Kwa wenye uzoefu wa ufugaji wa kuku msaada

Legeza mwendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
519
Reaction score
655
Habari za kazi wakuu? Naomba niende straight kwenye point yangu, nimekua nikifuga kuku wa kienyeji kwa mwaka sasa lakini kuna tatizo nimelipata siku za karibuni baadhi ya kuku wanapasua mayai wanakunywa na kula maganda yake kama hiyo haitoshi pia kuna baadhi ya kuku wamekua wanataga mara mbili kwa siku (sikuwahi ona kabla) lakini kibaya ni lile yai la pili linakua tepe tepe sana halina ngozi ngumu na anapokua anataga huwa halali popote atakapo kuwepo ye anadondosha tu kama vile kuku wa kisasa, (sijawahi tumia egg booster)

Naombeni mnisaidie tatizo la hao kuku wanaokula mayai na hawa wanaotaga mara mbili hasa nifanyeje ili yai la pili liwe na ganda gumu.
 
Hongera kwa kupambana ktk ufugaji; hakuna kuku anaetaga mara mbili kwa siku wachunguze vizuri kuku wako. Kuhusu tatizo la kunywa mayai waweza kuwakata midomo hasa ile ya juu, na kwa habari ya mayai kuwa tepetepe nunua chokaa na dcp changanya na chakula chao unachowapa kama vile pumba au mashudu. Chokaa na dcp vyote utavipata katika maduka ya kilimo na mifugo. Kila la kheri!
 
Asante mkuu, nilichogundua anataga mara mbili kuna muda asubuhi kuna kuku nilimshuhudia akitaga, jioni hii nilipoenda kuwaangalia tena nimemshuhudia kwa macho yangu kuku yule yule akidondosha yai ila kwa sababu lilikua laini likapasuka, labda kama niliwachanganya, ila nashukuru kwa ushauri mkuu
 
Huyo alikuwa hatagi ni mimba ambayo alitakiwa ajifungue kesho yake ilikuwa inatoka kabla ya wakati kutokana na matatizo yaliyomletea uchungu wa kujifungua kabla ya wakati.
 
Wape mboga za majani na kabichi kwa wingi huko kunywa mayai wataacha na vilevile itawasaidia kutaga vizuri.
 
Wafugaji...nimeshangaa kuona kuku wangu aliyekuwa ana atamia mayai katotoa vifaranga baada ya kuatamia kwa siku 17!!!!kwangu limenishangaza...katotoa mapema zaidi ya hata kuku aliyeanza kuatamia kabla yake...imenishangaza!!je kuna mwenye experience kama hiyo?
 
Huyo atakuwa alianza kuatamia pasipo wewe kujua kuku huwa haatamii chini ya siku 21.
 
sababu ninazo zifahamu mimi ambazo zinasababisha kuku kula mayai ni mbili ambazo ni ikosefu wa madini ya kalisi na fosfolasi na sababu nyingine ni kuku kutaga sehemu yenye mwanga mwingi,kama kuna mdau anafahamu zingine anaweza ongezea.
ufumbuzi hapo si kuwakata au kuchoma midomo na sikushauri kufanya hivyo kwani ni ukatiri dhidi ya kuku,chakufanya tengeneza viota vya mayai eneo lisilo na mwanga mwingi ikiwezekana funika kidogo pia changanya mifupa iliyosagwa na d.c.p kwenye chakula chao.

usisahau kutupa mrejesho
 
Habari za kazi wakuu? Naomba niende straight kwenye point yangu, nimekua nikifuga kuku wa kienyeji kwa mwaka sasa lakini kuna tatizo nimelipata siku za karibuni baadhi ya kuku wanapasua mayai wanakunywa na kula maganda yake kama hiyo haitoshi pia kuna baadhi ya kuku wamekua wanataga mara mbili kwa siku (sikuwahi ona kabla) lakini kibaya ni lile yai la pili linakua tepe tepe sana halina ngozi ngumu na anapokua anataga huwa halali popote atakapo kuwepo ye anadondosha tu kama vile kuku wa kisasa, (sijawahi tumia egg booster)

Naombeni mnisaidie tatizo la hao kuku wanaokula mayai na hawa wanaotaga mara mbili hasa nifanyeje ili yai la pili liwe na ganda gumu.

soma hapa anzishaproject .com
 
Mkuu wengi hapo wamesha changia mimi nikiandika nitakua narejea kilicho semwa.
Ila cha kuongezea ni jitahidi sana usiwe unawapa stress au kuwashtua. Pia chakula chao wachanganyie vizuri kwa kufuata formula.
Zingatia maji safi

Ufugaji una changamoto mkuu jitahidi kuwa mvumilivu utakula matunda baadae
 
Je kama ndo unataka kuanza kufuga hao vyuku mtaji ni kama sh. Ngapi kuanzia banda had kuku wenyew
Pia ni aina gani ya kuku ni nzur
 
Back
Top Bottom