Kwa yanayoendelea kwanini tusiamini kuna kichaka kimetengenezwa baadhi ya watu wa serikali kusaini makubaliano na DP World

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Amani iwe kwenu,

Nitangulie kwa kusema sijawahi kuihisi wala kuifikiri dhamiri isiyo njema ya Rais Samia kwa Tanzania, kila nikiamka asuhuhi namuombea kwa Mungu kwa sababu kuna kitu anacho na ndio hicho Tanzania inahikitaji isonge mbele nao ni uthubutu na maamuzi magumu.

Kwangu Rais Samia ni mzalendo wa kweli. Sisemi haya kwa lengo la kumsifia bali ni kwa lengo wa kumuonesha ni mtu wa namna gani na kwa nini sina wasiwasi wowote wa maamuzi yake kwa Tanzania ya sasa wala Tanzania ya kesho.

Niseme baadhi ya mambo machache yanayoendelea kujenga imani juu yake:

Kwanza kabisa, kuweka nia ya kuendeleza au kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Katiba ndio sheria kuu na Sheria mama na mabadiliko ya Katiba sio suala ndogo kwa nchi yoyote achilia mbali kuanzisha mchakato wa suala hilo upya maana yake muundo, mtindo na utaratibu mzima wa Uongozi ,utawala na utumishi kwenye Taifa unakwenda kubadilika either kwa uzuri au ubaya lakini siku zote mabadiliko yanayotegemewa ni yale chanya tu. Sasa kwa nini niwe na wasiwasi na mtu mwenye nia njema kiasi hiki?

Pili, kwenye utawala wake licha ya kwamba hajakaa sana madarakani lakini kuna maboresho makubwa ya Sheria mbalimbali yamefanywa. Maboresho yote yameliletea tabasamu pana na la muda mrefu Taifa. Hapa ndio Imani dhidi yake inaongezeka maradufu.

Tatu, Rais Samia ana kiu kuwa ya kutuletea maendeleo kwa kuhakikisha wadau mbalimbali wanashirikishwa. Kiu hii ndio inafanya serikali iingie ubia wa kiuwekezaji na taasisi mbalimbali ,Kama ubia ulioingia na kampuni ya DP WORLD.

Kwa hoja hizo tatu nikiri kusema imani yangu kwa Rais ni kubwa sana na nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kwamba Imani yangu ni haba au imenidanganya.

Makubaliano katika ya DP WORLD na Serikali si tu yataongeza mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Dubai bali yatachochea uchumi, uwekezaji na biashara. Kupitia kwa waziri Mbarawa tumeoneshwa faida nyingi za kukubali kushirikiana na DP WORLD kuliko kutokukubali.

Kwa uchache, bandari itaweza kuchangia mapato mpaka 67% kutoka 37% ya sasa, kutakuwa na kasi ya upakuaji mizigo bandarini na hivyo mzunguko wa biashara kuwa mkubwa na pia itasaidia kutengeneza ajira nyingi. Hizi faida zote si kwa ajili ya Serikali au kwa ajili ya Rais Samia pekee bali ni kwa kila mtanzania kwa sababu kuongezeka kwa mapato kutachochea maendeleo kwa haraka.

Lakini nasikitishwa na baadhi ya wanasiasa kulichukulia Jambo hili kisiasa kwamba "nchi inauzwa" na wengine wanasema "we are surrendering our sovereignty to Dubai". Hawa wote ni kwamba hawajuhi faida zitazopatikana kwa makubaliano hayo? Je, kuna faida gani Serikali kuingia makubaliano yenye kuitesa wenyewe? Kwamba nchi itakuja kuuzwa huku bado unafanyika uwekezaji wa kila namna, kwa hiyo tunataka mnunuaji aje anunue na uwekezaji unaofanyika?

Sifikiri kwamba hao wanaosema hivyo wana walau ufahamu wa nini wanasema kwa sababu wanaogea wasiyojua.

Au ndio tuamini kwamba kitendo hiki Cha kishujaa Cha Rais Samia kimeharibu baadhi ya mipango ya wapigaji pale bandarini?

Kwa sababu Jambo halijafanyika bado na faida au hasara hazijajulikana bado lakini makubaliano yanapingwa. Kwa nini? Kwa nini wasisubiri muda wa kupinga ufike?

Zaidi , kama nilivyosema namuamini Rais Samia sana pia niseme kwamba siamini yote yanayosemwa dhidi ya Rais Samia au serikali juu ya mkataba ila ni siasa tu zimejengwa kwenye suala hilo.

Mkataba sio Msahafu wala Biblia kwamba tuamini ni kweli ni wa milele au haiwezi kuvunjika makubaliano yanapokiukwa.
 
Mods rudisheni title iliyokuwepo tafadhali, isomeke hivi " Kwa yanayoendelea kwa nini tusiamini kuna kichaka kimeteketezwa Cha baadhi ya watu kwa serikali kusaini makubaliano na DP WORLD"
 
Mods rudisheni title iliyokuwepo tafadhali, isomeke hivi " Kwa yanayoendelea kwa nini tusiamini kuna kichaka kimeteketezwa Cha baadhi ya watu kwa serikali kusaini makubaliano na DP WORLD"
Uzalendo haupimwi kwa mazingaombwe hayo. Kwa huyu hapana. Ana mapungufu mengi mno. Katiba na marekebisho ya SHERIA hata goigoi anaweza fanya kwa msaada wa washauri wake.
 
Japo ulichoandika kinaeleweka na kina mantiki, lkn bado utaendelea kupingwa na lile genge au misukule ya wanasiasa uchwara, wakishirikiana na wakwepa kodi na wapiga madili pale bandarini.

Wengi wamekuwa wakiangalia kiongozi wangu wa chama kasema nini ili nimuunge mkono, hata kama huyo kiongozi wake amehongwa na nchi fulan ili kuididimiza nchi yetu iendelee kufanywa shamba la bibi na wasiokuwa wazalendo pale bandarini.

Haswa katika mambo yanayohusu vita vya kiuchumi vya bandari kati ya bandari Dar es salaam, Tanzania na Mombasa, Kenya.
 
Kwangu Rais Samia ni mzalendo wa kweli. Sisemi haya kwa lengo la kumsifia bali ni kwa lengo wa kumuonesha ni mtu wa namna gani na kwa nini sina wasiwasi wowote wa maamuzi yake kwa Tanzania ya sasa wala Tanzania ya kesho.
Mbona bandiko lako lote ni kusifia, au!
Kwanza kabisa, kuweka nia ya kuendeleza au kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Katiba ndio sheria kuu na Sheria mama na mabadiliko ya Katiba sio suala ndogo kwa nchi yoyote achilia mbali kuanzisha mchakato wa suala hilo upya maana yake muundo, mtindo na utaratibu mzima wa Uongozi ,utawala na utumishi kwenye Taifa unakwenda kubadilika either kwa uzuri au ubaya lakini siku zote mabadiliko yanayotegemewa ni yale chanya tu. Sasa kwa nini niwe na wasiwasi na mtu mwenye nia njema kiasi hiki?
ITAPENDEZA, ukieleza tatizo la muundo, mtindo na utaratibu mzima wa Uongozi, Utawala na Utumishi kwenye Taifa, kwa sasa, hoja yako iwe na nguvu
Pili, kwenye utawala wake licha ya kwamba hajakaa sana madarakani lakini kuna maboresho makubwa ya Sheria mbalimbali yamefanywa. Maboresho yote yameliletea tabasamu pana na la muda mrefu Taifa. Hapa ndio Imani dhidi yake inaongezeka maradufu.
Na hapa pia hoja yako ni ya ujumla, haina mifano kuthibitisha mabadiliko hayo yameleta faida gani.
Tatu, Rais Samia ana kiu kuwa ya kutuletea maendeleo kwa kuhakikisha wadau mbalimbali wanashirikishwa. Kiu hii ndio inafanya serikali iingie ubia wa kiuwekezaji na taasisi mbalimbali ,Kama ubia ulioingia na kampuni ya DP WORLD.
Unaamini maaendeleo ya nchi yataletwa na Wageni? Je, tatizo ni nini WaTz kushindwa kuendeleza bandari?
 
Mbona bandiko lako lote ni kusifia, au!

ITAPENDEZA, ukieleza tatizo la muundo, mtindo na utaratibu mzima wa Uongozi, Utawala na Utumishi kwenye Taifa, kwa sasa, hoja yako iwe na nguvu....
Tufike mahali tukubali tu kwamba kuna wenye uwezo zaidi yetu, kama tukishirikiana nao basi tutasonga mbele.

Sipingani na wewe kwamba tungewatumia watanzania lakini nawe ukubaliane na mimi kwamba Tanzania hatuna wawekezaji wakubwa wa kimkakati na hata hao wanaoitwa wakubwa sio wakubwa kivile kiasi cha kuchochea uwekezaji kwa haraka.

Sijasifia ila nimeelezea kwa marefu nia na dhumuni la serikali ambalo linapotoshwa
 
Nakubaliana nawe kuwa hatuna wenye mitaji mikubwa, je, hao wageni wanapata wapi mitaji kama siyo kwenye mabenki?

Juhudi za makusudi zichukuliwe kujenga uwezo wa WaTz kutekeleza miradi mikubwa. Serikali ikifanya hilo itakuwa "legacy" ya Awamu hii ya utawala.

Tunakopa, tunaomba misaada hadi utekelezaji wa miradi wakati nchi ni tajiri unaosombwa na hao wawekezaji.

Ni wakati sasa wa kuondokana na utegemezi
 
Amani iwe kwenu,

Nitangulie kwa kusema sijawahi kuihisi wala kuifikiri dhamiri isiyo njema ya Rais Samia kwa Tanzania, kila nikiamka asuhuhi namuombea kwa Mungu kwa sababu kuna kitu anacho na ndio hicho Tanzania inahikitaji isonge mbele nao ni uthubutu na maamuzi magumu...
Kwanini wanapewa bandari milele?
 
Back
Top Bottom