duh mkuu,mbna darasa limekuwa gumu? mi mekwambia maji ambayo ni sample ya maji ya kisima.[/QU
hapo no adjustiment coz maji ya kisima hutegemea sana source.
duh mkuu,mbna darasa limekuwa gumu? mi mekwambia maji ambayo ni sample ya maji ya kisima.[/QU
hapo no adjustiment coz maji ya kisima hutegemea sana source.
ok.huwez fanya adjustiment since maji ya kisima hutegemea sana source
Mkuu ninapozungumzia seasonal variation nina maanisha kipindi cha kiangazi na masika. Kama unavyofahamu kipindi cha masika mvua huwa zinanyesha sana na kima cha maji huwa kinaongezeka kutokana maji kupenya ardhini (infiltration), Sasa kama maji ya mvua yataongezeka na huenda haya maji yakawa ni acidic rain (sulphuric acid-H2SO4 au Nitric acid-HNo3). Kwa faida ya wengine acidic rain inasababishwa na deposition of chemicals (kama sulphate-So4, carbondioxide-Co2, Nitrogen gas etc) kwenye anga (atmosphere). Hizi gesi/chemicals angani linasababishwa na shughuli zetu za kila siku kama moshi wa magari, kuchoma misitu, moshi wa viwandani n.k na matukio ya asilia kama volcano.Mkuu unaposema seasonal variation unamaanisha nn?na umegusia hali Ya hewa nayo npe maelezo yke kvp?na kvp soda Ash (Naco3)huondoa minerals contents?nifahamishe hpo km cjaelewa!Asante
Mheshimiwa asante sana kwa ushauri wako. Naona kuna vitu unavijua pasipo shaka sasa pls nimashine zipi ambazo ni nzuri especially zisizosumbua.Wazo zuri lakini kuna mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyazingatia na kuyafahamu kabla ya kuanza.
Kwanza kabisa unatakiwa kuchagua eneo ambalo unataka kuanzisha hiyo firm yako.
Ukishapata pata eneo kabla ujaanza shughuli yoyote shauriana na wataalam mchague chanzo cha maji kulingana na ukubwa wa kiwanda.
Mkishakubaliana kama ni kisima, tafuta wataalam wa geology ili waweze kupima eneo husika kujua kama maji yanapatikana ktk eneo husika. Kama yanapatikana kwa kiasi kinachofaa unaweza kuanza kuchimba kisima halafu na kuchukua sample ya maji ili kupima mineral content zilizomo (hii itakusaidia kujua mfumo wa kutibu maji kulingana na quality of raw water yako).
Baada ya hapo Pima discharge rate uangalie kisima kinaweza kutoa maji lita ngapi kwa siku na uangalie uwezekano wa maji kukauka au kupungua hasa kipindi cha kiangazi ili usije kuanza halafu baada ya muda kisima kikakauka.
Baada ya hatua zote izo unaweza kujenga jenga kama godown ambalo utaligawa sehemu muhimu: sehemu ya kutibu maji, sehemu ya packaging, sehemu ya kutengenezea chupa, store na sehemu ya ofisi.
Katika Chumba cha kutibu maji tuweka raw water storage tank, filters (sand &'carbon), NF, RO, ozone machine, pure water storage tank... Kwenye hiki Chumba utafungiwa mfumo ambao ni computerised (self operating) kwa hiyo hiki Chumba kitahitaji mtu mmoja au wawili kwa kazi ya operation, data reading na kuadd chemicals kama Antiscalant & pH regulator.
Chumba cha packaging utafunga pia machine zote muhimu kwa ajili ya bottle cleaning, water filling & caping, bottle printing (priniting machine especially expire date), na machine kwa ajili ya kupack chupa za maji pamoja kama dazani 1.
Chumba kwa ajili ya kutengeneza chupa na cap kitakuwa na machine zake na umbo na size ya chupa unazotaka.
Uwe na store pamoja na ofisi na gari aina ya canter kwa ajili ya kusambazia maji.
CHANGAMOTO
Changamoto kubwa katika kiwanda ni kuharibika kwa baadhi ya part ktk machine. Mara nyingi machine za chumba cha packaging ndio zinasumbua Mara kwa Mara mfano printing machine ikihalibika tu hamwezi kupack maji maana yenyewe ndio ina print expire date kwenye chupa za maji (uwezo kuuza maji bila ya kuwa na expire date).. Mara nyingi hii machine hua inasumbua.
Kwa hiyo utapokuwa una nunua machine nunua na spare parts za muhimu in case tatizo likitokea unafunga mwenyewe badala ya kuagiza. Kuna baadhi ya spare parts unakuta kuna duka 1 tu ndio linauza (kariakoo), na bei zao ziko juu yaani kifaa ambacho ukikiagiza mpaka kinafika inaweza kukugharimu laki 9 lakini wao wanauza milion 7. Kwaiyo ni vizuri kuwa na baadhi ya spare parts.
Kuhusu kufunga machine, watakao kuuzia machine ndio waje wakufungie ili kuepuka shida yoyote itakayojitokeza wakati wa ufungaji. Lakini pia unapaswa kuwa na mtaalamu ambaye atapata maelekezo kutoka kwa hao waliokuuzia ili kufahamu jinsi ya kufanya maintenance na kutatua common problems.
Bei ya vifaa inategemeana na campun utakayonunua ila wachina wako cheap sana kuliko makampun mengine.
NB:hakikisha unapata vibali vyote muhimu kwanza kabla ya kuanza kujenga
ÑaombA kuwasilisha... Kwa msaada wowote usisite kuniuliza
Mkuu nimesema MARA NYINGI MAJI YA KISIMA (UNDERGROUND WATER) YANAKUWA NA PH BELOW 6. Nimesema hivi kwa sababu ukichukua sample ya maji ya kisima (underground water) kabla haijapita kwenye treatment yoyote Mara nyingi pH yake inakua acidic in nature (below 7), lakini haina maana ya kwamba maji yote ya kisima lazima pH iwe acidic.Sasa umejibu vizuri mkuu,sikuwa nmekuelewa ile mwanzo uliposema sodium carbonate inaremove minerals,ndo maana nikaomba ufafanuzi,na ulichokieleza hpo ndo kazi kubwa ya soda Ash,lakin pia umesema raw water ina pH below 6?hpo sikuungi mkono,n afikiri ni treated water kwa maana y maji yaliyotoka katika RO ndo huwa n pH around 6,na ndio maana ata iyo soda Ash uwekwa after treated water n siyo before kwa maana kwenye raw water!