Stories of Change - 2022 Competition

Ak 47 super

Member
Sep 12, 2022
9
10
Kuku ni moja ya ndege wanaopatikana kwa idadi kubwa sana hapa nchini kwetu na hata duniani kote kwa ujumla,watu wengi wamekua wakifuga kuku kwa mazoea na sio kama biashara,hii imepelekea watu wengi kutokuona tija na faida katika ufugaji wa kuku.kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuku kwa kasi kubwa, ongezeko la watu na uhitaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na ufugaji wa kuku kuwa mkubwa sana katika ufugaji kuku ili kukidhi mahitaji ya soko.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku katika jamii yetu,hii imepelekea ufukaji wa kuku kuwa fursa kubwa sana inayoweza kuajiri watu wengi sana iwapo utafanywa kibiashara kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji.katika ufugaji wa kuku mfugaji anaweza kuvuna mazao mengi ambayo yanaweza kumpatia kipato, mfano mayai,mbolea, nyama na manyoya.bidhaa zote hizi zina soko nzuri sana kutokana na kuhitaji kwa kiwango kikubwa sana wakulima,watu wa migahawa na mahoteli,pia watu wa mapambo.

Ipo mifumo mingi ya ufugaji kuku kibiashara kutegemeana na uwezo wa mtu,eneo ulilopo,idadi ya kuku unayotaka kufuga na aina ya kuku unayotaka kufuga.uchaguzi wa mfumo wa kutumia katika ufugaji kuku inatakiwa uendane na malengo yako na mahitaji ya aina ya kuku unao taka kufuga,hii ni kutokana na kuwepo kwa aina mbalimbali za kuku na wenye malengo tofauti,mfano kuna kuku ambao ni wazuri kwa uzalishaji wa mayai(layer breed),kuku wazuri kwa uzalishaji wa nyama(broiler breed) na kuku wazuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama(dual purpose breed)
ifutayo ni mifumo inayoweza kutumika katika ufugaji wa kuku kibiashra.

1. Mfumo huria
Huu ni mfumo ambao kuku huachiwa kuzunguka kadri awezavyo katika mazingira bila kizuizi chochote ili kujitafutia chakula,mfumo huu hauna gharama kubwa sana katika ulishaji wa kuku kwa sabubu kuku hujitafutia mwenyewe chakula na kuitaji chakuta kidogo tu cha ziada.hasara za mfumo huu ni uhitaji mkubwa wa eneo la ufugaji,usalama wa kuku ni mdogo pia mfugaji hawezi kukusanya mbolea itokanayo na kuku kirahisi na hivyo kuwafaa zaidi wayu walio vijijini sehemu zenye maeneo makubwa ya ardhi yaliyo wazi.

2. Mfumo wa nusu huria
Katika mfumo kuku wanafugwa katika eneo ambalo linakua na sehemu mbili,semehu ya kwanza ni nyumba iliyoje gwa vizuri kwajili yao na sehemu ya pili ni eneo la wazi lililozungushiwa uzio hiyo kuku hupewa chakula na maji na mfugaji kwa kiwango kikubwa na kiasi kidogo hujitafutia wenyewe katika eneo lao lililozungushiwa uzio,mfumo huu ni bora zaidi kuliko mfumo huria kutokana na eneo la mfumo huu kua na uzio hivyo kurahisisha ukusauaji wa mbolea ya kuku pia na usalama wakuku ni mkubwa.

3. Mfumo ndani
Huu ni mfumo wa ufugaji ambao kuku hufugiwa ndani mda wote,mfumo huu ni hutumika zaidi maeneo yaliyo na upugufu wa ardhi na idadi kubwa ya watu,mfano mijini,mfumo huu ni mzuri sana maana usalama wa kuku ni mkubwa zaidi na nirahisi kukusanya mbolea hata mayai.

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU
Kuna faida nyingi sana za ufugaji wa kuku ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo
1.chanzo cha kipato kwa mfugaji kupitia uuzaji wa mayai, mbolea ya kuku na kuku wenyewe.

2.husaidia kupunguza gharama za ununuzi wa mbolea za viwandani kwani mfugaji anaweza kupata mbolea mbadala kwa kutumia kinyesi cha kuku.

3. Ni chanzo kizuri cha mboga kwa familia,kwani kupitia ufugaji wa kuku mfugaji atapata nyama na mayai kwajili ya kula na familia,ni chanzo kizuri cha madini na vitamini kwajili ya afya zetu.

5. Chanzo cha ajira kwa watu wa rika mbalimbali,kutokana na ufugaji wa kuku inaidia watu wengi kujiajili na kuajili wengine kwa kufanya shughuli mbalimbali zinazohusu ufugaji wa kuku,mfano ulishaji wa kuku,kuuza nyama na mayai,kuuza vyakula vya kuku na usimamizi wa mashamba ya kuku.

CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA KUKU
Kumekuwa na changamoto nyingi sana katika ufugaji kuku, lakini changamoto kubwa zaidi kwa wafugaji wa kuku ni mangonjwa,wafugaji wengi wana shindwa kuendelea na ufugaji wa kuku kutokana na kukumbwa na magonjwa katika ufugaji wao wa kuku lakini changamoto hii inaweza kuepukika iwapo mfugaji atafuata taratibu za ufugaji bora na wenye tija ikiwa ni pamoja na kuzingatia utaratibu wa utoaji wa chanjo kwa wakati na utaratibu maalumu.mfano tumia ratiba ifuatavyo kutoa chanjo kwa kuku wako ratiba hii ya chanjo inawafaa kuku wanao andaliwa kwajili ya kuzalisha mayai (layer).

Siku1-3 chanjo ya mahepe(marek's)
Siku 7 chanjo ya kideri(mdondo)
Siku 14 chanjo ya gumboro
Siku 21chanjo ya kideri(mdondo)
Siku 28 chanjo ya gumboro
Siku 35 chanjo ya ndui

Rudia chanjo ya kideri kila baada ya miezi mitatu
Hizo ni baadhi ya chanjo muhimu kwa kuku ambazo zita wakinga na mangonjwa hatarishi kuku wako.

UTARATIBU WA ULISHAJI WA KUKU
Utaratibu wa ulishaji kuku hutegemea sana aina ya kuku husika,huu utaratibu kwa kuku wanao andaliwa kwajili ya mayai.

Wiki 1-8 wape kuku wako chakula cha vifaranga (chick starter feed).

Wiki 9-18 wape kuku wako chakula cha kuku wanaokua(grower feed).

Wiki 19 na kuendelea wape kuku wako chakula cha kuku watagaji (layer feed).

Katika utaratibu huu unaweza kuandaa chakula mwenyewe au ukanunua chakula cha kiwandani moja kwa moja kulingana na upatikanaji wake katika eneo husika. Angalizo kama huna ujuzi wa kuanda chakula ni vizuri ukinunua chakula cha kiwanda kwa matokeo bora zaidi.

Karibuni tufuge kuku,tuinue vipato vyetu,tujenge uchumi wetu na taifa letu
 
Kuna aina nyingi zinazo weza kufugwa kwa mfumo huo ila hizi ni baadhi tu,
1.tanbro
2.kuroiler
3.kenbro
4.kienyeji
 
Asante sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom