziaji.

Samahani kama nitamkwaza yeyote kwa mawazo yangu hasi.
hahaaaaaaaaaa tukutane kwa mkemia tukupime damu kama ina mzigo....natania tu
 
Wadau salaaam.

Ndugu zangu waswahili wanasema ''mficha maradhi kifo humuumbua''

Kwanza Mimi ni mwanachama wa JamiiForums tangu February 2013.
Mimi ni mhitimu wa shahada ya ualim ( Sanaa) mwaka 2015.

Kwa bahati mbaya nimetafuta kazi sijafanikiwa na hadi kufikia sasa hali tangu kiuchumi ni mbaya mbaya sana.

Nimefikiria mengi hasa kufanya biashara lakini nakwama kupata mtaji nimejaribu Kwa ndugu na jamaa nimekwama, nimetumia kila njia imeshindikana.

Nimeona niwashirikishe wenzangu humu jamvini ili Kwa yeyote atakayeguswa aweze kunisaidia namna ya kupata mtaji, ushauri na mawazo mbadala.

Kiasi cha mtaji kinachohitajika ni kuanzia 500,000 kwani nimeona niingie kwenye biashara ya nafaka ( mahindi).

Msaada huo uwe ni mkopo usio na riba , naweza kueleza mengi yakawachosha .

Nipo Mbeya na nipo tayar kujibu na kutoa information zozote ambazo itaonekana zimekosekana katika andiko langu.

Hali yangu kiuchumi inanichanganya mpaka nashindwa kuweka vizuri hoja zangu hapa.

Mungu awabariki.
WEWE NI JINSIA GANI? UNA SEHEMU ANGALAU YA KUISHI? UKO MBEYA SEHEMU GANI? KWA SASA UNAJISHUGHULISHA NA NINI KINACHOKUSAIDIA KUPATA HATA SABUNI NA HII BANDO ILIYOKUWEZESHA KUWEKA HII THREAD? NI MASOMO GANI YA ARTS ULIYOSOMA? NAOMBA NIJIBU HAYO ILI NIENDELEE
 
Pole sana mkuu, vipi hukuweza kupata ajira ya serikali ama uliipiga chini make kiukweli kuna wakati kuna maeneo palikuwa hapafai kufanya kazi na kufanya wengine kuhama na wengine waliokataliwa kabisa waliamua kuacha kazi. Vipi hii kwako ikoje?

Nakupa pole lakini kwani hakuna fundi wa maisha
Nafikiri ww siyo mtanzania. Hujui knachoendelea Tz? Pole sana.
Watu tukisema ccm mbaya na haifai mnabisha.
Kamuulize malaika mkuu atakupa jibu.
Wanasemaga hapa kazi tu kumbe maigizo matupu. Uongozi bila hekima na busara ni mzigo tena wa mavi
 
hahaaaaaaaaaa tukutane kwa mkemia tukupime damu kama ina mzigo....natania tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
WEWE NI JINSIA GANI? UNA SEHEMU ANGALAU YA KUISHI? UKO MBEYA SEHEMU GANI? KWA SASA UNAJISHUGHULISHA NA NINI KINACHOKUSAIDIA KUPATA HATA SABUNI NA HII BANDO ILIYOKUWEZESHA KUWEKA HII THREAD? NI MASOMO GANI YA ARTS ULIYOSOMA? NAOMBA NIJIBU HAYO ILI NIENDELEE
TATIZO NDUGU YANGU UMETANGULIZA NGONO SANA.
Jinsia na kutoa msaada inahusika vipi? Watu tuliosoma psychology wala hatuangaiki kbsa. Ukisoma maelezo tu unajua huyu ni jinsia gani. Huyu ni mwanaume kwa taarifa yako.
Pole sana. Umeuliza maswali mengi lkn mengine ni pumba tu. Angalau maswali mawili ndiyo nimeona ya muhimu.
ULITAKA AKOSE HATA 500 YA KUNUNUA VOCHA? Mawazo km yako ndiyo wanayo viongoz wa sisiem. Hatari sana
 
POLE SANA KWA KUABUDU NGONO!!!! NILIPOMUULIZA JINSIA NILIKUWA NINA MAANA NZURI. MIMI NIKO MBEYA NA HAPA NILIPO KUNA KAZI ILA NI ZA KUTUMIA NGUVU SANA KIASI KWAMBA KAMA NI WA KIUME NINGEMUULIZA KAMA ATAWEZA. PIA KUMBUKA HATA KWENYE KAZI YOYOTE HASA HIZI ZA KUAJIRIWA LAZIMA JINSIA HUWA INAULIZWA TENA KWA NIA NZURI TU NA SI KWA MAANA MBOVU KAMA HIYO ULIYODHIHIRISHA WEWE!!!!
 
Usijari ndugu,, perception tumetofautiana , jamaa pia yupo sahihi Kwa upande Fulani . Hata Mimi naamini maswali yako yote hapo sawa kabisa.

Mimi ni Me
Masomo History & Kiswahili
Nipo Mbarali.
Sijaunga bundle natumia data bila malipo. (Www.free basics.com)
Sina shughuli yoyote maana mvua ni utata.
 
Kuomba pesa kwa watu sio jambo la staha ni bora kuomba kukopeshwa pia kufanya hivyo kwa watu usiowafahamu sio jambo la staha.....
Tumia njia zote lakini sio kuomba msaada ingali una maarifa kichwani.

Jitahidi kumaster jamii inayo kuzunguka kuna rafiki yangu amewah kumshawishi mmasai fulani mpaka akauza ngombe 2 na kumpatia pesa yote kisha akaenda zake Comoro kutafuta maisha.

Siamini kama matatizo ama Shida zaweza mfanya mtu adumae akili, binafsi napokuwa na madeni + matatizo mengi akili yangu kufanya kazi sana na hatimaye napata suluhisho.

Nina mikasa mingi sana lakini haka ka utamaduni ka kuandika atakayeguswa sio njia sahii, kuna wakati watu wanafikia ukomo wa kufikiri wawapo wazee lakini vijana kinachotusumbua sio kukosa mitaji ni TAMAA ya kuwa na maisha bora pasipo kuwa na MIKAKATI.

Kwa sasa badala ya wazee kuomba misaada vijana ndio tunaongoza kwa kuandika stori za maisha yetu pengine tuonewe huruma ni vema kujitahidi uonekane na sio ujioneshe ama ujitangaze.

UKWELI ni kwamba wenye matatizo na Shida mbali mbali ni wengi kuliko wasio nayo ama wenye ahueni.....hapa nazani nimeeleweka

Mkuu umemwaga madini muhim sana.

By the way Mimi mikakati ninayo ndio nipo kwenye njia sasa za kutafuta namna ya kuitekeleza.

Kuhusiana na maelezo mengi niliyoyatoa lengo hasa si nionewe huruma bali kuweka taarifa zote muhim kuhusu Mimi ili kupunguza misunderstanding.

Kingine ni kuwa hata Mimi sitegemei mtu ghafla tu anipe huo mkopo na ndio maana nikaeleza na mahali nilipo ili kama kuna mtu yupo jirani na nilipo na ana nafasi ya kunisaidia kivyovyote vile tuweze wasiliana hata kuonana.

Maelezo mengine niliyoweka pia yana lengo la kupata ushauri, kujulishwa sehem ninakoweza kupata hata kibarua Kwa mfano nineeleza ujuzi nilionao Kwa kulenga kuwa hata wamiliki wa shule za private ni member him.
 
Back
Top Bottom