Kwa Wote Waliozaliwa DAR.....

Kwa Wote Waliozaliwa DAR.....

GAMBLER

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2009
Posts
303
Reaction score
12
Habari zenu..
Mimi nimezaliwa DAR, Sasa katika cheti changu cha kuzaliwa kwenye place of birth pamejazwa:- Dr K.K.Khan Maternity...nawaomba wana Jf wenye kujua hii sehemu iko wapi wanijuze ili niweze kwenda kuitembelea....ningeweza kuwauliza wazazi wangu lakini wametangulia mbele ya haki zamani
 
Hebu nenda pale Hindu mandal kwa nyuma kuna hospital ya dr Khan muulize mtu yeyote nenda kaulizie wanaweza kukusaidia...
 
DR K.K .KHAN MEDICAL SERVICES
P. O. BOX 78127
DAR ES SALAAM
+255 (0)22 2115759
+255 22 121552
+255 22 2126779

City Centre - India str.

DR K.K .KHAN MEDICAL SERVICES
P. O. BOX 78127
DAR ES SALAAM
+255 (0)22 2115759
+255 22 121552
+255 22 2126779

City Centre - India str.

Nadhani Ngoshwe hujakosea....ndiyo mtaa huo kama haijahamishwa/kufungwa au kubadilishwa jina.
 
Kwa hiyo wanaopajua kwa Dr. Khan ni wale waliozaliwa Dar tu?
 
Mwee!hicho cheti ulikipata zamani sana?siku zote ulikuwa wapi kuwauliza kutaka kujua?nenda hospitali yeyote ya serikali nadhani watakusaidia humu utapata porojo tu.
 
Mmmh jamani watu si makini eeh? kwa wote waliozaliwa Dar???? kupajua kwa dokta Khan kunataka mtu aliyezaliwa DAR.
Wengine wamezaliwa Dar wamekulia Kigoma wala hawajawahi kurudi Dar tena hivi wanaweza kukujibu swali hili? Mimi nilivyoona kwa wote waliozaliwa Dar basi nikajua labda kuna ishu inawahusu hawa watu specific kwasababu ndugu zangu wamezaliwa Dar basi nikakimbilia kuona kulikoni./.....kumbe!
Mix with yours
 
Hivi kuzaliwa Dar kumbe nako ni big deal?

Big Deal mkuu, hujasikia jamaa wanabishana "mi nimezaliwa Dar hunielezi kitu!!", si tunawaangalia tu, tunakuja toka mikoani tunatumia vitu vyao, tunawahamishia Ikwiriri.
 
Habari zenu..
Mimi nimezaliwa DAR, Sasa katika cheti changu cha kuzaliwa kwenye place of birth pamejazwa:- Dr K.K.Khan Maternity...nawaomba wana Jf wenye kujua hii sehemu iko wapi wanijuze ili niweze kwenda kuitembelea....ningeweza kuwauliza wazazi wangu lakini wametangulia mbele ya haki zamani

Hicho cheti cha kuzaliwa ulikiokota? Au umeenda mwenye kuchukua RITA? inaelekea umezaliwa kwenye late 80s! na utoto bado unakusumbua!
 
Hicho cheti cha kuzaliwa ulikiokota? Au umeenda mwenye kuchukua RITA? inaelekea umezaliwa kwenye late 80s! na utoto bado unakusumbua!

mzee hapo kwenye Bold upo sahihi sana, maana wa zamani wanazungumzia OCEAN ROAD AU "MAKUTI" PALE MUHIMBILI, KWELI NI UTOTO, MAANA KUPAJUA SEHEMU SIO LAZIMA UZALIWE HAPO,

HUYO DOKTA KHAN MWENYEWE HAJAZALIWA DAR LAKINI ANAPAJUA KWAKE (KWA DOKTA KHAN)
 
Back
Top Bottom